Njombe: Mtoto ajiua baada ya kufokewa na baba yake

Njombe: Mtoto ajiua baada ya kufokewa na baba yake

Kamanda Issah ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutafuta njia sahihi ya kuzungumza na Watoto huku pia akiomba Makanisa na Misikiti kuendelea kutoa mafunzo mema ya dini Kwa Watoto ili kutokuwa na maamuzi magumu.
Wanawakubali wakitoa mafunzo kwa watoto na siyo kwa askari ambao wamekithiri kwa rushwa, ubambikiaji kesi, kuwazonga watumishi wa Mungu wanapoikosoa serikali na dhuruma kwa raia
 
Hakuna mtu anaehoji hizi statement za kienyeji za polisi wa kibongo?

Amekunywa sumu gani?

Aliipata wapi ?

Wamejuaje kainywa mwenyewe ?

Kwa nini mchukue statement za Baba wa mtoto kama zilivyo wakati huyu ndio suspect number one ???

Nchi zilizoendelea suspect namba moja ni aliyemwona marehemu mara ya mwisho au aliyeripoti kifo au closest family members.

Pelekeni polisi, waandishi na waganga nje wakasome au wawekeeni films za Forensic Files, 48 Hours, CSI, Criminal Scene Investigation.

What if baba kampiga fimbo ya kichwa mtoto akaanguka mazima baba akakimbilia polisi na mchongo wa sumu ? Think a bit deeper guys.
Hizo gharama zote za ufatiliaji wewe utatoa?
 
Mtoto mmoja Wilayani Makete mkoa wa Njombe amekutwa amefariki kwa kujiua kutokana na kunywa sumu baada ya kuonywa kwa kufokewa na Baba yake aliyekuwa akimuonya baada ya kuwaacha punda waliokwenda kula mazao kwenye shamba la Watu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Mtoto huyo aliacha punda aliokuwa nao machungani na kwenda kucheza na Watoto wenzake hali iliyomfanya Baba yake kumuonya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwenye shamba.

“Huyu Mtoto alipewa punda akachunge, akawaacha na akaenda kucheza na matokeo yake wale punda wakala shamba la Mtu, Mzee wake akalalamikiwa ndipo akamuita Mtoto lakini kitendo cha Mzee kumfokea yule Mtoto achunge punda kwa umakini, yeye akachukua maamuzi magumu akatafuta sumu akanywa na kufariki”

Kamanda Issah ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutafuta njia sahihi ya kuzungumza na Watoto huku pia akiomba Makanisa na Misikiti kuendelea kutoa mafunzo mema ya dini Kwa Watoto ili kutokuwa na maamuzi magumu.
Kosa lipi hapo la kuonya? Mpaka itafutwe njia sahihi.

Kamanda aache ujinga.

Watu wakichapa viboko shidaz kuonya kwa mdomo shida

Wazazi tufanye nini sasa?
 
Dogo angekutana na mzee wangu angejinyonga siku ileile anazaliwa.
Kuna kitu hakiko sawa, hawajasema mtoto ana umri gani na baba alimkanya vipi mpaka mtoto achukue maamuzi magumu.
Bila shaka kuna kitu cha muda mrefu kizito na kichungu alikuwa nacho moyoni, lakini baada ya huo mkasa uvumilivu ukamshinda na kuamua kuchukua maisha yake.
Huyo mzazi anatakiwa akamatwe ahojiwe kwa kina na kuelezea maisha yote ya nyuma ya mtoto, hapo ndio watakuja na conclusion. labda kuna kitu kingine alimtamkia au alimfanyia ambacho kwa umri wa mtoto ni ngumu kuweza kusuluhisha kichwani kwake akili yake ya kitoto au kuliongelea.

Kuna asilimia 60% inawezekana mzazi ndio anahusika moja kwa moja na kifo cha mtoto, hasa kama mzazi ni mlevi.
 
Waliewapindikiza Watu, wa Iringa, kuwa kususa kuzuri, nikuwaachia Dunia, alipanda mbegu mbaya sana.
 
inasikitisha sana kwa kweli, yaani kufokewa tu mtu kajiua
 
Back
Top Bottom