Njombe: Wawili wauawa na mganga wa kienyeji na kutupwa msituni

Njombe: Wawili wauawa na mganga wa kienyeji na kutupwa msituni

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Watu wawili, Suzana Mtitu (38) na Kassim Kitamkanga (35) wakazi Makambako Mkoani Njombe wamekutwa wamefariki katika msitu wa Tanwat uliopo Njombe huku uchunguzi ukibainisha kuwa wameuawa na Mganga wa Jadi baada ya Watu hao waliokuwa Wateja wake kugundua dawa za kuwa Matajiri walizopewa hazijafanya kazi.

RPC wa Njombe, Hamis Issah amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Mganga huyo wa kienyeji, Joseph Mgunda (41) Mkazi wa Sovi Kata ya Mtwango Wilayani Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

“Watu wengi Wafanyabiashara huyu Mganga anawaambia ukipeleka hela anaziombea halau baadaye zinaongezeka, sintofahamu iliyotokea kwa hawa Watu wawili walipewa dawa tayari lakini wakaona matokeo hayaleti mafanikio wakaenda kumuuliza mganga mbona umetupa dawa ambayo haisaidii, Mganga huyo alishikwa na hofu na kushauriwa na Ndugu zake kutekeleza mauaji hayo"

“Ndugu zake wakamwambia ukitaka usipate shida waue hawa Watu na kweli Watu watatu na yeye mwenyewe Mganga akiwa ni wanne wakatekeleza mauaji, Mwanaume alikatwa mapanga sehemu za shavuni upande wa kulia na kushoto na kichwani na pia kapigwa rungu na kudondoka na Mwanamke alipigwa rungu moja tu na kudondoka chini

Kamanda Issah amesema Watu wengine wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo ni Andrew Vahuruka, Gadi Mwanzalila (36) na Kelvin Kilinge (29), Kamanda Issah ametoa wito kwa Wananchi kutafuta pesa kwa juhudi za kufanya kazi na sio kutafuta utajiri kwa Waganga kwa kuwa hakuna utajiri unaoletwa na Waganga.
 
Watu wawili, Suzana mtitu(38) na Kassim Kitamkanga(35)wakazi wa Makambako Mkoani Njombe wamekutwa wamefariki katika msitu wa Tanwat uliopo Njombe huku uchunguzi ukibainisha kuwa wameuawa na mganga wa jadi baaya ya wateja hao kugundua kuwa dawa za kuwa matajiri walizopewa hazijafanya kazi.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema jeshi la Polis linamshikilia mganga huyo wa huyo Kienyeji, Joseph Mgunda(41)mkazi wa Sovi kata ya Mtwngo Wilayani Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

"Watu wengi wafanyabiashara huyu mganga anawaambia ukipeleka hela anaziombea halafu baadaye zinaongezeka, sintofahamu iliyotokea kwa hawa watu wawili walipewa walipewa dawa tayari lakini wakaona matokeo hayaleti mafanikio wakaenda kumuuliza mganga mbona umetupa dawa ambayo haisaidii, mganga huyo alishikwa na hofu na kushauriwa na ndugu zake kutekeleza mauaji hayo"

"Ndugu zake wakamwambia ukitaka usipate shida wauwe hawa watu na kweli watu watatu na yeye mwenyewe mganga akiwa ni wanne wakatekeleza mauwaji. Mwanaume alikatwa mapanga sehemu za shavuni upande wa kulia na kushoto na kichwanina pia kapigwa rungu na kudondoka na mwanamke alipigwa rungu moja tu na kudondoka chini"

Kamanda Issah amesema watu wengine wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauwaji hayo ni Andrew Vahuruka, Gadi Mwanzalila9(36) na Kelvin Kilinge(29), Kamanda Issah ametoa wito kwa wananchi kutafuta pesa kwa juhudi za kufanya kazi na si kutafuta utajiri kwa waganga kwa kuwa utajiri unaoletwa na waganga.
 
Kipo cha kujifunza hapa ambacho ni kuamini kipato au riziki ya mtu inapangwa na aliye juu na si vinginevyo.
Hakika kikubwa ni kujituma kwa juhudi binafsi naza halali.
 
sasa uzi wangu mtakuwa mshaelewa kuwa :utajiri ni rahisi ila masharti ni magumu.

walio ni beza njoeni mjionee
 
sasa uzi wangu mtakuwa mshaelewa kuwa :utajiri ni rahisi ila masharti ni magumu.

walio ni beza njoeni mjionee
Ambatanisha bandiko lako tulione tulio pitwa na bandiko
 
Jamii bado inaamini upuuzi kuwa utajiri unapata kwa mganga badala ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa yenye stadi na ubunifu. Hawa waganga wapigwe maarufuku maana wamekuwa wakileta maafa kwa jamii
 
Ndio maana kuna sababu ya kumuamini Mungu wa kweli tuliyehubiriwa ndiye mtoa riziki kuliko kuamini hawa waganga tapeli kwa kisingizio cha kuendeleza mila na tamaduni. Ni ushenzi kuendeleza utamaduni huu, waganga wote ni mashetani tu wala hawana uwezo wa kumtajirisha mtu, utajiri wa mtu uko kwenye akili zake kwa namna anavyoweza kuzitumia vizuri katika kuona fursa za kujitajirisha mwenyewe. Waganga kama hawa wanaoleta maafa kwa jamii wapigwe marufuku kufanya shughuli zenye utata
 
Jamii bado inaamini upuuzi kuwa utajiri unapata kwa mganga badala ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa yenye stadi na ubunifu. Hawa waganga wapigwe maarufuku maana wamekuwa wakileta maafa kwa jamii
Watapigwa vipi marufuku wakati hao hao ndiyo wateja wao! Wengine wanajibadilisha CV nakujiita machifu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wawili, Suzana mtitu(38) na Kassim Kitamkanga(35)wakazi wa Makambako Mkoani Njombe wamekutwa wamefariki katika msitu wa Tanwat uliopo Njombe huku uchunguzi ukibainisha kuwa wameuawa na mganga wa jadi baaya ya wateja hao kugundua kuwa dawa za kuwa matajiri
Hivii Kilondalonda alikwenda wapi, yeye alikuwa na uwezo wa kutoka mahabusu kwenda kula chakula Kondoa Hotel na kurudi bila askari wa zamu kujua,
 
Back
Top Bottom