Njombe man-eaters: Simba waliokula zaidi ya watu 1500 Kusini mwa Tanganyika 1932-1947

Njombe man-eaters: Simba waliokula zaidi ya watu 1500 Kusini mwa Tanganyika 1932-1947

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
maxresdefault.jpg
Je umewahi kusikia historia kuhusu Njombe man-eaters?
Neno "man-eaters" limetoka kwa Kiingereza na maana yake kuu ni wanyama wala watu, yaani mnyama ambaye amejifunza au kuzoea kuwinda na kula binadamu kama chakula chake.
Moja ya visa vikubwa duniani vya wanyama kula watu ni kisa cha Man eaters of Njombe ambao walikuwa ni simba wa familia moja/ pride moja waliowafanya binadamu kuwa chakula chao kikuu

Njombe ilikuwa wilaya ambayo inapatikana Kusini Magharibi mwa Tanganyika (leo hii Tanzania). Miaka ya 1930s kulikuwa na mlipuko wa ugonjwa wa rinderpest kwa wanyama, ugonjwa huu ulipelekea vifo vya wanyama wengi sana ambao walikuwa chakula kikuu cha simba. Pia inasemekana Waingereza walikuwa wanaua wanyamapori wengine ili kuzuia ugonjwa kusambaa kwa kasi, hali iliyopelekea simba kukosa chakula.

Simba wengi walikufa kwa njaa, lakini sio Njombe man-eaters. Pride hii ya simba iligundua kuwa kuna alternative ya chakula mbali na nyati, swala, pundamilia nk. Walianza kula binadamu kama chakula chao kikuu. Walikuwa wakivamia vijiji mbalimbali vya wilaya ya Njombe na kula watu kila siku.

Simba hao waliogopwa sana hadi wanakijiji wakawa wanaogopa hata kuwaongelea. Wengi waliwahusisha na ushirikina. Pia walikuwa wanaweza kuvamia kijiji kimoja hadi mara 2 kwa siku. Walikuwa na akili sana na walikuwa wanawinda kwa ushirikiano, kwa mfano simba mmoja akivamia ndani ya nyumba wengine walikuwa wanaizunguka nyumba kwa nje, kwa hiyo mtu akifanikiwa kukimbia ndani anakutana nao wengine kwa nje.

Familia hii ya simba ilikula watu takribani 1500 kuanzia mwaka 1932 hadi 1947 na walikuwa hawabagui, walikuwa wanakula wanawake, wanaume mpaka watoto. Pia simba wadogo waliozaliwa kwenye hii pride walijifunza kuhunt binadamu kutoka kwa wazazi wao. Wali learn na kuadopt na kuona binadamu kama their normal prey

Mwisho wao ulifika. Mwindaji mmoja kutoka Uingereza aliyefahamika kwa jina la George Rushby, alianza mission ya kuua simba mmoja baada ya mwingine akishirikiana na wanakijiji hadi walipofanikiwa kuua simba wa mwisho. Baada ya kutokomeza hii pride ya simba, matukio yakaisha na vijiji vikabaki salama

Mpaka leo Njombe man-eaters wanabaki kuwa one of the deadliest man eaters to ever exist. Man eaters wengi walioacha historia ni tigers na leopards vijijini huko India, mamba wa Lake Tanganyika anayefahamika kwa jina la Gustave ambaye anahusika na vifo vya watu 300 mto Ruzizi-Burundi na Man-eaters of Tsavo ambao walikuwa simba dume wawili waliokula watu zaidi ya 135 huko Tsavo nchini Kenya miaka ya 1898 wakati wa ujenzi wa reli ya Kenya-Uganda

Ukitaka kujua kiundani kuhusu Njombe Man eaters unaweza kusoma articles za National Geographic au Wikipedia, wameelezea vizuri. YouTube nako kuna video kadhaa kuwahusu
Pia kuna documentary full kuhusu Njombe man-eaters

_____
Tanzania Terror

Njombe man-eaters - Wikipedia
 
Wakati nipo mdogo kwa kuongopewa na ninavyoona kwenye TV nilidhani simba ni size ya mbwa labda.

Siku niliyomuona kwa mbali nikasema okay hata mkikutana live ile stori sijui mkazie macho haisaidii kwakua anaweza kukutia kibao akang'oa kichwa.
 
Simba ni wakubwa sana. Binafsi nikikutana nae uso kwa uso sijui kama nitapata ujasiri wa kutazamana nae kama wanavyosema
 
Wakati nipo mdogo kwa kuongopewa na ninavyoona kwenye TV nilidhani simba ni size ya mbwa labda.

