Njombe: Wawili wauawa na mganga wa kienyeji na kutupwa msituni

Watu wawili, Suzana mtitu(38) na Kassim Kitamkanga(35)wakazi wa Makambako Mkoani Njombe wamekutwa wamefariki katika msitu wa Tanwat uliopo Njombe huku uchunguzi ukibainisha kuwa wameuawa na mganga wa jadi baaya ya wateja hao kugundua kuwa dawa za kuwa matajiri walizopewa hazijafanya kazi.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema jeshi la Polis linamshikilia mganga huyo wa huyo Kienyeji, Joseph Mgunda(41)mkazi wa Sovi kata ya Mtwngo Wilayani Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

"Watu wengi wafanyabiashara huyu mganga anawaambia ukipeleka hela anaziombea halafu baadaye zinaongezeka, sintofahamu iliyotokea kwa hawa watu wawili walipewa walipewa dawa tayari lakini wakaona matokeo hayaleti mafanikio wakaenda kumuuliza mganga mbona umetupa dawa ambayo haisaidii, mganga huyo alishikwa na hofu na kushauriwa na ndugu zake kutekeleza mauaji hayo"

"Ndugu zake wakamwambia ukitaka usipate shida wauwe hawa watu na kweli watu watatu na yeye mwenyewe mganga akiwa ni wanne wakatekeleza mauwaji. Mwanaume alikatwa mapanga sehemu za shavuni upande wa kulia na kushoto na kichwanina pia kapigwa rungu na kudondoka na mwanamke alipigwa rungu moja tu na kudondoka chini"

Kamanda Issah amesema watu wengine wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauwaji hayo ni Andrew Vahuruka, Gadi Mwanzalila9(36) na Kelvin Kilinge(29), Kamanda Issah ametoa wito kwa wananchi kutafuta pesa kwa juhudi za kufanya kazi na si kutafuta utajiri kwa waganga kwa kuwa utajiri unaoletwa na waganga.
FB_IMG_1644058260585.jpg
 
Wangesogea kule Makete kwa Mwakipande au kwa Meseketwa kupata utajiri.. Wao wameishia Njombe tu .
 
Haya mauaji yasiyo na mantiki yalikuwepo tangu enzi za Mwinyi na Nyerere.

Kinachofanyika sasa ni kuhakikisha hata ikitokea mtu akameza sisimizi akafa inatangazwa na anatafutwa mtuhumiwa aliyemtuma sisimizi.

Urais una mazonge aisee
 
Huyo mganga ni mpumbavu alishindwa vipi kucheza na akili za wateja zake, angewambia mmekosea masharti.
 
Kuna member humu alipost uzi wake wa kuutaka utajiri,
Ameiona hiii

Ova
mrangi duniani kuna mambo. Kuna siku nilifanya utani nikaandika hapa kuwa anayetaka utajiri aniambie nimtajie mganga. Huwezi kuamini, nilipata private meseji nyingi, watu wakiomba niliwaambie alipo huyo mganga na wapo tayari kwa lolote. Kwa namna hii imani za kishirikina hazitaisha. Kuna watu wengi sana wanadhani mafanikio hupatikana na wanganga na siyo kwa kufanya kazi.
 
Hahaha

Ova
 
Back
Top Bottom