Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

kivipi ,hebu fafanua mkuu
Imani ni kitu cha ajabu ....hapo tayr ushaamini kuwa bila hako kadude nothing gonna work so ukijaribu kujitoa utapata tabu sana

But in at the end of day return....utalipia
In every magic..... there is price to pay
 
Absolutely.
 
Ilikuwa mwaka 2009, Kuna siku nimelala nikawa naota kuwa nimepanda daladala kituo cha mwenge naelekea posta basi nikawa nimekaa siti ya nyuma ya Costa.

Basi kufika kituo cha Victoria akapanda mdada mmoja akaja kukaaa karibu yangu siti ya nyuma,tukaendelea na Safari kufika kituo cha mbuyuni yule dada wa ndotoni akaniachia kikaratasi kina namba za simu akashukia kituo cha mbuyuni,baada ya mda nikastuka kutoka ndotoni kucheki saa ya simu mda huo ni saa tisa za usiku.

Basi nimestuka kila kitu kwenye ndoto nilikuwa nakumbuka mpka namba za siku,kesho yake nawahadithia ndugu zangu nilichoota ndotoni na mpka namba za siku zilizokuwa kwenye karatasi nazikumbuka,wakaniambia tujaribu kuzipiga.

Baada ya kupiga anapokea msichana ana lafudhi ya kiarabu anaitwa Nasrat na anaishi sinza,nilichofanya ni kuvunja laini na kutafuta line nyingine mpka leo sielew ile ndoto na coincidence zake
Kudadeki,ungepigwa za uso hapo..acha tabia ya kuomba omba namba za simu hovyo.
 
Kaka mtoto wa mama mkubwa alienda kutandika kitanda baada ya kula usiku waende kulala.Pembeni ya nyumba yao kulikua na msufi mkuuuuuuuubwa ndio mti mkubwa zaidi pale kijijini.

Alipoenda kutandika hakurudi tena hadi saa linapita mtu hatoki ndani, kwenda kumtafuta hayupo! Walimuwinda nyumba nzima hawamuoni karibia masaa 3 nyumba yote hawaoni mtoto. Baadae walimuona chini ya meza ya kula (ndogo tu) kajikunyata hawesi kuongea. Wakampeleka kwa mganga usiku huo huo kafanyiwa dawa ndio akaanza kuongea kua kuna kitu kilimchukua kikampeleka ndani ya huo msufi.

Tumewangiwa utotoni kinoma noma..ilibidi mama ahamishe kitanda tulale chumbane mwake. Alikua akiwasha kibatali aone vizuri ndani anaona kiganja kinazima kibatali.

Wachawi waliniiba wakanitoa chumbani wanipeleka kunilaza chini ya mtungi..kwenye kona la nyumba. Walinipata asubuhi nikiwa nimesinzia nimefunikwa ushungi kama mtoto mchanga.

RIP kuna mbwa wetu alikua anapambana nao usiku wakamuuua
Duh pole Sana Mkuu, ila Mungu mwema upon hai Hadi leo
 
Baada ya kuzisoma story mbalimbali za kutisha ambazo watu wamezipitia katika uzi huu bila shaka na mimi pia nimeshuhudia uhalisia wa nguvu za giza kwa macho yangu haya mawili.

