Njombe: Viongozi wa CHADEMA pamoja na dalali wa mbao wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa

Njombe: Viongozi wa CHADEMA pamoja na dalali wa mbao wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa

Nchi kuharibika hua ni process.nchi hua haiaribiki overnight,tueni makini sana.lets not poison the village well

MUNGU amhukumu kwa huruma marehem,amfutie dhambi zake zote Na ampatie haki yake alionyanganywa hapa duniani
 
Huku bara mhalifu lazima awe Chadema wakati wa uchaguzi sawa na kule Zanzibar ilikuwa mhalifu awe Cuf wakati huo. Hii inaonesha polisi wanatumika kisiasa zaidi ya uweledi wa kiusalama


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Nikiona mtu wa CHADEMA amani huwa inaniisha,wao wanaamini njia kuuu ya kusuruhisha mambo ni kuwa,ona sasa wanaenda kufia jela,na hata kama watatoka sio Leo au kesho,wataonja joto la jiwe

Siasa za namna hii hazifai hata kidogo,
 
Chadema ikichukua nchi oktoba 28 italifuta jeshi la polisi , huu ujinga wa kuwanunua wagombea udiwani ulipangwa na kwamba wakikataa watapewa kesi yoyote , na hii imevuja tangu wiki 2 zilizopita eti leo ndio inatekelezwa ! Poor Polisi
Mwambie Masonga ajiandae kisaikolojia kwa sababu ndiye mchora ramani.
 
Siasa tu, yaani vyama vinatajwa kana kwamba ni mashindano. Mi nadhani kama wamehusika wangeshughulikiwa wao binafsi hii vyama vyama kutajwa inapoteza nia njema ya jeshi la polisi
Mkuu huu ndio utaratibu,kwani nani hajui kuwa CHADEMA wamekuwa wakiendesha mipango ya mauaji kwa raia sema na wale wote wanao wahisi kuwa wanawapinga?
 
Police wamejuaje kuwa ule mkanda wa kiunoni ulikuwa wa marehemu ?

Au ulikuwa na jina la marehemu ?
Duh..maswali mengine ni ya ajabu kwa kweli...uelewa wa baadhi yetu uko chini Sana....poor Tanzania...
 
Nikiona mtu wa CHADEMA amani huwa inaniisha,wao wanaamini njia kuuu ya kusuruhisha mambo ni kuwa,ona sasa wanaenda kufia jela,na hata kama watatoka sio Leo au kesho,wataonja joto la jiwe

Siasa za namna hii hazifai hata kidogo,
Ndo mana Lissu anasema akiwa Rais kila kesi itakuwa na mdhamana,wengi walioko magereza ni kesi za kubambikiwa..
 
Kiongozi mkubwa wa CCM aliyetaka kumuua Tundu Lissu amekamatwa?

Mara nyingi Tundu Lissu amemtaja bayana muuaji yule kwa kuonyesha ushiriki wake mwanzo mwisho lkn polisi wako kimya....

Je yuko juu ya sheria?
 
Kuna hasara sababu kuna siku atakuja kuwa chadema na pia kuwa kiongozi mkubwa sana wa upinzani. Rejea waliotoka ccm na sasa ni viongozi huko upinzani.

Mfano nyalandu ni mwenyekiti wa chadema kanda ya kati, na ni mmoja wa viongozi wa chadema wanaosifika sana kwa utendaji
Ninajiuliza hivi akifa ccm kuna hasara yoyote?
 
Polepole alitoa agizo kwa Sirro juzi. Na kasema mauaji yametekelezwa na "chama cha Mbowe". Kamanda katekeleza kama alivyoagizwa! Nchi imejaa unafiki sana.
Kama kuna watu wanaagiza kubambikia kesi za uongo wenzao kwa matakwa ya kisiasa naomba walaaniwe na Mungu awapige pigo takatifu,

Lakini kama ni kweli watuhumiwa wamehusika basi wachukuliwe hatua kali za kisheria
 
Hii kitu inaenda kumtafuna emma masonga, sijui ni kwa nini amekuwa hivyo!
 
Isidingo....

Kada wa CCM alifuata nini kwenye gari la chadema? alikuwa na mahusiano gani na madiwani wote hao wa chadema kipindi hiki cha kampeni?
 
[emoji16][emoji16][emoji16] ila polisi daah eti Mkanda!
Walimvua labda wakautmia kumnyonga nao unashangaa nini ? Ni ushahidi muhimu sababu lazima finger prints za washukiwa zitakuwa kwenye mkanda.Unaudharau?
 
Ni mauaji ya yule kijana wa CCM kule Njombe.

