Njombe: Mtoto ajiua baada ya kufokewa na baba yake

Njombe: Mtoto ajiua baada ya kufokewa na baba yake

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mtoto mmoja Wilayani Makete mkoa wa Njombe amekutwa amefariki kwa kujiua kutokana na kunywa sumu baada ya kuonywa kwa kufokewa na Baba yake aliyekuwa akimuonya baada ya kuwaacha punda waliokwenda kula mazao kwenye shamba la Watu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Mtoto huyo aliacha punda aliokuwa nao machungani na kwenda kucheza na Watoto wenzake hali iliyomfanya Baba yake kumuonya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwenye shamba.

“Huyu Mtoto alipewa punda akachunge, akawaacha na akaenda kucheza na matokeo yake wale punda wakala shamba la Mtu, Mzee wake akalalamikiwa ndipo akamuita Mtoto lakini kitendo cha Mzee kumfokea yule Mtoto achunge punda kwa umakini, yeye akachukua maamuzi magumu akatafuta sumu akanywa na kufariki”

Kamanda Issah ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutafuta njia sahihi ya kuzungumza na Watoto huku pia akiomba Makanisa na Misikiti kuendelea kutoa mafunzo mema ya dini Kwa Watoto ili kutokuwa na maamuzi magumu.
 
Kina Juniaa haoo

Zamani tulipo kuwa wadogo ukifanya kosa wazazi walikuwa wana tunafokea na kipigo juu lakin mtu unaona kawaida tuu na maisha yanaendelea na unajirekebisha sijui hivi vitoto vya sasa hivi vinajikuta ni akina nani havitaki kuonywa..
 
Thubutuu !!! Junia achunge punda ? Junia aishi Njombe !!!! Kina junia wapo Daslamu, Arusha, na Mwanza kidogoo maeneo ya Isamilo na capripoint
 
Lazima alikuwa na tatizo la muda mrefu. Kugombezwa siku moja kusingesababisha ajiue
Mtoto kujiua kwa kukaripiwa kidogo ni mtihani ila hiki kizazi kipya kipo na utambuzi na uhuru wa kuongea na kujiamlia mambo yao wenyewe.

Zamani mtoto unadanganywa kuwa mama katoka kununua mdogo wako hospitali na unakubali ila juzi kati kitoto cha jirani hata shule akijaanza kinamuambia mama ake amzalie mdogo wake

Sijui approach gani sahihi itumike
 
Mtoto kujiua kwa kukaripiwa kidogo ni mtihani ila hiki kizazi kipya kipo na utambuzi na uhuru wa kuongea na kujiamlia mambo yao wenyewe.

Zamani mtoto unadanganywa kuwa mama katoka kununua mdogo wako hospitali ila juzi kati kitoto cha jirani hata shule akijaanza kinamuambia mama ake amzalie mdogo wake

Sijui approach gani sahihi itumike
Tatizo ni sisi wazazi na sio watoto.
 
Kina Juniaa haoo

Zamani tulipo kuwa wadogo ukifanya kosa wazazi walikuwa wana tunafokea na kipigo juu lakin mtu unaona kawaida tuu na maisha yanaendelea na unajirekebisha sijui hivi vitoto vya sasa hivi vinajikuta ni akina nani havitaki kuonywa..
Ni genes genetic issues wenyeji wa huko wanapendaga kujiua
 
Hakuna mtu anaehoji hizi statement za kienyeji za polisi wa kibongo?

Amekunywa sumu gani?

Aliipata wapi ?

Wamejuaje kainywa mwenyewe ?

Kwa nini wanachukua statement za Baba kama zilivyo wakati huyu ndio suspect number one ???

Nchi zilizoendelea suspect namba moja ni aliyemwona marehemu mara ya mwisho au aliyeripoti kifo au closest family members.

Pelekeni polisi, waandishi na waganga nje wakasome au wawekeeni films za Forensic Files, 48 Hours, CSI, Criminal Scene Investigation.

What if baba kampiga fimbo ya kichwa mtoto akaanguka mazima baba akakimbilia polisi na mchongo wa sumu ? Think a bit deeper guys.
 
Back
Top Bottom