Lupembe Nyave
New Member
- Mar 31, 2022
- 2
- 0
Kwako mheshimiwa, pole na majukumu ya kujenga taifa na pia hongera kwa kazi nzuri unazofanya. Mheshimiwa tunahitaji msaada
wako wa kupata haki yetu (tumedhulumika).
Tumefanya kazi, hatujalipwa fedha tulizofanyia kazi mpaka sasa. Tuliongea na Fanuel
Sabini (Facebook anatumia jina la Seven Sabini na Instagram anatumia jina la Seven Sabini) lakini amekataa kutulipa fedha tunazodai. Tumeamua kuandika kwenye mitandao ya kijamii huenda tukapata msaada kutoka kwa viongozi wetu na tukalipwa fedha tulizofanyia kazi.
Tumefanya kazi kwenye kampuni ya Kilimo Kwanza Tanzania (Pamoja Estate Farm-PFP) iliyoko mkoani Njombe kijiji cha Nyave (Barabara ya kuelekea Lupembe, unapita Kibena, Lupembe, Ukalawa kisha Nyave). Kampuni hii imepakana na kampuni ya NOVA inayomilikiwa na mzungu Michael na Oscar Luvanda. Ukifika Nyave kuna gari la kuchonga barabara (Bulldozer), linalochonga barabara ya kampuni ya Kilimo Kwanza Tanzania, linaloendeshwa na Msaura na Dady (Mdogo wake Seven Sabini). Hawa pia tushawahi kuwafikishia malalamiko yetu ya kutolipwa.
Kampuni hii inashughulika na uzalishaji wa parachichi yenye hekari zaidi ya 2,000 inayomilikiwa na Fanuel Sabini (Seven Sabini). Shughuli zinazofanyika kwenye kampuni hii ni kuchimba mashimo kwa ajili ya kupanda parachichi, kufukia mashimo yaliyochimbwa, kupanda miti ya parachichi na kupiga dawa kwa ajili ya kuua magugu. Hapo shambani amemuweka msimamizi anayeitwa Isack (Facebook anatumia jina la Aroldy Shadrack) ambaye anapokea maelekezo kutoka kwa Fanuel Sabini (Seven Sabini) kuhusu shughuli zote zitakazofanyika hapo shambani.
Tunataji msaada wako mheshimiwa tulipwe pesa zetu maana tushaongea naye sana atulipe pesa zetu ila aliishia kutuhaidi na mwisho wa siku alituambia hatulipi. Lukelo Mgana pia alikuja shambani, tukaweka naye mambo (peg) 144 lakini naye alikataa kutupa pesa zetu. Naye tunamdai pesa tulizoweka naye mambo (peg)
Taarifa za kiasi cha pesa tunachodai pamoja na shughuli tulizofanya kwa kila mmoja anazo Isack, msimamizi aliyewekwa na Seven Sabini shambani.
Tutashakuru kama ombi letu litakubaliwa na kufanyiwa kazi. Mama usitusahau, vijana wako tumefanya kazi lakini tumeishia kudhulumiwa. Tunahitaji msaada wako, tupate haki yetu.
Tunahitaji tulipwe fedha tulizofanyia kazi.
WATU TUNAODAI FEDHA
1. SHAIBU SEIFU
2. MAJALIWA JOSEPH
3. GEORGE GURAY
4. EMMANUEL SANGAWE
5. YASIN MLULU
6. KESHENI NYAHI
7. CLAUD KITUMBIKA
8. YUNIS MAHENGE
9. JUMA ANDRIANO
10. HAJI ALPHAN
11. LAWI SANGA
12. MKOMBOZI ALMAS
13. PETRO SIMON
14. DAIMA MDEMU
15. ISACK KAGUO
16. LITIA NYAGAWA
17. TEGEMEA CHAULA
18. ADOLF ADAPTATIUS
19. FRANK HEZILON
Usomapo ujumbe huu, tunaomba umfikishie kiongozi yoyote unayemjua. Atusaidie tupate haki zetu. Tunahitaji tulipwe hela tulizofanyia kazi
Imetolewa 01/04/2022
nyavelupembe@gmail.com