Njombe: RC Mataka: sitaki kusikia mtu ameambiwa gloves hazipo kwa mama mjamzito kwa kuwa huduma ya mama na mtoto ni bure

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amepiga marufuku wataalamu wa afya mkoani humo kutoza fedha wala vifaa tiba kwa mama mjamzito kwa kuwa huduma ya mama na mtoto ni bure, na kuwataka kufuata muongozo wa Sera ya Afya kwa usahihi.

RC Mtaka ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC) ambapo amesema wanawake wajawazito hawatozwi gharama za kujifungua hivyo wataamu wa afya wanapaswa kutekeleza agizo hilo.

"Wanawake wajawazito hawatozwi gharama za kujifungua, sitakubali kusikiliza kwamba mtu ameenda hospitali ameambiwa ‘gloves’ haipo, nyuzi ya kushona haipo, sijui pamba haipo tusiruhusu hilo jambo", amesema RC Mtaka

Pia soma: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani.

Nchi hii inaujinga sana.kinachosemwa ni tofauti na uhalisia.Bora kichaa chalamila alisema ukweli kuwa Huwa wanatozwa pesa wakati wa kujifungua pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano Huwa wanahudumiwa Kwa pesa japo kuwa sera ya wizara ya afya ni kupata huduma bure
 
Njombe hii hii nayoishi au kuna nyingine!!!?,au hii haikuepo kabla imeanza sasa?
 
View attachment 3225153
Huyu jamaa sio kiongozi mzuri maana kasifiwa mbio kapiliza nyumbani?

Naamini Bora mropokaji anayesema ukweli kuliko anayejifanya anabusara muongo.

Maana mkweli anafanya tujue Kuna tatizo tutalijadiri ila mwongo anayejifanya anabusara anafanya propaganda ionekane tatizo hakuna wakati lipo.
Sera ya afya ya taifa yote ni moja DSM na Njombe Sasa huyo mwongo atueleze hiyo budget wameitoa wapi ili tujue DSM wamefeli wapi
 
Njombe hii hii nayoishi au kuna nyingine!!!?,au hii haikuepo kabla imeanza sasa?
Huyu jamaa sio kiongozi mzuri maana ni mwongo na watanzania wengi wanapenda watu wa aina hii wale wanaosema ukweli hutuwataki kumbe kiongozi akisema ukweli ataonyesha tatizo lilipo ili litatuliwe.
 
Nashangaa,,coz watu tunaambiwa kabisa andaa mipira (gloves),si chini ya mitano,apo ndo pamoja na zile karatasi,ndoo nk....na nilinunua
 
Huyu jamaa sio kiongozi mzuri maana kasifiwa mbio kapiliza nyumbani?

Naamini Bora mropokaji anayesema ukweli kuliko anayejifanya anabusara muongo.

Maana mkweli anafanya tujue Kuna tatizo tutalijadiri ila mwongo anayejifanya anabusara anafanya propaganda ionekane tatizo hakuna wakati lipo.
Sera ya afya ya taifa yote ni moja DSM na Njombe Sasa huyo mwongo atueleze hiyo budget wameitoa wapi ili tujue DSM wamefeli wapi
Kama sera na muongozo wa wizara ya Afya unasema huduma za mama mjamzito kujifungua ni bure, sasa mjamzito anapodaiwa kulipa pesa ya kujifungua wakati huduma hizo ni bure hiyo pesa inakwenda kwa nani?
 
Nashangaa,,coz watu tunaambiwa kabisa andaa mipira (gloves),si chini ya mitano,apo ndo pamoja na zile karatasi,ndoo nk....na nilinunua
Harafu huyu mjinga anafanya siasa kwenye maisha na afya za watu na kuwasababishia mzigo watumishi wa afya maana watu hawatajiandaa harafu wakifika huko waanze kulaumu watumishi maana sidhani kama hao watumishi wakiuza hizo groves Hela wanachukua wao
 
Mkuu tunanunua pharmacy unapoenda unaenda nazo
 
Kama sera na muongozo wa wizara ya Afya unasema huduma za mama mjamzito kujifungua ni bure, sasa mjamzito anapodaiwa kulipa pesa ya kujifungua wakati huduma hizo ni bure hiyo pesa inakwenda kwa nani?
Mimi nnachosemea ni kiongozi kuwa mkweli watu wanalipishwa fedha harafu yeye asema hawalipishwi ili apate millage kisiasa au amoutsmart kiongozi mwingine
 
Nchi hii inaujinga sana.kinachosemwa ni tofauti na uhalisia.Bora kichaa chalamila alisema ukweli kuwa Huwa wanatozwa pesa wakati wa kujifungua pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano Huwa wanahudumiwa Kwa pesa japo kuwa sera ya wizara ya afya ni kupata huduma bure
Tatizo la yule mjinga Chalamila ni namna alivyosema. Angeweza kusema kwa namna ya kistaarabu na siyo kusema yule mama aende kwa mume wake akamzalishe.
 
Mkuu tunanunua pharmacy unapoenda unaenda nazo
Sasa huyo jamaa atatengeneza bomu maana wanaume watagoma kutoa pesa za vifaa wakihisi wanapigwa na wake zao na kuwasababishia ugumu wa kazi wakunga
 
Back
Top Bottom