Njombe: Viongozi wa CHADEMA pamoja na dalali wa mbao wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa

Njombe: Viongozi wa CHADEMA pamoja na dalali wa mbao wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa

Kama kuna watu wanaagiza kubambikia kesi za uongo wenzao kwa matakwa ya kisiasa naomba walaaniwe na Mungu awapige pigo takatifu,

Lakini kama ni kweli watuhumiwa wamehusika basi wachukuliwe hatua kali za kisheria
Lakini inaelezwa kuwa mmoja wao amekiri na kueleza tukio zima. Ushahidi wa kimazingira unaonesha mtu wa mwisho kuongea na marehemu ni mtuhumiwa pia. Sauti itaeleza waliongea nini.

Unadhani huyo dalali amekamatwa kwa makosa?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Mkanda wa marehemu kwenye gari ya mgombea udiwani wa Chadema!! Ebu Polisi kuweni serious basi msilete isidingo kama ya watekaji wa Mo, kumbukeni Rais aliwaambia watanzania sio wajinga.
Hakika hii ni isindingo! Mtu auawe tarehe 20/9 na mkanda ubaki ndani ya gari hadi tarehe 28/9?

Lazima kuna namna!
 
Mpaka raha yani so smooth...

Polisi wala hawajatumia nguvu kubwa, wamefuatilia mawasiliano ya simu then wakawaokota mmoja baada ya mwingine chap.

Mpaka na mkanda wa marehemu kwenye gari yani kuonyesha jinsi wauaji walivyo malofa.

Kumbe yule aliyekuwa anamtishia ben saanane kwenye sms pia angeweza kupatikans kwa urahisi hivi?

Na ile gari aliyoitajaga lissu kuwa inamfuatilia ingeweza kupelekea watuhumiwa kujulikana ndani ya siku kadhaa?

Labda mikoa inapishana uwezo wa kiuchunguzi. Hongereni Njombe mko fit.
Alifahamika, alikuwa Mbowe. Umewahi kusikia anakanusha?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Mbona hizi mbinu ni za zamani sana?
Tanzania has a long journey to go kama ni hivi!.
Mbona watu wanasahau kwamba kuna Mungu ambaye kila mtu atasimama mbele zake baada ya kufa ambako ni mara moja tu?

Tutumai elevator gani ili akili za watu wenye dhamana za uongozi wapande kiwango?

Ni nani role model wa fikra duni namna hii?

Ohh My Country Tanzania!. I m Crying for you my Mama land!. God, have mercy on us in Jesus Name!. We need you God. Is only you who can rescue my Country!. We need you Heavenly father.

Mungu naomba Umtume malaika Raguel kwenye nchi ya Tanzania aje kusimama katika haki na kweli juu ya shauri hili. Katika Jina la Yesu Kristo aliye hai nimeomba . Watu wote tuseme Amen.
Majani ya Malawi si ya mchezo. Ulianza kuvuta lini mkuu?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ni mauaji ya yule kijana wa CCM kule Njombe.

Wagombea udiwani wawili na Katibu mwenezi wa kata wote wa CHADEMA na dalali wa mbao wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu na kada wa CCM yaliyotokea huko Njombe.

Pamoja na wao pia gari la mtuhumiwa mmojawapo limekamatwa na kukutwa baadhi ya vitu vya marehemu vikiwa ndani yake.

=======
RPC wa Njombe, Hamis Issa amesema,gari namba T457 DAB Toyota Gaiya ya George Sanga mgombea udiwani kata ya Ramadhani(CHADEMA)ilitumiwa wakati wa utekelezaji wa mauaji ya Kada wa CCM Emmanuel Mlelwa kutokana na kukutwa mkanda wa kiunoni wa marehemu baada ya gari hiyo kushikiliwa


Jeshi la polisi mkoani Njombe limesema mpaka sasa wanashikiliwa watu wanne wakiwemo makada watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za mauaji ya Emmanuel Mlelwa mwanafunzi wa chuo cha Tumaini Iringa ambaye ni mwenyekiti wa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu (UVCCM) mkoa wa Iringa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa akizungumza na vyombo vya habari,amesema jeshi hilo limewashikilia watu hao kutokana na upelelezi wa awali wa mawasiliano yake.

“Jeshi la polisi lilianza upelelezi na tukajua mtu wa mwisho aliyekuwa anaongea naye ni mtu mmoja anaitwa Tadei Mwanyika,huyu ni mgombea udiwani kupitia kata ya Utalingolo,tulimkamata na hakuwa na maneno mengi yeye anasema kweli nilikuwa na Marehemu”alisema kamanda Issa

Aidha amesema mtu wa pili kutambuliwa ni George Sanga mgombea wa Udiwani kupitia Chadema kata ya Ramadhani ambaye gari yake ilitumika kuwabeba watu hao akiwemo marehemu Emmanuel Mlelwa.

Vile vile amesema mtuhumiwa mwingine aliyeshikiliwa ni Optatus Mkwera katibu mwenezi wa kata ya Ramadhani wa Chadema ambaye kwa mujibu wa maelezo yake ameeleza tukio zima lilivyokuwa.

“Huyu naye alihusika kushiriki mauaji kwa mujibu wa maelezo yake”alisema Kamanda

Mtuhumiwa wa nne ni Gudluck Mfuse anayejishughulisha na udalali wa magari yanayobeba mbao na viazi ambapo kamanda wa polisi amesema tukio hilo anaamini lilikuwa limepangwa na jeshi hilo linaendelea na upepelezi dhidi ya mtandao huo ili haki itendeke.

