LGE2024 Njombe: Wagombea waonywa kukiuka kanuni wakati wa Kampeni

LGE2024 Njombe: Wagombea waonywa kukiuka kanuni wakati wa Kampeni

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Halmashauri ya mji wa Njombe imekiri kuweka sawa mazingira ya uchaguzi wa serikali za mitaa hadi kwa makundi maalumu ili yaweze kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo Novemba 27 mwaka huu.

Mbele ya Vyombo vya Habari Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amesema kila kitu kipo sawa kuanzia kuzinduliwa kwa Kampeni hapo Kesho na kwamba makundi maalumu yatapewa kipaumbele siku ya Kupiga kura.

Pia, Soma: Yanayojiri kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoa wa Njombe

Aidha Kuruthum Sadick amevitaka vyama vya siasa vya CCM na CHADEMA Vinavyoshiriki uchaguzi huo Katika Halmashauri yake pamoja na wagombea kufuata kanuni na taratibu kwa mujibu wa Sheria na makubaliano katika uendeshaji wa Kampeni.

Kwa upande wao wananchi mkoani Njombe akiwemo Seif Mtamike,Deus Sanga na Rejino Mwapinga wamesema hawataki sera za uongo kwa wagombea ambazo hazitekelezeki.

Kituo hiki kimezungumza na Vyama vya siasa kwa njia ya Simu kutaka kujua namna vilivyojipanga katika Kampeni na Wagombea wao ambapo Katibu wa Siasa na uenezi CCM Mkoa wa Njombe Josaya Luoga anasema kila jimbo limeweka utaratibu wa kuzindua kampeni hizo.
1732030577262.png
 
Back
Top Bottom