Wakati ule wa miaka ya Tisiini na moja au mbili nilikua nalala na braza wangu katika chumba kidogo pale nyumbani ambacho baadae kilikuja kutumika kama Jiko. Mkabala na chumba icho tulikua tumepakana na nyumba moja ya mama wa kiruguru ambae ndie mwanzilishi wa mji ule(aliewauzia watu wote viwanja eneo lile) na alikua akisifika kama Gwiji au mchawi katika eneo lile. huyo mama alikua na watoto wanne niliowafahamu, wa mwisho alikua wa kiume alimfatia alikua wa kike alafu dada yao tena na wa kwanza alikua wa kiume (bwana Shaabani).
Siku iyo tukiwa tumelala mzungu wa nne mimi nikiwa wa kwanza na kaka yangu akiwa upande wa ukutani usiku mkubwa kama mida ya nane ghafla nilistuka kutoka usingizini nipo ndani ya shuka ilihali kichwa changu kipo nje ya shuka nilikua nimelala chali nikitizama juu, ndipo nilipomwona live yule mtoto wa kiume wa mwisho wa jirani akiwa amemkalia kaka yangu kwenye mapaja na alikua akimkanda tumbo lake yaani kama vile mtu anakanda unga wa ngano kwenye beseni. wakati naendele kushuhudia anachokifanya nahisi alijua kama mimi nipo macho hivyo akawa anateremka kitandani, wakati anashuka kitandani mimi nikageuka nikalalia ubavu na kuvuta shuka mpaka kichwani(gubigubi). Alisogea upande wangu wa kichwani na kukaribisha uso wake karibu na uso wangu nikiwa ndani ya shuka bhasi nilipokua najaribu kuvuta shuka ili nione anafanya nini nikawa nakutana nae macho kwa macho yaani lile shuka ndo lilikua linatutenganisha. nililala kwa shida sana usiku huo mpaka nilipoona mwanga dirishani nilipoangaza vizuri sikuona mtu sijui alitokaje mle ndani.
Siku iliyofata nikamsimulia familia yangu tukakubaliana kusali kwa pamoja kabla ya kulala na utaratibu ukawa huo.
Siku nyingine kabisa tukiwa tumelala usiku nahisi mda kama ule wa siku ile nikastuka tena, upande ule wa kwangu nilipokua nimelala mwanzo wa kitanda ndipo nilipomwona msichana(yule binti wa pili kwa yule jirani) akiwa amekaa katika kitanda huku miguu ikiwa chini(yaani kama vile kwenye chumba huna kiti sasa unaweka kitako kwenye kitanda) alafu alikua kama vile anasoma kitabu kikiwa kakipakata kwenye mapaja yake, yaani alikua ametulia akiangalia chini kana kwamba ame-concentrate na kile kitabu ilihali ni giza mle ndani. nilijaribu kujitingisha labda ataniangalia waapi alikaa vile vile mpaka nakuja kustuka asubui sikukuta mtu. nikasimulia tena familia wakasema tuongeze masaa ya kusali ila jamaa zangu maskani walitushauri tulale na sindano na ndimu ili ntakapowaona nichome sindano kwenye ndimu asubui tumkamate mchawi lakini havikufanya kazi.
Mi nakubali uchawi upo hata katika vitabu vya Mungu uchawi umetajwa zaidi ya mara elfu tatu.
 
Hapana ni tabora ndio ila shule haiitwi mwenge ila kwa sasa hiyo wilaya inaitwa uyui zamani ilikuwa inaitwa tabora vijijini
Nmekupata mkuu. Shule ni MTAKUJA kijiji Mtakuja, pembeni kuna main road na mlimani ndo kuna miti ya ubani
 
Noma na nusu
 
Hatari saaana
 
Sikujua kama kuna siku nitakuja kuiba biblia moaka siku nilipolala kwa mama mkubwa. Hiyo siku walikuja nikaba live kabisa bila chenga. Siku hiyo ndio nilielewa vile watu wanasemaga "nywele zinasisimuka", mimi hazikuishia hapo yan zilisimama kabisaa mpaka vipele vya barid vilinishika usiku wa manane na joto kali Dar hii.
Nimeamka niko macho kabisa ila nahis kabisa kuna mtu/nguvu imesimama kando yangu inani attack, niiltafuta mule ndani bible ilipo nikaikamta huku nasali vya hapa na pale mpaka situation ilipotoweka , kulala naogopa nikakesha nasoma maandiko tu mpaka kunakucha

Ile bible nikaiba nikaondoka nayo.
Toka siku hiyo sikuwah kurud tena kwa mamkubwa licha ya yeye kuwa ndio mtu alienipokea mjini hapa tunabaki kukutana kwenye matukio tu
 
Nakumbuka miaka ya 13 hv na kuendelea nami nlikuwa hvyo,mfano unakuta kila ikifika saa9 usik kamil naanza kusali huku ndani ya nafs yangu napata msukumo sana wa kusali huku nazifeel negative energies,hapo nakuwa na sali sana hadi nalia huko usingizini,yaan nasali kama mtu kasimama juu ya kilima anatazama bondeni lengo sauti isikike basi hapo.
Hapo ndio ntaanza kuhisi kabisa zile negative energies zinatoweka halafu nami ndio naamka huku natota jasho ijapokuwa njombe ni baridi

Kwakweli namuomba Mungu anipe nguvu nirudi ktk himaya yake maana dah
Hiz ni tabia za mke wangu mpaka leo. Unakuta saa 9 za usiku ghafla anaanza kuongea maneno ya kama ana fight, kuna muda mwingine huwa ananena kwa kugha zile za kilokole, kuna muda anaongea kingereza na kuna muta anasali kiswahil kwa kukemea.

