Njombe: Watoto wawili wa Kiongozi wa Kijiji cha Kipengele wauawa kikatili

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Vijana wawili wa familia moja wameuawa kikatili kwa kupigwa na vitu vizito kichwani usiku wa kuamkia april 27 katika kijiji cha Kipengele kilichopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema vijana waliouwawa ni Felis Frank Chaula(20) mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Dar es salaam pamoja na Fabio Frank Chaula mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mount Kipengele ambapo wote ni watoto wa mzee Frank Chaula ambaye ni kiongozi wa kijijini hapo.

Kamanda Issah amesema katika tukio hilo ambalo limetokea katika nyumba ya biashara ya familia hiyo , watu saba wamekamatwa ili kusaidia upelelezi wa tukio hilo huku pia kamati za ulinzi na usalama kutoka ngazi ya wilaya na mkoa zikilazimika kukutana kwa dharura kujadili namna ya shughulikia tukio hilo.

Mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa vijana hao ambao ni wanafunzi unamfanya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kushindwa kujizuia na kuagiza kuchukuliwa hatua kali dhidi ya wahalifu watakapobainika.

Baadhi ya wakazi ambao wamefika katika eneo la tukio wanasema kumekuwa na matukio ya mauaji mabaya ya kufatana takribani 7 hivyo wanaiomba serikali kuchukua hatua madhubuti za kuwabaini wahusika .
 
Aisee!! Lakini mbona imekaa kama kulipiz kisasi,,,tokea jana ni tanzia tu
 
Pumzikeni kwa amani vijana, hawa wangekua wasomi wetu kesho. Poleni wafiwa.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Vijana wawili wa familia moja wameuawa kikatili kwa kupigwa na vitu vizito kichwani usiku wa kuamkia april 27 katika kijiji cha Kipengele kilichopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema vijana waliouwawa ni Felis Frank Chaula(20) mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Dar es salaam pamoja na Fabio Frank Chaula mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mount Kipengele ambapo wote ni watoto wa mzee Frank Chaula ambaye ni kiongozi wa kijijini hapo.

Kamanda Issah amesema katika tukio hilo ambalo limetokea katika nyumba ya biashara ya familia hiyo , watu saba wamekamatwa ili kusaidia upelelezi wa tukio hilo huku pia kamati za ulinzi na usalama kutoka ngazi ya wilaya na mkoa zikilazimika kukutana kwa dharura kujadili namna ya shughulikia tukio hilo.

Mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa vijana hao ambao ni wanafunzi unamfanya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kushindwa kujizuia na kuagiza kuchukuliwa hatua kali dhidi ya wahalifu watakapobainika.

Baadhi ya wakazi ambao wamefika katika eneo la tukio wanasema kumekuwa na matukio ya mauaji mabaya ya kufatana takribani 7 hivyo wanaiomba serikali kuchukua hatua madhubuti za kuwabaini wahusika .
Jamani mbona binadamu tunakuwa wakatili hivi siku hizi,so sad MUNGU aipe nguvu familia ktk kipindi hiki kigumu.
 
Raha ya milele uwape ee Bwana na mwanga wa milele uwaaangazie wapumzike kwa amani. Amina x 3

Ila korona hiiii !!!!!shu
Isingekuwa shule na vyuo kufungwa kwa korona yawezekana madogo wangekuwa mbali na home (bwenini)
 
Bidamu ..hasa baadhi ya Africa tuna itikadi kali sana ambazo Mzungu hana,Mungu atusamehe
 
Back
Top Bottom