Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Nilipogundua waganga na wachawi ni wana tu.

Baada ya kupata kibarua cha kwanza na mshahara kuwa mdogo sana nilikuja kukaa dar kwa ndugu yangu .

Basi majombii yalikua yanamchezesha balaa. Mara kunyolewa, mara kupigwa chale yan ili mradi vurugu tu.

Akasema kuna mganga anafahamiana nae hivyo hana hata malipo ikabid twende akatupige kijikinga. Sikua na namna kwa kuwa naishi hapo tukaenenda mitaa ya vingunguti huko.

Phase1; Kufika bhana mida ya saa moja jioni, tukapewa madawa yamewekwa kwa maji kila mtu akaenda kuoga tukaambiwe tukalale , tutaanza kuroga mida ambayp wachawi wanatoka.

Phase; mida ya saa 7 usiku nikaamshwa. Nikawekwa kwenye kistuli, nakuta mganga kapandisha majini anafoka foka tu. Daaah.
Nikaambiwa nigeukie Kibla (nanukuu , hili lisihusishwe na dini tafadhali) nikawa sielwi elewi nikaelekezwa chap.

Gongwa chale kadha wa kadha na midawa inawashaaa. Fala yule sijui alitupaka pilipili.

Zoezi likafanyika kwa wote.

Phase3 : kuingia ndani kwenda malizia tulale sasa, ukaanza upepo mmoja sio wa kawaida unaingia ndan ya nyumba. Ikawa juu ya bati kama kuna disco wat wanacheza. Varangat mtindo mmoja.

Yule mganga akatoka na madawa na vifaa vyake nje, piga ndumba sana mpaka hali ile ikapotea.

Akarudi akatuambia ni hao washua wanaotupatiaga kichapo ndio wamekuja kumuomba kuwa wanegotiate atupe kidawa uchwara alafu baada ya muda waendele kutupa mbata kama kawa na wamemuahidi pesa. Ila akadai kawagomea.

Tukamaliza, kesho yake tukarudi home. Hali ikatulia ila baada ya muda wale wachawi sijui walireceive Major updates sijui walitumia VPN gani moto ukawa pale pale.
😂 😂 😂
 
Jamaa alisema kwenye kona ya nyumba kwa nje. Hiyo stuli na jiwe(silaha) nilijiongeza sababu jamaa oale juu anasema walipigwa ganzi,nikaona kama ikianza vita basi niwe tayari.Ila angekuja huyo mama tungemalizana kidiplomasia😄😅.Jamaa hakueleza ni mida gani ya kukaa katika kona tatizo...
😹😹😹😹😹😹😹
 
Naomba nimuite ndugu Mshana Jr aweke neno. Haya mambo yapo kwa kuusema usemi, "lisemwalo lipo,kama halipo, litatokea."

Binafsi sijawahi shuhudia chochote kwa macho yangu ya nyama zaidi ya haya...

Wakati flani nilikaa maeneo ya bonde la mpunga, hapo wakazi wake wengi ni waswahili na mie maisha yangu ilikuwa kwenda kazini kurudi najifungia ndani.

Usiku mmoja nimelala chumbani kwangu nikastuka naona taswira kama ya kibibi kinaingia dirishani kwangu kwa njia za kimiujiza huku anapiga kelele. Nikaanza kusema kwa jina la Yesu tokaa (nililelewa kwenye familia za kilokole) kikapotea nikarudi kulala.

Siku ingine nimelala nastuka kabisa nasikia mtu amevuta nywele zangu za utosini kwa kuzikata na kucha ya kidole chake na baada ya hapo akatoweka sikuona mtu ila hali ya nywele kutoka kwenye utosi wangu niliisikia kabisa japo sikusikia maumivu na hapakubaki kipara nilikuwa na nywele ndefu.

Mara nyingine inanitokea usingizini napambana na nguvu za giza usingizini maana ya kwamba kama mashetani au kitu kinanikaba. Kisha sauti inaniambia kemea, sali nikianza kusali napata nguvu na kile kitu kinakimbia, baadae kinarudi tena nakemea naongeza nguvu nazidi kukemea halafu najiona nguvu za maombi zinaniongezeka ghafla nastuka kutoka usingizini najikuta naendelea kusali na inaweza kuchukua hata nusu saa nzima kama si lisaa ndo maombi yanakata, nikijaribu kuacha kusali nashindwa nakuwa sina utashi wa kunyamaza hadi hali ya kusali iishe..

Huwa najiuliza kama ni ndoto nilipostuka ilitakiwa ikate, sasa nastuka bado najikuta naendeleza kusali kwa kukemea, safari moja hadi nikainuka kitandani out of my will nikiwa nasali.

Sijajua kama hayo nayo ni matukio ya kutisha au vimbwanga ama laah...

Nachojua, ulimwengu wa roho upo na unapande mbili, nuru na giza. Si mtu wa dini sana ila...lisemwalo lipo kama halipo litatokea.

