Njoo tukumbushane visa na matukio kutoka kwa viranja ,mamonitor wa secondary na primary:

Mi nilipewa umonitor form 2...na mwalimu wa darasa sio kwa kua nilikua na akili au mstaarabu bali mkorofi niliyetukuka..sasa aliona akinipa umonitor nitakua mpole nk.
Lakin haikua ivyo nilikua naandika majina ya noise maker jumatatu tu...na hayo majina nayatumia kuanzia j.tatu had ijumaa...yani kama upo j.tatu utapigwa hadi ijumaa.
Siku mwalimu alipogundua nilipigwa mno..mno...na kibarua kikaota nyasi...mbez beach 2004-2008..it was awesome.
 
Nilikuwa Monitor la sita sasa bhna kuna kademu Nilikuwa nakapenda sanaa... Yani hata kapigee kelele vip nilikuwa Simuanindiki...!! Siku nkaja semewa kwa mwalimu flani hivi nae akataka kujua ka nikweli..akatega akawachungulia dirishani kwa mda ka wa dakika kumi... Kile kimanzi kinapiga kelele na wenzie hatari ile mwalimu kaingia darasa lote kimya...Kuulizia majina yule manzi hayupoo...!!!


Haa ha ha ha...sitaki kukukumbuka zile mbokoo dadekii.. nlikuwa nkishika kalio nazihesabu...
 
Nilikua monitor form two na three Ajabu nlikua MBABE ila walikua wananipendekeza wenyewe kua kiongozi form 3 muhula wapili nikawa kiranja wa nidhamu shule ilinyooka ikakaa kwenye reli darasani kwangu nlikua nikisema sitaki kelele hadi head boy anakaa kimya... Maisha bwana nmefika chuo sikutaka kabisa uongozi na saivi me ni mpole mpk najishtukia aisee maisha yanaenda kasi sana sitaisahau shule yangu chief senge sec Singida mjini.
 
nakumbuka nilifukuzwa Ifunda baada ya kumwambia kiranja hutufai na huna uwezo wowote ..ila nikaaambiwa niame shule niondoke pale basi nikapelekwa Dom sec ipo dodoma ..Enzi izo mkuu alikua Mhaya mmoja anaitwa kaishozi. Eti kulikua kuna kiranja alikua anapigisha watu Magoti nikamfata nikamwambia haya mamlaka yakupigisha watu magoti umeyatoa wapi? nikamwambia wewe ni mwanafunzi tu kama hawa wenzako kazi wewe uwe mtetezi wa sisi sio haya unayofanya..tulibishana sana akanishtaki kwa mkuu kaishoz mkuu akaniita akaniambia kwanzia wewe ndo kaka mkuu full stop yule jamaa mpaka leo ananiambiaga brother ulikua na akili ukiwa mtu mdogo saana..
 
Nilikua kafupi hafu kadogo enzi za prima.. la sita nilimtwanga Ticha wa sayansi mpaka leo heshima ipo Chezea kidono wewe.
Sec nilipataga history 26 hafu chini ya C kuna bakola aisee nilidundwa hadi mabinti wanalia..
Mtundu, ukorofi, upole, fujo vyote vyanguu..
Tulikua tunaenda shule na gunia la mahindi hafu tunayapika porini saa sita tunayazukia..
 
Ule mchezo wa kuweka kioo chini halaf wasichana wakipita unaona mambo sitosahau...siku nmetega kioo halaf akapita mwalimu mkuu
Umenikumbusha ayo mambo tulikuwa tunawaangalia afu tunatafta karatasi tunaanza kuchora kila mtu na rangi ya chupi yake kuna siku monitress alitushitaki kwa mwalim mkuu tukaitiwa wazazi tulichezea kichapo never seen
 
Mm primary nlikuwa mtundu sana...nakumbuka tuliiba ubwabwa tukaenda kula chooni ...kipindi cha sayansi kimu watu wamepika ubwabwa wakarudi class nkabeba sufuria lote
 
Mm primary nlikuwa mtundu sana...nakumbuka tuliiba ubwabwa tukaenda kula chooni ...kipindi cha sayansi kimu watu wamepika ubwabwa wakarudi class nkabeba sufuria lote
Mi nakumbuka tulikuwa na kundi letu tunachanga pesa tunaenda kupikia ubwabwa porini kuiba mihogo na mafenesi pia nakumbuka m na jamaa yangu alikuwa kiranja tuliiba mipira ya shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…