Njoo tukosoane/tuelimishane

Njoo tukosoane/tuelimishane

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,508
Reaction score
2,619
Njoo tukosoane.

Andika kitu chochote unachoamini au kuwa na uhakika nacho kwamba ni cha kweli unavyofahamu wewe halafu member mwingine atakuja kukukosoa.

Mfano mimi siku zote nilikuwa nafahamu kuwa zile ndege zinazoacha mstari angani zilikuwa ni rocket na ile mistari ni moshi

Kumbe sivyo
Zile ni ndege na ile mistari ni mafuta yanayomwagwa, kuna uzi humu JF ulikuja kunikosoa

Uzi hauhusiani na yale usiyoyajua (Je, wajua?) bali ni yale unayoyajua halafu kumbe sivyo unavyojua wewe.

NB: Tusikosoane kwa lugha chafu, lengo la uzi ni kupanua ufahamu na kuelimishana zaidi.

Let's go!!

#MapachaDaima
 
Bado sijapata mantiki ya uzi, nini hasa kinahitajika hapa?
 
Zinaitwa Contrails.

Nilisoma zinazosababishwa na engine ya ndege ambayo inakuwa na joto halafu inafika kwenye hali ya ubaridi "cold air". (Hapa kuna maelezo ya kitaalamu nimeyasahau).

Na hizo zinategemea na temperature ya hiyo siku. Siku ambayo haikutani na cold temperature huko juu basi inakuwa haiachi chochote. Siku wakikutana na cold temperature changanya na joto la kwenye engine ndiyo inatoa hizo Contrails.

Sikumbuki vizuri nasubiri kukosolewa.
 
Kwa kifupi, Ile mistari mirefu mfano wa mawingu ni mvuke ulioganda.

Huo mvuke wa maji-maji unaozalishwa na mabaki ya nishati unapotolewa kutoka katika injini na kukutana na joto la anga la kiwango cha chini lililopo katika umbali mrefu sana kutoka katika uso wa dunia (altitude), ndiyo husababisha hiyo mistari kutokea ama kuonekana.
 
Mwanga tunaouona usio na rangi utokanao na jua ni muunganiko wa mianga saba yenye rangi saba tofauti, kwa kiingereza ni kama zifuatazo Violet, Indigo,Blue,Yellow, Orange,Green and Red.

Nimesoma hivyo na ninaamini hivyo.

Karibu wa kunikosoa...
 
I
Mwanga tunaouona usio na rangi utokanao na jua ni muunganiko wa mianga saba yenye rangi saba tofauti, kwa kiingereza ni kama zifuatazo Violet, Indigo,Blue,Yellow, Orange,Green and Red.

Nimesoma hivyo na ninaamini hivyo.

Karibu wa kunikosoa...
indigo ni rangi gani!?
 

Attachments

  • images.png
    images.png
    2 KB · Views: 2
Back
Top Bottom