Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Leo tarehe 3 Agosti 2025 nimepita kwenye Ofisi za CCM Wanging'ombe hapa Mkoani Njombe, nimekuta baadhi ya Wanafunzi wakiwa nje ya Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Wanging'ombe.
Sijajua nini hasa ambacho kinaendelea lakini imenishangaza kidogo kuona Wanafunzi wakiwa nje ofisi hiyo tena Jumapili, wanataka nini? Kwa nini Wanafunzi? Wamevaa sare za Shule hawa ni Wanafunzi wa wapi?
Nimeshindwa kusogea kwa kuwa yasije kunikuta ambayo hayanihusu kwa kuwa mudu mfupi baadaye waliingia ndani ya ofisi.