Si muamini wa mambo ya kishirikina na yafananayo ila kwa dini yangu ya kikristo niliyokulia natambua ulimwengu wa giza unamazagazaga kama hayo waliyoelezea memba wengine halo juu.
Nakubaliana nawe chief

Binafsi katika ukuaji wangu nmekua katika kumjua Mungu,hivyo nakuwa na nmekuwa na hofu ya Mungu na mara zote nakuwa najitahid kujichunga,but maisha tena unajua baada ya kukua na utafutaji tunakingiuka

Nakumbuka miaka ya 13 hv na kuendelea nami nlikuwa hvyo,mfano unakuta kila ikifika saa9 usik kamil naanza kusali huku ndani ya nafs yangu napata msukumo sana wa kusali huku nazifeel negative energies,hapo nakuwa na sali sana hadi nalia huko usingizini,yaan nasali kama mtu kasimama juu ya kilima anatazama bondeni lengo sauti isikike basi hapo.
Hapo ndio ntaanza kuhisi kabisa zile negative energies zinatoweka halafu nami ndio naamka huku natota jasho ijapokuwa njombe ni baridi

Kwakweli namuomba Mungu anipe nguvu nirudi ktk himaya yake maana dah
 
Nakumbuka kipindi nmemaliza tu kidato cha nne hapo 2008 basi hamu ya kujitafutia pesa na kujinunulia vitu ilininia kwa nguvu sana,basi kufika 2009 mwanzoni kuna mama mmoja rafiki wa mamaetu mdogo pale nyumbani mamdogo akampasha habari kuwa kijana wake nahitaj shughul ya kunipa pesa ndgndg hvyo kama anajua mahala anisaidie.Ikawa hvyo kweli akanielekeza sehem amabyo yy alikuwa katoka siku si nyingi tokea wakat ule,Basi yakafanyika maandalizi ya unga visufuria viwil nkapewa ili nkajitafutie rizik .

Basi nkapewa maelekezo namna ya kufika kule,hehehe niseme tu ukwel,maelekezo nliyopewa na kuyanukuu kwny karatasi yangu yalikuwa simple sana hadi nikawa najiamini.

Safarr ikaanza nkasafiri tokea mji wangu nyumban hadi mafinga,nkafika kama saa 3hv,nkatafuta bas linakwenda mahali kunaitwa mdaburo kama nlivopewa maelekezo nkalipata nkakata tiket saa5 nkaambiwa gari itaondoka.

Basi wakati nasubir muda wa kuondoka gari sjui kwakweli jins ulimwengu unavofanya kazi nkakuta macho yangu yanagonganagongana na ya msichana fulani alikuwa na babu yake pemben yangu,basi nkajikuta napata nguvu za ajabu kumzoea yule msichana pamoja na babu yake,mambo yakawa kama msemo wa YAJAYO YANAFURAHISHA.

Safar ikaanza fresh tukapita donbosco kuelekea kusini mashariki.Njiani nikawa namdadisi umbali wa ile safar na taswira ya maeneo yahuko kwakuwa nlikuwa nshamwambia kuwa mi ni mgeni.Akaniuliza nina ndg huko na nnaenda kufanya nn basi akanishangaa sana na kuanza kuniangalia juu hadi chini[emoji3064][emoji3064][emoji3064],nkapata mfadhaiko kidogo baada ya kumjibu nachofata huko maana ni kama alinionea huruma ni kama sikupewa taarifa kutosha.

Yule rafikiake mamaetu mdg aliniambia kule kuna shughuli nzur za kunipatia pesa daily so kama unalengo na kiasi fulan cha pesa basi mahala kama pale ni rahis maana kwa wiki unaweza make hata 90elf hapo kwanini hustle virgin kama mimi nisijitupe huko?[emoji6][emoji6]so nkawa convinced ndio kuifunga hiyo safar sasa.Shughuli yenyew ilikuwa ni kusomba mbao na unalipwa kwa kila ubao.so nkaona opportunity mwnzenu.

Safar ilikuwa freshi basi maana nlishamuambia nachofata huko akaahid atanikabidhi kwa wana ambao huwa wanakuwa kwny kilabu cha pombe za kienyeji wanapata 'vyombo' kwa maana eneo ambalo zile shughuli za kubeba mbao ni sehemu nyngne tofaut na pana umbali sana.Kwakwel kwa jins yule rafikiake mamdg alivonielekeza kifikra tu ni kama masaa ma3 yalioptia ningekuwa ndio nilifika ila uhalisia ni kulikuwa mbali sana,pia mbali kutoka kwny makazi ya watu.

Basi tulipofika pale kilabuni wana walikuwa washasepa na hapakuwa na mtu anavuka kwenda kule porini.Hvyo yule babu akasema itabid nkalale na ikaamuliwa nkalale kwao tule sista.Tukaenda tukapokelewa na anko wake pamoja na wadogo zake maana yeye alikuwa katoka Dar na ndio alikuwa karudi nyumbani sasa.Kufika kapokelewa kwa furaha na wakadhani labda mi ni mumewe lakn akawanbia hali ilivyokuwa,bas nakalala hadi asbh.

