Hanny danny
Member
- Oct 29, 2019
- 61
- 31
Aisee Maisha Magumu sana Watu tunatafuta short cut
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo we enzi zile tungekuitaje mkuuI have seen that shit. Sorry for those foolish people. Waache kukurupuka na kukimbilia kwa matapeli.
kwasababu yeye ni tapeli, angesepa tu kuliko kutoa roho zao tena. too bad. lkn, mshahara wa dhambini mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele. hasara ninayoiona hapo ni watu wawili kufa bila Mungu na kuelekea motoni moja kwa moja, hiyo ndio hasara kubwa kuliko hata kifo chenyewe. tulio hai tujitafakari na kujifunza toka kwao, haya maisha unaishi mara moja tu, na baada ya kifo ni hukumu. hata watu wakikuombea huku duniani ukishakufa kama hukumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, utaelekea moja kwa moja motoni ukaungue pamoja na shetani. hii ni kwasababu bila kupitia imani (ya neema) kwa Yesu Kristo, Mungu hakutambui, ni Yesu tu alimwaga damu kama ukombozi na njia ya kufuta dhambi za wanadamu. alifanyika kafara la dhambi zetu na ukombozi wetu, alilipa deni letu lote, ni sisi tu kwenda kwake kwa kutubu tukimaanisha kuacha dhambi ili atusamehe na tuishi maisha ndani yake, hapo ukifa unaenda mbinguni.Watu wawili, Suzana mtitu(38) na Kassim Kitamkanga(35)wakazi wa Makambako Mkoani Njombe wamekutwa wamefariki katika msitu wa Tanwat uliopo Njombe huku uchunguzi ukibainisha kuwa wameuawa na mganga wa jadi baaya ya wateja hao kugundua kuwa dawa za kuwa matajiri walizopewa hazijafanya kazi.
RPC wa Njombe Hamis Issah amesema jeshi la Polis linamshikilia mganga huyo wa huyo Kienyeji, Joseph Mgunda(41)mkazi wa Sovi kata ya Mtwngo Wilayani Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
"Watu wengi wafanyabiashara huyu mganga anawaambia ukipeleka hela anaziombea halafu baadaye zinaongezeka, sintofahamu iliyotokea kwa hawa watu wawili walipewa walipewa dawa tayari lakini wakaona matokeo hayaleti mafanikio wakaenda kumuuliza mganga mbona umetupa dawa ambayo haisaidii, mganga huyo alishikwa na hofu na kushauriwa na ndugu zake kutekeleza mauaji hayo"
"Ndugu zake wakamwambia ukitaka usipate shida wauwe hawa watu na kweli watu watatu na yeye mwenyewe mganga akiwa ni wanne wakatekeleza mauwaji. Mwanaume alikatwa mapanga sehemu za shavuni upande wa kulia na kushoto na kichwanina pia kapigwa rungu na kudondoka na mwanamke alipigwa rungu moja tu na kudondoka chini"
Kamanda Issah amesema watu wengine wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauwaji hayo ni Andrew Vahuruka, Gadi Mwanzalila9(36) na Kelvin Kilinge(29), Kamanda Issah ametoa wito kwa wananchi kutafuta pesa kwa juhudi za kufanya kazi na si kutafuta utajiri kwa waganga kwa kuwa utajiri unaoletwa na waganga.
Kwani nae alifia kwa mganga?Yale yale ya super summy
Aliuwawa na mganga?Yale yale ya super summy
Sasa mganga, mchawi, mshirikina jumlisha chifu unaweza kutofautisha hapo? Hao wote idara moja ni vitengo tuKwani ni lazima 'chifu' awe mganga?
Mimi sio mmoja wao
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wangesogea kule Makete kwa Mwakipande au kwa Meseketwa kupata utajiri.. Wao wameishia Njombe tu .
'Chief' si kiongozi wa kabila tu?... Au kwa sababu kuna mila ndio kunamfanya yeye mganga?Sasa mganga, mchawi, mshirikina jumlisha chifu unaweza kutofautisha hapo? Hao wote idara moja ni vitengo tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo chief unayo isema hapa sio, hao machifu tunawajua na kila kabila wapo ndiyo utawakuta kina mtemi, mwene majina yao hayo, sasa wewe kama huamini nenda kwa chifu wa Urwira - Katavi kisha urudi hapa'Chief' si kiongozi wa kabila tu?... Au kwa sababu kuna mila ndio kunamfanya yeye mganga?
Ina maana kina Mirambo,Mkwawa, Isike,Abushiri hawa wote walikuwa waganga?
Wote hao vigagula'Chief' si kiongozi wa kabila tu?... Au kwa sababu kuna mila ndio kunamfanya yeye mganga?
Ina maana kina Mirambo,Mkwawa, Isike,Abushiri hawa wote walikuwa waganga?