Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

kivipi ,hebu fafanua mkuu
Imani ni kitu cha ajabu ....hapo tayr ushaamini kuwa bila hako kadude nothing gonna work so ukijaribu kujitoa utapata tabu sana

But in at the end of day return....utalipia
In every magic..... there is price to pay
 
Imani ni kitu cha ajabu ....hapo tayr ushaamini kuwa bila hako kadude nothing gonna work so ukijaribu kujitoa utapata tabu sana

But in at the end of day return....utalipia
In every magic..... there is price to pay
Absolutely.
 
Kudadeki,ungepigwa za uso hapo..acha tabia ya kuomba omba namba za simu hovyo.
 
Duh pole Sana Mkuu, ila Mungu mwema upon hai Hadi leo
 
Baada ya kuzisoma story mbalimbali za kutisha ambazo watu wamezipitia katika uzi huu bila shaka na mimi pia nimeshuhudia uhalisia wa nguvu za giza kwa macho yangu haya mawili.

Wakati ule wa miaka ya Tisiini na moja au mbili nilikua nalala na braza wangu katika chumba kidogo pale nyumbani ambacho baadae kilikuja kutumika kama Jiko. Mkabala na chumba icho tulikua tumepakana na nyumba moja ya mama wa kiruguru ambae ndie mwanzilishi wa mji ule(aliewauzia watu wote viwanja eneo lile) na alikua akisifika kama Gwiji au mchawi katika eneo lile. huyo mama alikua na watoto wanne niliowafahamu, wa mwisho alikua wa kiume alimfatia alikua wa kike alafu dada yao tena na wa kwanza alikua wa kiume (bwana Shaabani).
Siku iyo tukiwa tumelala mzungu wa nne mimi nikiwa wa kwanza na kaka yangu akiwa upande wa ukutani usiku mkubwa kama mida ya nane ghafla nilistuka kutoka usingizini nipo ndani ya shuka ilihali kichwa changu kipo nje ya shuka nilikua nimelala chali nikitizama juu, ndipo nilipomwona live yule mtoto wa kiume wa mwisho wa jirani akiwa amemkalia kaka yangu kwenye mapaja na alikua akimkanda tumbo lake yaani kama vile mtu anakanda unga wa ngano kwenye beseni. wakati naendele kushuhudia anachokifanya nahisi alijua kama mimi nipo macho hivyo akawa anateremka kitandani, wakati anashuka kitandani mimi nikageuka nikalalia ubavu na kuvuta shuka mpaka kichwani(gubigubi). Alisogea upande wangu wa kichwani na kukaribisha uso wake karibu na uso wangu nikiwa ndani ya shuka bhasi nilipokua najaribu kuvuta shuka ili nione anafanya nini nikawa nakutana nae macho kwa macho yaani lile shuka ndo lilikua linatutenganisha. nililala kwa shida sana usiku huo mpaka nilipoona mwanga dirishani nilipoangaza vizuri sikuona mtu sijui alitokaje mle ndani.
Siku iliyofata nikamsimulia familia yangu tukakubaliana kusali kwa pamoja kabla ya kulala na utaratibu ukawa huo.
Siku nyingine kabisa tukiwa tumelala usiku nahisi mda kama ule wa siku ile nikastuka tena, upande ule wa kwangu nilipokua nimelala mwanzo wa kitanda ndipo nilipomwona msichana(yule binti wa pili kwa yule jirani) akiwa amekaa katika kitanda huku miguu ikiwa chini(yaani kama vile kwenye chumba huna kiti sasa unaweka kitako kwenye kitanda) alafu alikua kama vile anasoma kitabu kikiwa kakipakata kwenye mapaja yake, yaani alikua ametulia akiangalia chini kana kwamba ame-concentrate na kile kitabu ilihali ni giza mle ndani. nilijaribu kujitingisha labda ataniangalia waapi alikaa vile vile mpaka nakuja kustuka asubui sikukuta mtu. nikasimulia tena familia wakasema tuongeze masaa ya kusali ila jamaa zangu maskani walitushauri tulale na sindano na ndimu ili ntakapowaona nichome sindano kwenye ndimu asubui tumkamate mchawi lakini havikufanya kazi.
Mi nakubali uchawi upo hata katika vitabu vya Mungu uchawi umetajwa zaidi ya mara elfu tatu.
 
Hapana ni tabora ndio ila shule haiitwi mwenge ila kwa sasa hiyo wilaya inaitwa uyui zamani ilikuwa inaitwa tabora vijijini
Nmekupata mkuu. Shule ni MTAKUJA kijiji Mtakuja, pembeni kuna main road na mlimani ndo kuna miti ya ubani
 
Noma na nusu
 
Hatari saaana
 
Sikujua kama kuna siku nitakuja kuiba biblia moaka siku nilipolala kwa mama mkubwa. Hiyo siku walikuja nikaba live kabisa bila chenga. Siku hiyo ndio nilielewa vile watu wanasemaga "nywele zinasisimuka", mimi hazikuishia hapo yan zilisimama kabisaa mpaka vipele vya barid vilinishika usiku wa manane na joto kali Dar hii.
Nimeamka niko macho kabisa ila nahis kabisa kuna mtu/nguvu imesimama kando yangu inani attack, niiltafuta mule ndani bible ilipo nikaikamta huku nasali vya hapa na pale mpaka situation ilipotoweka , kulala naogopa nikakesha nasoma maandiko tu mpaka kunakucha

Ile bible nikaiba nikaondoka nayo.
Toka siku hiyo sikuwah kurud tena kwa mamkubwa licha ya yeye kuwa ndio mtu alienipokea mjini hapa tunabaki kukutana kwenye matukio tu
 
Hiz ni tabia za mke wangu mpaka leo. Unakuta saa 9 za usiku ghafla anaanza kuongea maneno ya kama ana fight, kuna muda mwingine huwa ananena kwa kugha zile za kilokole, kuna muda anaongea kingereza na kuna muta anasali kiswahil kwa kukemea.

Sijui tuna link gani lakin mara zote huwa mimi nashtuka kabla hajaanza kufanya haya so huwa namsikilizaaa moaka anamaliza, i dont know lakin mimi lazima nishtuke tu kabla hajazama kwenye hizi scenario.

Asubuh kukikucha hwa namuuliza vipi mwenzangu leo yalikukuta yapi, basi atakaa kuvuta kumbukumbu ndio ataanza kunisimulia ndoto ambazo huwa anaota na humo kwenye ndoto anakua ana fight against evil spirits, kuna muda huwa inamchukua siku nzima ku memorize ndio anisimulie.

NB.
Kwa mara ya kwanza kabisa ku cheat mimi, yf aliniambia mara 2 kabla kuwa nakuota sana uko na mwanamke mnafanya zinaa, 2 times, nilikua kwenye harakat zangu mwanza, aahh nikamlamba school mate wangu ambaye nilimuepuka sanaa nikiwa chuo na alikua akinipendaga sana
 
Kazi unayo huchepuki
Sema kiimami uko na mtu mzuri sana.
 
Nimeipenda
 
 
Daaah 🙌🙌

Unaweza ukafa kwa presha aise.
 
Na Mimi nitamkie mema/baraka niione hio neema uliyopewa
 
Basi wewe ndo mchawi mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…