Asubuh yake akaja bro mmoja 'bishoo wa kijiji' unaweza kusema akajitambulisha na akanitambulisha jamaa zake.Basi yule sista akaniambia kama ntona nmeshndw kulala kule pori basi nirud nilale pale hadi ntakapokuwa mwnyj kdg.Basi safar ikaanza kuelekea huko zinakopasuliwa mbao maana ule ni msitu wa serikali na ni mkubwa mno,watunwalikuwa wamepewa vibar ndio wanapasua hzo mbao na hvyo sisi ndio vibarua wnyw.Tulitembea kama saa 1 na kidg tukafika huko.

Maana yule rafiake mamdg aliniambia nikifika huko site nimtafute mama msabato ndio atanikabidh kibanda alichokuwa anakitumia yy kbl hajaondoka,nkaonyeshwa kibanda chenyewe 'Mungu wangu' ilinilipuka kimoyomoyo.Kibanda kilikuwa hakijaezekwa na wala hakinawahi kuezekwa na majani yameota kwa kifup hali ilikatisha sana tamaa.Dah yule mama akaniangalia toka juu hadi chini huku anasubiri kuona nasemaje,basi nkamshukuru nkaondoka zangu na kutafuta sehemu nianze kujichanganya kwa maana wale jamaa nliokuwa nao wao walikuwa wana mambo yao mengine huko nisikokufahamu.

Nkajitoa nkajisogeza maeneo fulani kuna vijana rika langu walikuwa hapo,nkawa nasikiliza stori zao na kujua nini kinaendelea,kwakweli nkaja kujua kuwa hakuna lelemama maana mzigo ukishakuwa tayar huko porini unagombewa watu wanabeba hadi mbao 6 za futi 12 kwa maramoja.Muda mchana nkaenda kwa tule mama msabato maana alikuwa anamgahawa,nkapata chakula nakbakiwa na 1000.Hapo ndio nkashtuka maana inabid nipate mishe ili nipate hela la sivyo ntakufa njaa.Bahati akaja jamaa fulan rika langu pia anaonekana alikuwa anamfanyia kazi mume wake mama msabato,tuseme msabato mwenyewe.Tukapiga story ikajakuwa kumbe maeneo nliyosoma shule na ndio alikuwa anakaa yy na baadhi ya marafik zangu aliwajua,basi nkajisikia faraja sana.Akaniuliza kama nina shughul kwa mda huo,nkamkijib sina hapo tukatoka na kwenda porini huko alikokuwa anafanya kazi yy.Tulipiga kazi siku 2 mfulilizo chakula tunakula bure kwa mama msabato baadae tukawa tunadai pesa lakin ikaonekana ni mpk msabato arud maana hakuwepo.Kazi ikawa ngumu,ila nikazidi kuambatana na huyu jamaangu maana yy ndio mwnyeji zaidi.Basi tukawa tunaamka saa 10 usik tunasomba mbao toka bonden huko nako kunakuwa na vilimavilima pamoja na majimaji na tope pamoja na uterezi.Wakati siku za mwanzoni nakumbuka nlibanwa na haja nikamuuliza jamaa yangu oya choo wapi,jamaa akanionyesha pori fulani na kunakanjia hafifu kanaelekea huko,kukafuata nikitumain kuona choo cha miti.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].daaah nafika nakuta eneo kama mduara katikat nyasi zimelala na kuna haja kubwa nyiiingi kwamba watu huja eneo hili na kunisaidia na baadae akija tena anazilaza nyas kuelea nje anajisadia tena isipokuwa tu ile inaonekana haikuwa shughul ya mtu mmoja.Mzee nikaghairi nkarud zangu na mzigo wangu mpk kuna sehem niliona choo wanatumia mabosi maana pana kabar kakizushi ka mabanzi nkazama huko.

Hapo ndio nkaona wana wanabeba mbao 6 futi 12 mbichi na anaharakisha kiulaini kama anacheza.Jomba mimi mbao 3 tu zinanitoa jasho,shingo inauma,mgongo unauma pumzi juujuu jumlisha na njaa ongeza na hofu ya kufia ugenn.Mzee nlikwenda hvohvo wakat mwngne nasomba mbao nusu safar idadi nayotaka then baadae nazisomba polepole lasivyo wana wanazibeba na huambulii chochote zaid ya hela ya kulansiku hyo.Basi nikaendelea namna ile kwa siku na make 5000 au 3000 mpk tena jion au usiku.Kwakwel maisha ya kule ni kama machimbo tu chakula kilikuwa ghrama halafu kichache,nlivotoka nyumbani nlikuwa nakula kirembo kufikia ndani ya ile wiki mzee mzima nakula kinoma.
So hyo 3000 au 5000 ilikuwa inakidhi mahitaji ya siku tu so kuweka akiba ikawa ni mswada ambao ilibid nifikirie upya.So kwakifupi hakuna fedha ilikuwa inatunzika either nishnde njaa.