Sijui tuna link gani lakin mara zote huwa mimi nashtuka kabla hajaanza kufanya haya so huwa namsikilizaaa moaka anamaliza, i dont know lakin mimi lazima nishtuke tu kabla hajazama kwenye hizi scenario.

Asubuh kukikucha hwa namuuliza vipi mwenzangu leo yalikukuta yapi, basi atakaa kuvuta kumbukumbu ndio ataanza kunisimulia ndoto ambazo huwa anaota na humo kwenye ndoto anakua ana fight against evil spirits, kuna muda huwa inamchukua siku nzima ku memorize ndio anisimulie.

NB.
Kwa mara ya kwanza kabisa ku cheat mimi, yf aliniambia mara 2 kabla kuwa nakuota sana uko na mwanamke mnafanya zinaa, 2 times, nilikua kwenye harakat zangu mwanza, aahh nikamlamba school mate wangu ambaye nilimuepuka sanaa nikiwa chuo na alikua akinipendaga sana
 
Kazi unayo huchepuki
Sema kiimami uko na mtu mzuri sana.
 
Mi binafsi sijawahi kuona mambo ya kutisha Sana ila nmeshuhudia utaalam wa hayo mambo.

Nina mjomba wangu anaishi msumbiji huwa anakujaga Tanzania kuwasaidia watu wenye matatizo mbali mbali ila somehow ni nyang'au na Mimi ni rafiki yangu sana so huwa ananiambia kila kitu and huwa haogopi ananiamini sana.

Kuna siku Kuna msanii mkubwa tu wabongo flava 2012 alikuja home Mtwara anataka kusafishiwa nyota sijui sasa alifatana na mwanamke mmoja anadai ni mke wa mkubwa serikarin anataka kumtuliza mmewe sijui asa uncle tukiwa pale chumbani night akamwambia yule mama anahitaji nywele za sehem ya Siri za mmewe Yule mama Hana na haezi safiri Kwenda Dar usiku ule mi niko nachezea sim huku naskiliza uncle akamwambia atoe 200k atume kijana afate Dar. mama akauliza itachukua siku ngapi uncle akacheka akamwambia saizi tu zinaletwa. Mi nikapause kidogo sikuelewa kauli nikasema uncle mbona kama anataka kumpiga chnga la macho huyu madame anapataje nywele ziko Dar within few minutes. Sasa bhana mama kishingo upande akasema sawa, bas uncle akajifunika nguo nyeupe baada ya kupewa jina kamili akaongea ongea kidogo na kiarabu juu then akajifunua story zikaendelea na mambo mengine. Ndani ya dakika kama 10 hizi akawanyamazisha akachukua karatasi nyeupe kama anakinga kitu juu ile kutua chini nywele hizi hapa [emoji23] kazi ikafanyika asubuhi yule mama anakuja anatuambia mmewe kampigia na meseji katuma katuonesha anasema amtafute mtaalam huku Mtwara maana anahisi wakubwa wenzake wanamchezea wamemnyoa nywele zote za Siri am'bebee dawa ikibidi maana ye alimuaga amekuja Mtwara kufanya survey ya mazao [emoji23][emoji23] bas nilishtuka nikamuuliza uncle imekuaje akacheka akasema nitakusimulia kesho. Akanambia vyote alivyofanya.

