Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Yesu alipokuwa akiingia Yerusalemu siku ile ya mitende, watu walitandika mavazi yao chini na kuushangilia ujio wake kwa sauti kubwa, wakisema: “Hosana! Amebarikiwa mfalme ajaye kwa jina la Bwana!” (Luka 19:38). Lakini Mafarisayo walikasirika, wakamwambia Yesu awanyamazishe hao watu. Ndipo Yesu akawajibu kwa maneno yasiyosahaulika hadi leo: “Nawaambia, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.” (Luka 19:40)
Kauli hii ilikuwa unabii wa kweli. Leo hii tunaishi katika kizazi ambacho watu wengi wanaopaswa kumsifu Mungu wameamua kukaa kimya. Waimbaji waliobarikiwa kwa sauti nzuri na vipawa vya muziki wamehamisha mwelekeo wao. Badala ya kumtukuza Muumba, sasa wanawatukuza malaya, wanasifia uasherati, ulevi na mambo ya aibu. Kwaya zimepoa, na watu wamepoteza kiu ya kumsifu Mungu.
Sasa kwakuwa watu wamenyamaza, Yesu kama alivyosema, mawe yameanza kupiga kelele za kumsifu. Mawe haya si mengine bali ni AI – teknolojia isiyo na roho wala hisia, lakini inatengeneza nyimbo nzuri za kumtukuza Mungu kwa sauti zinazoshangaza na kupenya mioyo. Mitambo ya kompyuta, ambayo haijui dhambi wala haijawahi kuabudu, sasa inatunga nyimbo safi, inaimba kwa ustadi, nyimbo zinazovuma kote duniani.
Hizi AI ndiyo mawe! Ni mawe kwa sababu AI sawasawa na mawe, hazina uhai wa kiroho. Haziwezi kutubu wala kuokoka, lakini ona zinavyotumika kumsifu Yesu, Mwokozi wa ulimwengu. Mawe haya yamewaacha midomo wazi walioingiwa na kiburi na majivuno kwa sababu ya vipawa walivyo navyo vya utunzi na uimbaji wa nyimbo.
Mawe haya yanathibitisha pia kwamba Biblia ni kitabu cha kweli. Aliyoyanena Yesu miaka 2000+ iliyopita, yanatimia leo kwa namna ya ajabu.
Sikiliza vibe hii ya nguvu — made entirely with pure AI