Kabla sijaanza kulala na mimi kule mwituni nilikuwa narud kulala kule kijijin kwao yule dada kama mara mbili hv na asubuh na damka zangu kuja chimbo so yule rafikiangu ndio akaniambia tuwe tunalala ili tuotee dili za uski maana kuna jamaa walikuwa wanatokea Chita huko morogoro wanakuja pale wanapiga kazi kinyama ndio hao wanaobeba mbao 6 futi 12[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

SIKU NILIYOKUTANA NA MAAJABU YENYEWE SASA HUENDA HATA NISINGEKUWEPO LEO.(Mungu ni Mtetezi wangu)

Katika hizo mara 2 nlizokuwa narudi kule kijiji kuna njia tulitoipita mara pili baada ya kuja na wale wana 'bishoo wa kijiji'.Njia hii nlipitishwa na ndg mwngne wa yule sista kule kijijini maana wale jamaa wanipitisha pkrini tu siku ile hadi tunafika.So safar ya pili ndio nkapita hii njia mpya hvyo namimi nikawa naitumia wakati wa kurup kule kijijini kwa yule sista mwnenyeji wangu.

Siku hyo nimetoka kupiga kazi mida ya saa 11 na nusu inaelekea saa12 nkamuaga rafikiangu baada ya kula wote matunda fulani ya mwitu tunayaita mapasheni yanaganda gumu na huota kwa kutambaa kama mboga maboga.Nikavuka mto kama kawaida nkaanza kukwea kilima kidogo hapo kuna tambalale na kuna shamba kubwa la mahindi.Na njia inapita katikati ya hilo shamba.Wacheni tu niseme nguvu mbaya zipo na miili yetu imeumbwa kuzitambua nguvu za namna zote.Nikiwa natembea polepole nakaanza kuhisi nimebeba mzigo mzito sana hadi natamani nijitue nikae chini.Na nahuku nahis kausingizi fulani kananijia kwa mbali.Kwakweli nikujikuta kitu tu kinanionya kukaa chini bali nikimbie kwa nguvu zangu zote,kwakweli ikabid nianze kukimbia uzito ukawa mkubwa sana lakn kichwani ni kama napata taarifa kuwa nikimaliza usawa wa lile shamba ntakuwa salama.Kweli nlijikaza nkakimbia kwanguvu bila kugeuka nyuma huku masiko ni kama hayakua yanasikia vzr.Nkatokea mwisho wa shamba.Kwakwel nikaona ajabu ilikuwa kweli,nkajikuta nipo normal safe na sina tatzo wala hakuna uzito wowote.Nkafika kijijini nikawasimulia anko wa yule dada na dada mwnyw wakaangaliana wakaniomba radhi kwa kutokuniambia mapema maana lile shamba ni la tule babu alisafir nae siku ile tunakuja pale kijijini na babu na le ndio mzee wa kamati ya ufundi.Nkaambiwa kupita kwny lile shamba mwisho ni saa 11 jion.Nkanusurika hvyo.
################
###############

So baada ya hapo mimi nikawa natafuta nauli tsh 11000 tu nirud home,maana kempu unakuta umefight 5000 unakula hyo asubuh 2000 jion 2000 usik tena job ngumu wiki ikakata hakuna hesabu inatunzika.Kwakweli Sikuwa nimesoma kitabu chochote cha maarifa ya kujitambua na kujiendeleza but nikakuta nimefosi situation fulani hadi nkapata 10000.
Siku hyo nimetoka kupiga kazi mfukon nina 5000 ilikuwa mida ya saa5 asbh afya yangu ishazorota tayar naharisha bila maumivu ya tumbo nywele timutimu nmekuwa mweusi kama sjui nini.Wazo likaja inabid siku 2 zijazo niondoke kwa namna yyte ile.Sasa pesa yenyw haitulii inabid nifosi kitu ila sitakiw kumuibia mtu,bali inabid mtu anipe pesa mwnyw hiayar yake.

Kwakweli nkakuta napata ukakamavu ambao sielewi ulitokea wapi,maana nlikuta siogopi mtu na nahitaj nionane na mtu mwenye uwezo wa fedha.Tena wazo langu anipe 10000 tu tena sio kinyonge bali anipe kama inapaswa anipe kwakweli ilikuwa hvyo.

Kwa mbali nilimuona bosi mmoja mmama wa kichaga,anawapa watu maagizo huku nawakaripia hvyohvyo,hapo nkaona yulyule ndio mhusika wangu.Nlifika nkamwangalia huku sisemi kitu ilatu nikoserious,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] yule mama akaanza kuwa mpole huku anasema nilishawaambia wenzio ntawalipa mkimaliza kazi[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] kwakweli nkastajabu ila nkajikuta namwambia MI NAHITAJI HELA SAHIZ mama yule akatoa 10000 akanipa halafu aknipa maagizo nimalize kazi yake.Nliondoka natabasamu jioni hyo nliondoka na rafiki yangu hadi pale kijijin kwa yule sista nkamshukuru nikamuaga nkaondoka tuakenda kulala kijiji kwa yule rafikiangu usiku saa9 nkapanda gari kurudi nyumbani.
Nlifika home nmechoka kiafya nmekonda sielewk ni kama nlikuwa mwtuni.Kila mtu alinishangaa sana.
TUPEANE TAARIFA KAMILI JAMANI SIO TU KURAHISISHA TAARIFA NA KUMUINGIZA MTU KWNY MAJUTO
 
