Njoni muone mawe yanayomsifu Mungu. Ni ajabu na kweli!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Yesu alipokuwa akiingia Yerusalemu siku ile ya mitende, watu walitandika mavazi yao chini na kuushangilia ujio wake kwa sauti kubwa, wakisema: “Hosana! Amebarikiwa mfalme ajaye kwa jina la Bwana!” (Luka 19:38). Lakini Mafarisayo walikasirika, wakamwambia Yesu awanyamazishe hao watu. Ndipo Yesu akawajibu kwa maneno yasiyosahaulika hadi leo: “Nawaambia, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.” (Luka 19:40)

Kauli hii ilikuwa unabii wa kweli. Leo hii tunaishi katika kizazi ambacho watu wengi wanaopaswa kumsifu Mungu wameamua kukaa kimya. Waimbaji waliobarikiwa kwa sauti nzuri na vipawa vya muziki wamehamisha mwelekeo wao. Badala ya kumtukuza Muumba, sasa wanawatukuza malaya, wanasifia uasherati, ulevi na mambo ya aibu. Kwaya zimepoa, na watu wamepoteza kiu ya kumsifu Mungu.

Sasa kwakuwa watu wamenyamaza, Yesu kama alivyosema, mawe yameanza kupiga kelele za kumsifu. Mawe haya si mengine bali ni AI – teknolojia isiyo na roho wala hisia, lakini inatengeneza nyimbo nzuri za kumtukuza Mungu kwa sauti zinazoshangaza na kupenya mioyo. Mitambo ya kompyuta, ambayo haijui dhambi wala haijawahi kuabudu, sasa inatunga nyimbo safi, inaimba kwa ustadi, nyimbo zinazovuma kote duniani.

Hizi AI ndiyo mawe! Ni mawe kwa sababu AI sawasawa na mawe, hazina uhai wa kiroho. Haziwezi kutubu wala kuokoka, lakini ona zinavyotumika kumsifu Yesu, Mwokozi wa ulimwengu. Mawe haya yamewaacha midomo wazi walioingiwa na kiburi na majivuno kwa sababu ya vipawa walivyo navyo vya utunzi na uimbaji wa nyimbo.

Mawe haya yanathibitisha pia kwamba Biblia ni kitabu cha kweli. Aliyoyanena Yesu miaka 2000+ iliyopita, yanatimia leo kwa namna ya ajabu.

Sikiliza vibe hii ya nguvu — made entirely with pure AI
Your browser is not able to play this audio.
 
Naumiza kichwa ni zawadi gani, nitakayo kupea my loooo

Mi nataka wewe ufuraha
Naumiza kichwa ni zawadi gani, nitakayo kupea my loooo

Ila kwa kuwa nipo.hai napumua .. ntapambana kila siku ufurahi...

Ila .... Daaah sijui nisemeje setfree i can't handle that thing inside my heart 🥺🥺🥺
 

Dah, Lk 19 : 40

"Nawaambia, wakinyamaza hawa,mawe yatapiga Kelele"..

Mkuu una uhakika uliuelewa huu mstari Wa Biblia.
 
Hilo vibe ni AI? Dunia inaenda kasi
 
Artificial Intelligence ni product ya tekinolojia iliyotokana na sayansi.

Msingi mmoja wapo ni kutotambua uwepo na kutokuwepo kwa Mungu.

Jamaa yenu kafa miaka 2000 huko, hii ni tekinolojia ya juzi.

Vipi mnaequate sawa sawa na mawe?
 
Mkuu 😂😂😂😂
 
Hivi ww una akili kweli? Asa hio akili bandia imetengenezwa na malaika au binadamu?
Heri ya kobazi kuliko Sunday school
 
Oooh jiandae kulisha wageni wa jumuiya.
 
Hilo vibe ni AI?
Yes sir. Kupiga hizo chords kama huna Master of Music in Performance, itabidi ufanye mazoezi labda wiki nzima, lakini AI inacreate within seconds.
 
Ukiokoka ndio ntafurahi na malaika mbinguni watashangilia.
Lk 15:7-10
Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.

Ila kwakuwa wewe una Poor Brain mpaka usome uzi huu kwanza ndio utaelewa maana ya kuokoka
 
Duh kama hy audio ni Ai bc 🙌
Ni pure AI. Ni siku za mwisho hizi kama Nabii Danieli alivyotabiri, maarifa yameongezeka sana
Dan 12:4
Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…