Siku niliyomuona kwa mbali nikasema okay hata mkikutana live ile stori sijui mkazie macho haisaidii kwakua anaweza kukutia kibao akang'oa kichwa.
Sasa kuna wanyama kama tigers ambao ni wakubwa na wana nguvu kuliko simba. Sema tu huku Africa hatuna
 
Mmmh simba na Njombe wapi na wapi?ni sawa na kungoja tren Airport
 
Mmmh simba na Njombe wapi na wapi?ni sawa na kungoja trend Airport
Actually miaka ya 1930s Tanzania (Tanganyika then) ilikuwa na wanyamapori wengi kuliko sikuhizi. Leo hii Njombe hadi Ruaha ambayo ndio hifadhi ya taifa yenye simba wengi zaidi Africa ni km 284. Miaka ya nyuma wanyamapori walisambaa zaidi maeneo mengi kuliko leo.
That's why hii ni verified story ambayo ipo hadi Wikipedia na website ya National Geographic. It means ni documented history, sio tu story za vijiweni

View: https://youtu.be/ih4iOQVfR9A?si=3Y9pZSci-OAWI2cT
Screenshot_20260823-213009.png
 
View attachment 3655784

Okay,nilidhani simba wanaishi savanna kumbe hata kwenye baridi kali wanaweza ishi!.shukrani
 
Okay,nilidhani simba wanaishi savanna kumbe hata kwenye baridi kali wanaweza ishi!.shukrani
Njombe ni Savanna tu, ok Kuna 'baridi kama tukilinganisha na maeneo mengi ya Tz, lakini sio baridi inayoweza kubadili uoto wa asili na wanyama....Baridi kama hizo utazikuta Maeno ya bara la Ulaya na America, ambapo kipindi cha baridi joto linafika -10, -15 na theluji huanguka, sehemu kama Urusi joto linafika Hadi -50

Njombe baridi Kali kabisa inagika nyuzi 5 au 6, hajawahi kufika zero
 
Afu mtu anakwambia ati masai haogopi simba cjui anaweza kumshika kwa mikono yake. Mda mwingne nikiwaambia kuwa wanyama wote n wa kula nyama ili tulipize mnasema ati nyago zimeshka. Hiyo miaka sikuwepo lakin walioliwa na simba ntasema ni uzembe wao, yaan jitu haliongei ati nisimame hadi linifikie, uongo. Mim kusema ukweli hata kama ni mbuzi akileta ujinga wa kujifanya anataka kupgana vihedi na watoto huyo ni mboga direct. Mda mwingne uoga unasaidia sana.
 
Actually miaka ya 1930s Tanzania (Tanganyika then) ilikuwa na wanyamapori wengi kuliko sikuhizi. Leo hii Njombe hadi Ruaha ambayo ndio hifadhi ya taifa yenye simba wengi zaidi Africa ni km 284. Miaka ya nyuma wanyamapori walisambaa zaidi maeneo mengi kuliko leo.
That's why hii ni verified story ambayo ipo hadi Wikipedia na website ya National Geographic. It means ni documented history, sio tu story za vijiweni

View: https://youtu.be/ih4iOQVfR9A?si=3Y9pZSci-OAWI2cT
View attachment 3655784

Ni kweli hadi Dar kulikuwa na Simba wengi tu ,Gezaulole watu waliliwa na simba sana ,ukienda Mwasonga simba nje nje miaka ya 80s ,Mwandege Kongowe miaka ya 90 simba unawasikia wakiunguruma Usiku ,Ukienda Mingoi Kerege Vikawe Simba nje nje.

Wanyama pori wameisha sana na ni moja ya endandered species....Miaka ya mbele vizazi vyetu vitakuja kuona kwenye picha tu na video kama sisi tunavyoona Dayanasori.
 
Kwa sababu ya ujangili wanyamapori wamepungua sana. Sasahivi dunia nzima ina simba 20000 tu na katika hao 14000 wapo Tanzania, maeneo mengine yaliyobaki yanashare hao simba 6000

Lakini kwa sababu ya juhudi za conservation miaka ya karibuni wanyamapori taratibu wanaanza kuongezeka. Miaka ijayo tutakuwa na wanyamapori wengi zaidi perhaps mbeleni sana tutarudi kwenye ile idadi tuliyokuwa nayo miaka ya 1900s
 
Kwa sababu ya ujangili wanyamapori wameoungua sana. Sasahivi dunia nzima ina simba 20000 tu na katika hao 14000 wapo Tanzania, maeneo mengine yaliyobaki yanashare hao simba 6000

Lakini kwa sababu ya juhudi za conservation miaka ya karibuni wanyamapori taratibu wanaanza kuongezeka. Miaka ijayo tutakuwa na wanyamapori wengi zaidi perhaps mbeleni sana tutarudi kwenye ile idadi tuliyokuwa nayo miaka ya 1900s
Kumbe tuna Simba wengi sana!!
 
Kumbe tuna Simba wengi sana!!
Tunao wengi sana, dunia nzima ndio tunaongoza
Ruaha National Park pekee ina simba 2000 hadi 3000 sawa na zaidi ya asilimia 10 ya simba wote duniani, Kiufupi population ya simba waliopo Ruaha pekee ni sawa na idadi ya simba wote nchini Kenya
 
Mmmh simba na Njombe wapi na wapi?ni sawa na kungoja tren Airport
Hii nchi huko nyuma ilikua mbuga za wanyama,mpaka 1990s tabora pembezoni tu ya mji tuliwinda digidigi,sungura,nsha,siku hizi hata kwale hakuna,tunaoneshwa maeneo jirani tu na mji palikua na Simba,siku hizi ni fisi na bweha tu
 
Back
Top Bottom