KISA CHA NYUMBA YA KUPANGA ILIYOKUWA NA MAUZAUZA KIPINDI NIKO

Baada ya baba yangu kuachana na mama yangu wa kambo aliwekuwa ananisulubu huku ananifunza maisha tulihama ule mtaa na kuhamia mtaa mwningne mtaa mwa ng'ambo maana unavoka bonde kubwa sana.Kipindi hicho nlikuwa darasa la 6.

Baada ya kuhamia kwny ile nyumba mambo yalikuwa shwari kbs kipindi cha mwanzoni,huku tukikaa mimi na baba tu na wapangaji wnengine vijana wawili wakisabato.Nyumba ilikuwa ya mtindo wa self containing kwamba choo iko ndani na wote tunaitumia pamoja wale wapangaji wa kisabato.Sisi tulikuwa na sebule kubwa chumba changu,cha baba pamoja na jiko wakat wale jamaa upande wao walikuwa na chumba chao jiko na se hall ambayo walikuwa hawaitumii na hata hicho choo kilikuwa upande wa kwao.

Basi baada ya kipindi fulani kupita nadhan itakuwa nlikuwa darasa la saba tayar maana tuliahamia mwishon mwa mwaka,nlianza kuota ndoto za kutisha sana tena sana ukizingania miaka yangu ndio hyo 13 au 14 hv,nlikuwa naota ndoto niko makaburini ambayo yako jirant tu pale mtaani,yaan naota nimevaa mavazi meupe na naona kuku wekundu wanakimbizana pale makaburini mimi hapo nakuwa nasali sana hadi mwanga meupe unatokea then nashtuka nmeloa jasho na nimechoka ni ndoto NAJIAMBIA.

Tuko darasa la saba mwanzoni pale darasan akafariki mwanafunzi mwenzetu tenaaa nlikuwa nakaanaye dawati moja,[emoji3064][emoji3064][emoji3064] yule bwana alikuwa na vipaji vingi sana,ijapokuwa uwezo wa darasani ulikuwa sio mzur sana,jamaa alikuwa anajua kucheza mpira vzr sana,bek mzr foward ndio kabs kipa ndio usiseme,jamaa anaogelea kinoma mchizi zile nyimbo za kongo anacheza hadi unapenda but alikuwa hajui kuchora na alikuwa anapenda kuchora,mimi ndio nlikuwa masta wa michoro.Hvyo nlikuwa namfundisha,jamaa alikuwa artist naturally,sikuwahi kumwambia ila nlikuwa najua.

Basi ikafika siku hyo nko na jmaa zangu wnegne mtaani tunacheza zetu akaja rafikiangu nyumba ya jirani akaniambia bwana kuna mwanafunzi unasoma nae kafariki,akaniambia sifa zake alivyo nikatambua kuwa ni jamaa ninae kaa nae kiti kimoja pale class,but sikuamini sana sabab huyu mtoa taarifa anakuwaga na masikhara sana na siku hyo ilikuwa siku ya pili kabla ya kuanza wiki mpya ndio jamaa kafariki ghafla.
Basi nkaenda kwa jamaa nlikuwa nasoma nae tukakutana na jamaa mwngne wa pale class tukawa watatu,wote hatukwa tunaamin lile taarifa maana mwana alikuwa afya njema kbs,maana hata jamaa mwngne akaanza kutania na kuleta mzaha juu swala lile.

Ikafka siku tunaripot shule baada wikend kuisha,ndio tukajipatia ukwel halis,Wanafunzi wa madarasa mawili ya juu tukaambiwa na mwalim mkuu tutaenda kumuaga mwenzetu lakn hatutaenda kumzika maana atasafirishwa hadi kijijini kwajili ya maziko.Tukafika msbani pale majonzi mengi na vilio tukaingia chumbani alikolazwa marehemu,Mwili umelala pale tumbo limekuwa kubwa na kavaa nguo za shule...dah kiukweli nasema wazi.Mimi uchungu siku ukaniisha nikakuta niko relaxed ni kama jamaa hajafa.Hadi nkashangaa kwann.Mwili ukaandaliwa ukawekwa kwny jeneza tukawa tunapita kuuangalia....[emoji3064][emoji3064][emoji3064] nasema wazi kbs nlipigwa tu butwaa ubongo ulifreeze sikuwa na ufahamu bali nlikuwa lite headed,sikuw na judgement nzur hata kidg sjui kwnnn lakn maan kila nichek kwny kioo cha jeneza mi naona kiza totoro na shada za maua,nkamuuliza mwanafunz wanmbele ya ngu vp umeona? akanijibu ehhh tena uso umevimba sana hadi umegusa kioo[emoji3064][emoji3064][emoji3064] nikiangalia huku najongea mandg sion kitu.Tukamaliza mjongeo tukaenda kusimama pembeni ila kichwani mawazo na fikra nying zinanijia.Kitu gan kimefanya nisimuone yule ndg pale kwny jeneza?Sikupata jibu maana tukaambiwa sasa turudi majumbani tukapumzike na tulipoti shule baada ya siku 3

Tukarudi majumbani but mimi nikiwa troubled sana huku tayar iman kuwa jamaangu kafanyiwa kitendo sicho,nlifika nyumbani na mbua ilinyesha sana siku ile.Mimi nkaamua nkalale maana nlikuwa nmechoka sana.