Cha pili Kuna mtu alimuagiza alete kunguru mzima ambae sio mkubwa Sana jamaa akasema hawezi winda kunguru kwanza wasumbufu atapata shida uncle akasema leta 20k ya supu nkuwindie ile jamaa kutoa pale pale unlce kaongea ongea nini sijui kunyoosha mkono juu akatua kunguru toka juu ya mwembe Hadi mkononi hii sikushtuka nlicheka maana jamaa akawa anamwambia uncle amrudishie hata buku 10k maana kamshika kirahisi [emoji23][emoji23] uncle akampa buku5 Tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Experience yangu na uncle imenifanya niamini haya mambo

Ahsante
Nimeipenda
 
Baada ya kuzisoma story mbalimbali za kutisha ambazo watu wamezipitia katika uzi huu bila shaka na mimi pia nimeshuhudia uhalisia wa nguvu za giza kwa macho yangu haya mawili.

Wakati ule wa miaka ya Tisiini na moja au mbili nilikua nalala na braza wangu katika chumba kidogo pale nyumbani ambacho baadae kilikuja kutumika kama Jiko. Mkabala na chumba icho tulikua tumepakana na nyumba moja ya mama wa kiruguru ambae ndie mwanzilishi wa mji ule(aliewauzia watu wote viwanja eneo lile) na alikua akisifika kama Gwiji au mchawi katika eneo lile. huyo mama alikua na watoto wanne niliowafahamu, wa mwisho alikua wa kiume alimfatia alikua wa kike alafu dada yao tena na wa kwanza alikua wa kiume (bwana Shaabani).
Siku iyo tukiwa tumelala mzungu wa nne mimi nikiwa wa kwanza na kaka yangu akiwa upande wa ukutani usiku mkubwa kama mida ya nane ghafla nilistuka kutoka usingizini nipo ndani ya shuka ilihali kichwa changu kipo nje ya shuka nilikua nimelala chali nikitizama juu, ndipo nilipomwona live yule mtoto wa kiume wa mwisho wa jirani akiwa amemkalia kaka yangu kwenye mapaja na alikua akimkanda tumbo lake yaani kama vile mtu anakanda unga wa ngano kwenye beseni. wakati naendele kushuhudia anachokifanya nahisi alijua kama mimi nipo macho hivyo akawa anateremka kitandani, wakati anashuka kitandani mimi nikageuka nikalalia ubavu na kuvuta shuka mpaka kichwani(gubigubi). Alisogea upande wangu wa kichwani na kukaribisha uso wake karibu na uso wangu nikiwa ndani ya shuka bhasi nilipokua najaribu kuvuta shuka ili nione anafanya nini nikawa nakutana nae macho kwa macho yaani lile shuka ndo lilikua linatutenganisha. nililala kwa shida sana usiku huo mpaka nilipoona mwanga dirishani nilipoangaza vizuri sikuona mtu sijui alitokaje mle ndani.
Siku iliyofata nikamsimulia familia yangu tukakubaliana kusali kwa pamoja kabla ya kulala na utaratibu ukawa huo.
Siku nyingine kabisa tukiwa tumelala usiku nahisi mda kama ule wa siku ile nikastuka tena, upande ule wa kwangu nilipokua nimelala mwanzo wa kitanda ndipo nilipomwona msichana(yule binti wa pili kwa yule jirani) akiwa amekaa katika kitanda huku miguu ikiwa chini(yaani kama vile kwenye chumba huna kiti sasa unaweka kitako kwenye kitanda) alafu alikua kama vile anasoma kitabu kikiwa kakipakata kwenye mapaja yake, yaani alikua ametulia akiangalia chini kana kwamba ame-concentrate na kile kitabu ilihali ni giza mle ndani. nilijaribu kujitingisha labda ataniangalia waapi alikaa vile vile mpaka nakuja kustuka asubui sikukuta mtu. nikasimulia tena familia wakasema tuongeze masaa ya kusali ila jamaa zangu maskani walitushauri tulale na sindano na ndimu ili ntakapowaona nichome sindano kwenye ndimu asubui tumkamate mchawi lakini havikufanya kazi.
Mi nakubali uchawi upo hata katika vitabu vya Mungu uchawi umetajwa zaidi ya mara elfu tat
 
Nikiwa na umri mdogo kama miaka 15-17 hivi Niliwahi kwenda msibani na shangazi yangu. Kipindi hicho naishi kwake. Tulipofika yeye alielekea kwa wamama (wanawake wenzake) kuendelea na shughuli za jikoni na mambo mengine ya akina mama, mimi nikabaki nje ila maeneo hayo hayo ya msibani.

