Njombe marufuku kula nyama ya nguruwe.

Njombe marufuku kula nyama ya nguruwe.

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
images(1).jpg



Serikali Wilayani Ludewa Mkoani Njombe imepiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe, kuingiza mfugo wa Nguruwe pamoja na kutumia mazao yoyote ya Nguruwe ikiwemo Damu, samadi, mifupa na nywele kwa muda usiojulikana isipokuwa kwa idhini ya Daktari wa mifugo wa Wilaya hyo.

Taarifa iliyotolewa na Daktari wa mifugo wa Wilaya hiyo Dkt. Festo Mkomba imeeleza yafuatayo "kwa Mamlaka niliyopewa na sheria ya mifugo namba 16 (2),17 ya mwaka 2003, kuanzia leo tarehe 15/03/2023 natangaza kwamba Wilaya ya Ludewa itakuwa chini ya Karantini mpaka hapo itakavyotangazwa vinginevyo hii ni kutokana na matukio ya ugonjwa wa homa ya Nguruwe kujitokeza katika Wilaya ya Ludewa"

Taarifa hiyo imeeleza kuwa adhabu kali itatolewa kwa mujibu wa sheria kwa yeyote atakayekiuka masharti yaliyotolewa kutokana na uwepo wa ugonjwa huo wa homa ya Nguruwe.

Source: MillardAyoUPDATES
 
Je vipi wale wanyama waliosafirushwa kutoka hapo Ludewa kwenda miij mingine kuliko na wapenzi bashasha wa hiyo kitu pendwa kama Darnes Salaam.
Mmefuatilia na hilo na pia mmekataza kusafirisha au ni ulaji tu wa hapo Ludewa!?

Umakini zaidi ulitakiwa nchi nzima si ajabu umeshatapakaa.!
 
Back
Top Bottom