NDOTONI

Nikiwa nmelala nikaanza kuota lakn kuota kwnyw sio kwa kawaida ni kama niko active awake kbs,nkaona niko makaburini kule jamaa anazikwa,ilikuwa ni kwny kilima kias,watu wamezunguka kaburi huku mvua inanyesha,na kwakwel nikamuona marehemu nae ananiangalia mimi,ana huzuni mpweke.Kuna mtu nyuma yake kama kawaida nashuhudia mazishi.Sikumtambua mtu yyte pale makburini ila niliamka nimeloa jasho huku nahema ovyo...Nikanyamaza maana hata wa kumuambia sielewi.

Siku 3 baadae kama kawaida nmelala nkaomuota tena jamaa,safar hii nlikuwa nasikia akiniita jina langu maana sasa nkaona nipo maeneo ya kwao nje ya uwanja kabla hujaingia fensini
Jamaa ananipa directives nimfikie alipo,ananiambia "X njoo uwanjan kabla hujaingia getini kushoto kuna shimo"kweli sikuwa naogopa bali nlikuwa najiskia kama adventure hiv nikafika pale kweli kuna shimo toka nlipo kama mita tano.Lakn lilikushimo dogo mithili ya mdomo wa chungu cha mboga lilikuwa rough sana vipande vya vyungu vilivovunjika na majivu.Ajabu kila nikisogea panakuwa pakubwa baadae likawa pango kbs,nkaingia nkajikuta nipo kwny shimo limekaa kama chungu ndan halafu kuna uwazi kuelekea upande mwngne ambao ndio sasa nlikuwa namsikia jamaa ananiambia "x jifiche bibi anakuja asikuone".Ndg sielew ilikuwaje bali mimo nlikuwa kamtu kadg sana bibi yake sikumuona sura bali nliona miguu mikubwa imevaa ndala inashuka kutoka nje huku mimi nikiwa chini kushoto pembeni ya tuta miguu inamopita....masalaaleeee nliamka ktk njozii hii jasho kama kawaida.

Jamaa baada ya hapo alikuwa anajia ndotoni haongei tena bali ananitazama sana,hapo nlianza kujisikia vibaya sana na guilty ni kama sikumsaidia jamaangu,aliendelea kunitokea but haongei na alikuwa na huzuni sana,mara ya mwisho kumuota ilibid ndio nimwambie "J mbona ulushakufa wewe?"alicheka sana baadae alipotea.Ikawa mwisho.

ILE NYUMBA YA KUPANGA NAYO SASA

Mara zote nlipokuwa natoka shule baada ya kujipikia chakula basi nalala usngz,baadae naamka naweka mabo sawa jikoni then nafanya kazi huko nje.
Sasa ilikuwa ikifika usiku tu hali inakuwa sio nzr baba anakabwa mpk namsikia ananiita inabid niende nikamuamshe,then anasema ni wachawi,sasa kipind baba anapokuwa ananiita ndani kwake nasikia saut ya kama ukizama ndani ya maji ile saut inayosikia ndio nakuwa naisikia,bas mzee nae akakubal kuwa panashida.Uski watoto wanalia darini mara bundi kwnye kamba uwanjani na kila kitu ilimradi vitimbi.Sasa wakat wote huo wale wapangaji wenzetu hatujawah kudiscuss nao hali inayoendelea pale ndan bali kila tu anapigana vita yake,wale jamaa walikuwa wanaamka usik wanapiga maombia ya kutosha.so pale ndan hapakuwa clean

Kuna binamu yangu mmoja alikuja kututembelea,yeye ana kama mizimu huwa inamwambia vitu,wakat mwngne anakuwa kama kachanganyikiwa but ndio hali yake kwa kipindi hicho.Huyo binamu hakuwa kufika kabla pale nyumban hapo awal hyo ilikuwa ndio awam ya kwanza.Ikabid mimi nimwachie alale chumbani kwangu na mdg wake na mimi na binam yang mwngne tulale sitting room,ikawa hvyo.

