Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

ushalishwa maduse
 
yule ambaye mwandan wake ndo mumtafute anayo
 
Tafuta mganga mdau ushalishwa mauzauza
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah umenchekesha sana mkuu.......umekula mbio [emoji119][emoji119]
 
Sana,mi ningeenda kumripoti police huyo muuaji
 
Kisa kama hiki kiliwahi tokea Dodoma maeneo ya Area A
Jirani na shule ya msingi chamwino
Miaka ya mwanzoni 2000 hukoo
 
NILISIMULIWA TU;Kuna muhubiri mmoja wa kilokole,alienda kuhubiri kijijini mkoani rukwa,
Uwanja wa kanisa la mahubiri ulikuwa jirani na kilabu cha pombe za kienyeji,sasa yule muhubiri akawa anahubiri kuwa kunywa pombe ni dhambi,utachomwa moto,sasa yale maneno yakawachoma sana wauzaji na wanywaji.

Siku ya tatu wakamfuata mchungaji wa kanisa lile wakimwambia,amwambie muhubiri arekebishe mahubiri yake,lakini muhubiri na mchungaji wakagoma,c unajua walokole nao kwa utata.

Siku iliyo iliyofuata,wale jamaa wakakusanya fimbo nyingi sana,wakazjficha kilabuni,wakawa wanasubiri muhubiri afike jioni kidogo wakatembeze bakora mkutano wote, Sasa pale kijijini kulikuwa na mwendawazimu mmoja alikuwa mkorofi na ana nguvu sana,na hapo kijijini watu wote walikuwa wanamwogopa sana,maana aliwahi kuua mtu.

Ghafla huyo mwendawazimu akashika fimbo kubwa akawa anachapa watu kilabuni,anawambia nendeni mkutanoni wote,ikawa mshikemshike,pale mkutanoni wakashanga ghafla watu wamejaa,huku wanahema.

Kwa mbali wakamuona yule chizi anakuja, na alipokaribia akatupa fimbo zake,akaenda mbele akasema anataka kuokoka, wote wakawa hawaamini, wanamuogopa, yule mhubiri akamwombea,akanyoa na nywele,wakampa na nguo nzuri,akapona uchizi wake
Hivi tunavyoongea ana familia na ni mhubiri wa injili
,,,HAKIKA MAISHA NI YA MUNGU...
 
Eti nimezingua....

Kiongozi ngoja nimalizie kucheka 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…