Nikiwa nimejitenga mbali kidogo na watu alikuja mbaba mmoja sio mkubwa sana na wala sio mzee akakaa nami, alionekana kuhuzunishwa sana na ule msiba. Nilimuamkia akaitika alafu kila mtu akawa kimya.

Baada ya dakika chache akanambia "Kijana, wewe bado mdogo sana. Ukipata nafasi ya kufurahia maisha furahia kadri uwezavyo" nikamwambia "sawa". Wala sikumuelewa ila sikusema neno lengine.

Baada ya muda mwili ukafika na watu wakaanza kuaga, nikasubiri ilivyofika zamu ya watu wengine nami nikaenda kuaga.

Yule mbaba alienambia nifurahie maisha ndo yule alikuwa amelala kwenye jeneza. Oya asikwambie mtu, jasho lilinitoka balaa. Kidogo nianguke mtu wa nyuma yangu akanishika kunisogeza pembeni.

Tulivyorudi nyumbani katika kumuuliza muuliza shangazi akanambia marehemu ana pacha wake na wanafanana balaa. Hata msibani pia alikuwepo. Lakini mbona wakati wa kuaga sikumuona? Mbona aniambie maneno yale?
Daaah 🙌🙌

Unaweza ukafa kwa presha aise.
 
mimi pia sijui ni miongoni mwa hao watu ambao macho yamefungwa, sijui ndio nini mm huwaga ni mgumu sana kulala usingizi ila nikilala huwa nimelala, jambo lolote la hatari watu wengine wanaweza kulisikia mi nisisikie, kuna mwaka nikiwa young kama darasa la 5 hivi Bundi aliliaga mti ambao uko pembeni kabisa na dirisha langu sikusikia hata robo wakati huo karibu mtaa mzima wanamsikia.

haya mambo ya sijui kumwagwa mchanga juu ya bati, watu kutembea wataskia wote mimi nalala sisikii hata tone.

Labda ujanja wa ndoto, nikiota kitu au kusema (foresee) inakua hivyo hivyo imepelekea watu wangu wa karibu hawatakagi nitie neno kwenye jambo lolote wanalotaka kufanya maana neno langu haliangukii chini
Na Mimi nitamkie mema/baraka niione hio neema uliyopewa
 
Sijawahi ona kiumbe Cha ajabu wala kuhisi sijui minyato ya kichawi au uchawi hapana kabisa!.. hii inanifanya hata niwe mgumu kuuamini huo ulimwengu! Japo nimekuwa muda mwengine mzururaji sometimes maeneo hatarishi ambayo wengine huogopa lkn binafsi hakuna la ajabu nililoliona!.. yanayonitokea ni matukio ya kawaida kabisa ila Kuna baadhi yanaleta utata ila sio utata wenye kunifanya niamini kuwa kuna walakini!!

Mfano kuna mahali palikuwa panasemekana kuwa huwa kuna sijui majini ama mizimu ila kuna miti ya miembe na mapera,siku moja nipo mi najamaa fulani ktk pitapita tukakuta mti wa mpera tukaanza kuchuma lkn sio kwa kupanda punde tukiwa tunachuma aliongezeka kijana mwengine Sasa utata baada ya kuondoka Yule kijana ndo tukaanza kujiuliza alitokea wapi!!

Maana kipindi anakuja hatukumuona! Si tulishangaa tu tupo watatu nae anachuma mapera lkn chengine alichotutatanisha ni ni maswali yake juu ya ule mpera na hata sikumbuki Kama alichuma hata!!

Swala la kutokumuona alivyokuja nililivunjilia mbali maana kibarabara tulikuwa bize kutafuta mapera wahuni😂
Na apotelea pote huko tukio lake halina mantiki..
Sijui nini kitakuja nifanya niamini haya mambo ila mi nachohisi kitu usipokiweka bayana nawe kukuzingua au kujionyesha mbele yako kina nafasi ndogo Sana ya kujionyesha..

Na mnaona hayo mambo na muone siku nikishuhudia huo ulozi kwa sababu ya kimantiki iliyoshiba nitakuja kusimulia humu.
Basi wewe ndo mchawi mwenyewe
 
Back
Top Bottom