Sasa usiku ule kule jikoni wakawa wanasikika watu wanapiga soga huku wanasikika kbs wanapika na ugali maana sufilia lilikuwa linapiga kelele mtindo wa kutoa vishindo vidogovidogo huku banio la ugal nalo kama linafyatuaka na kupiga kelele,daaah mazee pale ndan hatunaga panya wala nyau.Yule binamu wetu mwenye watu kichwani akaniita kwa sauti kubwa hadi nikashtuka,nikaenda kule room kumsikiliza,akanuliza "Bina,hapa ndan kuna wachawi?"heheheh nkajua tu hilo sio swali bali ananiambia nikamjib ni kweli wachaw wapo na wanasumbua sana...akasema tukalale nae kule ndani basi ikawa hvyo na tayar muda ule ilikuwa mida yenyew ya 9 usik.

Basi tukatandika mito ya makochi pale chumbani tukalala zetu,Mazee ule usiku ulikuwa special sana kwa wachawi sijui how ila tu timbwili lile lilikuwa sio mchezo.Tukalala mimi kama kawaida ni mzee wa njozi, kaanza kuota tena vivid kbs nko hewani juuu na kilichonipeleka sielewi ila tu nlikuwa na elea nyumba naiona toka juu vzr na ajabu naona na kitu ndan kama haina paa.mzee nkaanza kushuka kwaspidi isiyoelezeka,wakat nakaribia nkaona pale sebuleni kuna watu kama waarabu lakin wanabarakashia na kanzu wamenyanyua mikono kama wanataka wanidake huku midomoni wamejaa damu,sisemi uongo na sipata faida yyte kuusema,nlipokuwa nawakaribia tu nkaaamka tena sio kufumbua macho tu bali hadi kuinua kichwa,UCHAWI NA MAJINI VIPO nliona pale mlangoni maana tulilala miguu inaangaliana na mlango tena mlago haukuwa na lango lenyew la kufunga na komeo bali mapazia ya mtumba ndio yaliwekwa,pale mlangon nliona mtu 3seconds vivid kbs kavaa kanzu nyeupeee na barakashia na alikuwa anangozi nyeupe anapotelea kulia koridoni,pazia halikuwa lifunguliwa kama tulivozoea bali pazia lilikuwa linaslide kwny kamba yake,sasa na lile pazia ni mimi ndio nililiweka ila jins ya kulipitisha kwny ile kama ya ilikuwa kazi hvyo kulislaidhisha haikua rahis ukichangia na kuwa ile kama ilikuwa na vifundo.basi pazia lili slife na mtu alipotelea kiupandeupande koridon lakn nikama anaingia ukutani hv.kama vile mlango wa dvd deck unaingia ndani.i was shocked nlipouliza wenzangu kama wameona hakuana hata alieona chchte.
Basi tukalala kukakucha fresh.

KIBWANGA KILICHOTUHAMISHA KABISA NYUMBA.

Siku hyo kama kawa mtabe niko zang form 2nmetoka shuke nmechoka nkapika nkala then nkadose off,mida ya saa 12 hv nkaamka then nkaenda jikoni,niwakumbushen kitu ile nyumba ni ilikuwa imejitenda na ilikuwa na eneo kubwa sana hvyo majirani unawaona kwa majirani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].Basi nko zangu jikoni ambapo mlango wa jiko unatazamana na chumba cha kulala mzee wangu (R.I.P my wisdom and philosopher) hapo kati ndio korido had mlango wa room yangu pamoja na sebulen. Basi mzee nahangaika niwashe mkaa mara nkasikia saut hapo kwny hilo kolodo...nkatulia labda kuku wa mtu kaja ndan.nkasikia tena sauti safari hii nliisikia vzr maana ni kama uchukue kiatu chenye soli ngum halafu uwe unakanyaga sakafu yenye mchanga.duuh nkaona zile sauti zinazid kusonga mbele kuelekea maeneo ya room kwangu na sebule.Sauti zenyew zinapokanyaga zinaachiana sekunde mojamoja...Mzee nlijikaza hata hewa nikawa sivuti vzr nkajongea mpk pale kwny lile pazia langu ambalo yule mtu mwny kanz na baragashia alipotelea nkalishika ilinione kama kaingia room kwangu maaana hakuna mlangonwa kuufunga,Ndg jamaen ile kulishika lilepazia nilipigwa shot yaumeme ambao hata waya wake sijauona.nlitoka mbio mpk nje huko nlikaaa mpk mzee anakuja saa1 usik.Nikamueleza,wiki ile tuliihama ile nyuma.
 
Kuna kisa kingine mkipenda niwasimulie ok
 
Sijawahi ona kiumbe Cha ajabu wala kuhisi sijui minyato ya kichawi au uchawi hapana kabisa!.. hii inanifanya hata niwe mgumu kuuamini huo ulimwengu! Japo nimekuwa muda mwengine mzururaji sometimes maeneo hatarishi ambayo wengine huogopa lkn binafsi hakuna la ajabu nililoliona!.. yanayonitokea ni matukio ya kawaida kabisa ila Kuna baadhi yanaleta utata ila sio utata wenye kunifanya niamini kuwa kuna walakini!!

