Njombe: Mwanafunzi wa miaka 9 afariki wakati akicheza mchezo wa kujinyonga na wadogo zake

Njombe: Mwanafunzi wa miaka 9 afariki wakati akicheza mchezo wa kujinyonga na wadogo zake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Ikelu iliyopo Makambako mkoani Njombe, Claud Florence (9) amefariki dunia baada ya kujinyonga akiwa anacheza na wenzake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Hamisi Issah amesema mwanafunzi huyo alikwenda shambani na wazazi wake na wadogo zake watatu akiwa huko alianza kucheza na wadogo zake na baadae kuchukua kikoi na kuanza kujaribisha namna mtu anavyojinyonga.

Amesema baada kufanya kitendo hicho katika mti pori uliopo hapo shambani matokeo yake alijikuta amening'inia kwenye mti huo huku wazazi wakiwa hawana taarifa yoyote wakiwa wanaendelea na kulima.

Amesema wazazi walipofika walifungua hicho kikoi na kumkuta mtoto wao akiwa taabani na kuchukua uamuzi wa kumpeleka hospitali na baadae kufariki dunia.

Amewataka wazazi kuwa makini na malezi ya watoto wao kwani malezi ya watoto ni pamoja na kuangalia aina ya michezo wanayocheza katika mazingira yanayofaa.

"Watoto hawa wamecheza michezo ya kupitiliza mpaka wamejaribisha kujinyonga na mwenzao mmoja kajiua kabisa" amesema Issah.

Michuziblog
 
Duuh!! Pole kwa hiyo familia.

Japo nawaza hao wadogo zake kwa nini hawajaenda kuwaita wazazi waone jinsi kaka anavyoning'inia au ndo walikuwa wanajua kuning'inia kwake bado ni sehemu ya mchezo?
 
Litakua kosa la Bongo movie dogi kaiga.. .mtu ana jinyonga uku ana tabasamu
 
watoto wanafanya kile wanachokiona, kuna mengi sana ya kuzingatia wakati wa malezi, nakumbuka wakati tunakuwa ilikiwa marufuku kuangalia movie za ngumi, siku hizi access imekuwa soft sana watoto wanaona kila kitu, hata mfano watoto wanacheza mchezo wa kibaba na kimama wanafanya yale wanayoona wazazi wao wanafanya usiku, utakuta wanasema tufanyw kama baba na mama wanakitanisha vikojoleo, hii mambo ya kulala single room na watoto, Mungu atuepushe
 
Back
Top Bottom