Wagombea udiwani wawili na Katibu mwenezi wa kata wote wa CHADEMA na dalali wa mbao wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu na kada wa CCM yaliyotokea huko Njombe.

Pamoja na wao pia gari la mtuhumiwa mmojawapo limekamatwa na kukutwa baadhi ya vitu vya marehemu vikiwa ndani yake.

=======
RPC wa Njombe, Hamis Issa amesema,gari namba T457 DAB Toyota Gaiya ya George Sanga mgombea udiwani kata ya Ramadhani(CHADEMA)ilitumiwa wakati wa utekelezaji wa mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa kutokana na kukutwa mkanda wa kiunoni wa marehemu baada ya gari hiyo kushikiliwa


Jeshi la polisi mkoani Njombe limesema mpaka sasa wanashikiliwa watu wanne wakiwemo makada watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za mauaji ya Emmanuel Mlelwa mwanafunzi wa chuo cha Tumaini Iringa ambaye ni mwenyekiti wa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu (UVCCM) mkoa wa Iringa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa akizungumza na vyombo vya habari,amesema jeshi hilo limewashikilia watu hao kutokana na upelelezi wa awali wa mawasiliano yake.

“Jeshi la polisi lilianza upelelezi na tukajua mtu wa mwisho aliyekuwa anaongea naye ni mtu mmoja anaitwa Tadei Mwanyika,huyu ni mgombea udiwani kupitia kata ya Utalingolo,tulimkamata na hakuwa na maneno mengi yeye anasema kweli nilikuwa na Marehemu”alisema kamanda Issa

Aidha amesema mtu wa pili kutambuliwa ni George Sanga mgombea wa Udiwani kupitia Chadema kata ya Ramadhani ambaye gari yake ilitumika kuwabeba watu hao akiwemo marehemu Emmanuel Mlelwa.

Vile vile amesema mtuhumiwa mwingine aliyeshikiliwa ni Optatus Mkwera katibu mwenezi wa kata ya Ramadhani wa Chadema ambaye kwa mujibu wa maelezo yake ameeleza tukio zima lilivyokuwa.

“Huyu naye alihusika kushiriki mauaji kwa mujibu wa maelezo yake”alisema Kamanda

Mtuhumiwa wa nne ni Gudluck Mfuse anayejishughulisha na udalali wa magari yanayobeba mbao na viazi ambapo kamanda wa polisi amesema tukio hilo anaamini lilikuwa limepangwa na jeshi hilo linaendelea na upepelezi dhidi ya mtandao huo ili haki itendeke.

Hata hivyo kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema gari namba T457 DAB Toyota Gaiya inayomilikiwa na George Sanga mgombea wa udiwani kata ya Ramadhani ndio inayotuhumiwa kutumiwa wakati wa utekelezaji wa mauaji ya Kada huyo wa CCM kutokana na kukutwa mkanda wa kiunoni wa marehemu baada ya gari hiyo kushikiliwa.

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amesema mwili wa marehemu Emmanuel, ulikutwa eneo la bwawa la maji kibena na alipotea tangu tarehe 20 mwezi wa 9 huku akiwa ni miongoni mwa vijana walioko kwenye timu ya kampeni ya mgombea wa Ubunge jimbo la Njombe mjini.

“Kwa mara ya mwisho simu yake ilikuwa hewani tarehe 20 tangu hapo hakupatikana lakini kwa kuwashirikisha ndugu wa marehemu ilibainika mwili uliokuwepo hospitali ni wa Emmanuel Mlelwa na ushahidi wa awali unaonyesha ndugu Emmnuel ameuawa kikatili katika mazingira ya kisiasa”alisema Marwa Rubirya

Hata hivyo uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia kwa mwenyekiti wake Rose Mayemba wameliomba jeshi la polisi kuweka wazi juu ya taarifa za wagombea wao bila kuharibu uchunguzi wao.

“Tunaliomba jeshi la polisi kama kuna mambo inafuatilia ni vema sisi na wao kuwe na taarifa za wazi kama wamehusika na mauaji watuambie lakini kitendo cha kuficha taarifa sahihi hatuwezi kuishi kwa namna hiyo kwa kuwa wale ni wagombea”alisema Rose Mayemba.
Duh hilo ndilo geshi letu...yaani siku zoote wanafikiria kuwa I.Q za watanzania woote zinafanana na za kwao (Std Seven looser)..Nendeni Motuary chukueni mkanda wa mrehemu arafu turetee sisi tutajua ra kufanya au chukua madawa ya kurevyaa muweke nyumbani kwake arafu tutarifunguria kesi ya madawa rimekwishaaa rire...
 
Back
Top Bottom