Hata hivyo kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema gari namba T457 DAB Toyota Gaiya inayomilikiwa na George Sanga mgombea wa udiwani kata ya Ramadhani ndio inayotuhumiwa kutumiwa wakati wa utekelezaji wa mauaji ya Kada huyo wa CCM kutokana na kukutwa mkanda wa kiunoni wa marehemu baada ya gari hiyo kushikiliwa.

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amesema mwili wa marehemu Emmanuel, ulikutwa eneo la bwawa la maji kibena na alipotea tangu tarehe 20 mwezi wa 9 huku akiwa ni miongoni mwa vijana walioko kwenye timu ya kampeni ya mgombea wa Ubunge jimbo la Njombe mjini.

“Kwa mara ya mwisho simu yake ilikuwa hewani tarehe 20 tangu hapo hakupatikana lakini kwa kuwashirikisha ndugu wa marehemu ilibainika mwili uliokuwepo hospitali ni wa Emmanuel Mlelwa na ushahidi wa awali unaonyesha ndugu Emmnuel ameuawa kikatili katika mazingira ya kisiasa”alisema Marwa Rubirya

Hata hivyo uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia kwa mwenyekiti wake Rose Mayemba wameliomba jeshi la polisi kuweka wazi juu ya taarifa za wagombea wao bila kuharibu uchunguzi wao.

“Tunaliomba jeshi la polisi kama kuna mambo inafuatilia ni vema sisi na wao kuwe na taarifa za wazi kama wamehusika na mauaji watuambie lakini kitendo cha kuficha taarifa sahihi hatuwezi kuishi kwa namna hiyo kwa kuwa wale ni wagombea”alisema Rose Mayemba.
Huo ni uwongo wa CCM, Mtu mwenye akili timamu anajua huo ni uongo mtupu.
 
Taarifa ya Jeshi la Polisi imekaa kienyeji sana. Kuna uwezekano mkubwa huyu kijana ameuawa na greenguards. Kwa analysis ifuatayo:

1) Marehemu alikuwa mwanatimu ya kampeni ya CCM

2) Watu aliokuwa akiwasiliana nao ni makamanda wa CHADEMA - alikuwa anaongea nao nini?

3) Kama Polisi ambao wanatumika na CCM wanasema waliweza kunasa mazungumzo ya marehemu na makada wa CHADEMA, ina maana wanajua marehemu alikuwa na uhusiano gani na hap viongozi wa CHADEMA

Maswali:

1) Je, haiwezekani kuwa greenguards walikuwa wanamwona marehemu amewageuka, na labda pengine kuridhika kuwa alikuwa jasusi wa CHADEMA?

2) Kama marehemu alihisiwa kuwa amewasaliti wenzake wa CCM, hakuna uwezekano kijana huyu ameuawa na greenguards kwa kpsa la usaliti

HISTORIA

1) CHADEMA haijawahi kuwa na historia ya kuua, kuteka au kwapoteza watu

2) Greenguards imesheheni vijana wauaji na katili. Uchaguzi wa 2010, mwenyekiti wa CHADEMA Arusha, aliuawa na greenguards kwa kukatwa shingo kwa kutumia chainsew

3) Mwaka 2010, greenguards walimwua kwa kumkata mapanga marehemu Mawazo Geita, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa

4) Kama sikosei, mwaka 2016, greenguards walimwua kwa kumkata mapanga diwani kupitia CHADEMA huko Morogoro

5) Greenguards walimjeruhi vibaya kwa mapanga mbunge Haines kupitia CHADEMA huku polisi wakiwa pembeni wamesimama kuwapa ulinzi greenguards wanapomshambulia Hyness.

Na mara zote, ukiona kiongozi wa CHADEMA au mpenzi wa CHADEMA ameuawa, halafu hakuna mtu yeyote aliyekamatwa wala kutuhumiwa, ujue mauaji hayo yamefanywa na greenguards au na wasiojulikana.

Hakuna polisi mwenye uwezo wa kumkamata greenguard au asiyejulikana.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi mkubwa wa ccm aliyetaka kumuua Tundu Lissu amekamatwa?

Mara nyingi Tundu Lissu amemtaja bayana muuaji yule kwa kuonyesha ushiriki wake mwanzo mwisho lkn polisi wako kimya....

Je yuko juu ya sheria?
Tuweke jina alilotaja.
Halafu anaongea na vyombo vya habari, kwanini asiende polisi?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Polepole alitoa agizo kwa Sirro juzi. Na kasema mauaji yametekelezwa na "chama cha Mbowe". Kamanda katekeleza kama alivyoagizwa! Nchi imejaa unafiki sana.
Ninafurahi kwamba kumbe watu wanafuatilia na kuelewa kila njama zenye nia ovu zinazofanywa kwa hila. Mtu eliyemsikiliza polepole juzi atagundua kabisa kwamba kuna jambo lilikuwa linapangwa na sasa kweli limetimia. Hizi damu zinazomwagika kwa njia hizi siyo dalili nzuri.
 
Mwambie Masonga ajiandae kisaikolojia kwa sababu ndiye mchora ramani.
Tunafahamu si leo wala juzi kwamba Masonga anasakwa ili Mhujumu uchumi Deo Mwanyika ambaye hatakiwi Njombe apitishwe kwa nguvu , lakini damu itamwagika kwenye hili mkitaka kulazimisha
 
Hata Deo akishinda, nadhani ushindi wake utatenguliwa mahakamani kirahisi kwa sababu hana sifa ya kugombea ubunge in the first place.
Tunafahamu si leo wala juzi kwamba Masonga anasakwa ili Mhujumu uchumi Deo Mwanyika ambaye hatakiwi Njombe apitishwe kwa nguvu , lakini damu itamwagika kwenye hili mkitaka kulazimisha
 
Back
Top Bottom