Mfano kuna mahali palikuwa panasemekana kuwa huwa kuna sijui majini ama mizimu ila kuna miti ya miembe na mapera,siku moja nipo mi najamaa fulani ktk pitapita tukakuta mti wa mpera tukaanza kuchuma lkn sio kwa kupanda punde tukiwa tunachuma aliongezeka kijana mwengine Sasa utata baada ya kuondoka Yule kijana ndo tukaanza kujiuliza alitokea wapi!!
Maana kipindi anakuja hatukumuona! Si tulishangaa tu tupo watatu nae anachuma mapera lkn chengine alichotutatanisha ni ni maswali yake juu ya ule mpera na hata sikumbuki Kama alichuma hata!!
Swala la kutokumuona alivyokuja nililivunjilia mbali maana kibarabara tulikuwa bize kutafuta mapera wahuni[emoji23]
Na apotelea pote huko tukio lake halina mantiki..
Sijui nini kitakuja nifanya niamini haya mambo ila mi nachohisi kitu usipokiweka bayana nawe kukuzingua au kujionyesha mbele yako kina nafasi ndogo Sana ya kujionyesha..

Na mnaona hayo mambo na muone siku nikishuhudia huo ulozi kwa sababu ya kimantiki iliyoshiba nitakuja kusimulia humu.
Duuuh upo kama mimi mkuu..
Sijawahi kuona ushubwada wowote sijui takataka gani hizo kwanz siamini kama vinaweza kujichukulia maamuzi ya kunifanya jambo lolote baya japo naamini vipo.

Natembea usiku mkubwa na sehemu nyingine zinahadithi kama hizo lakin sihisi wala kuona chochote japo kwa mazingira ya kawaida najikuta nipo kwenye mazingira ya kutisha na kuogofya lakini hujing'amua bila woga , hofu wala sijui takataka gani.
Kujiamini kwangu kwote ni kumtanguliza Mungu mbele.
 
Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Na kwa Bahati nzuri akaweka kizuizi kwa kupitia uwezo wake wa kiungu hili tusiweze kushuhudia viumbe hivyo ambavyo havionekani kwa macho yetu ya kibinadamu isipokua kwa utaalamu flani wa mambo ya kiroho.

Viumbe hivyo vikiwemo , Malaika, Majini , Wachawi pamoja na viumbe vingine vya kutisha sana, ikiwemo wanyama wa ajabu wenye ukubwa wenye kutetemesha na kuogofya kwa wanadamu wa kawaida.

Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.”

Danieli 8:3 “Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.”

Danieli 8:5 “Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.”

Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

Wengi tukisoma Habari kama hizi za kuona simba mwenye vichwa vinne na miguu kama ya binadamu, beberu mwenye pembe kumi, nyoka mwenye vichwa saba na wanyama wengine wa kutisha, tunajipa moyo na kusema hiyo ni lugha tu ya biblia/ lugha ya picha hakuna viumbe kama hivyo. Ila ukweli ni kuwa viumbe hivyo vipo na vinaishi kwenye ulimwengu mwingine tofauti na huu wetu unaonekana. Na kuna binadamu wenzetu wameshashuhudia kabisa kwa macho yao.

Tuachane na hayo na turudi kwenye maada yetu ya leo . Tuzungumzie kuhusu mikasa ya kutisha ambayo tumewahi kukutana nayo kwenye ulimwengu huu ambayo kwa namna moja au nyingine vimekuacha midomo wazi na kukufanya uwe traumatized.

Ngoja nianze na mikasa / mambo ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani ambayo mpaka sasa hivi bado najiuliza kama ni viini macho au ni kweli , lakini ukweli unabaki kuwa ni kweli .

1. Jini kuchomoza baharini na kuelea hewani.

Nakumbuka ilikua ni usiku wa manane, nikiwa kwenye harakati za ushikirikina Uko sehem( sipendi kutaja jina). Nikiwa na mganga akiendelea kufanya mambo ya kishirikina baharini, Ambapo alisema anaita kiumbe( jini) hili anitimizie haja zangu . Kwa akili yangu nilijua tu ni danganya toto, hakuna lolote. Baada ya kama dakika 45 za yule mganga kufanya ushirikina wake. Ghafla akatokea mwanamke mrefu tofauti na urefu wetu wa kawaida wa binadamu alikua baharini anaelea tu, miguu haionekani kwa kweli nilikimbia, Bahati nzuri wale wasaidizi wa mganga wakanikamata kunizuia nisikimbie. Uzuri hakua anatisha wala nini, alikua tu ni mwanamke wa kawaida ingawa alikua na urefu usio na kawaida, na alikua kakasirika sana, alikua analalamika tunamuita sana tuna shida gani.....

2. Niliwahi kushuhudia kwa macho yangu , binadamu akiwa nusu mtu , nusu simba, Ana sura ya kutisha sana , mbaya mfano hakuna, ilibaki kidogo tu nizimie.

3. Binadamu mfupi kama stuli, Ana ndevu nyingi mpaka chini na alikua na mguu mmoja tu , na macho yake yanawaka moto.

4. Mzimu wa mtu maarufu ambaye alikufa miaka mingi iliyopita.

Hii ndo mikasa ya kutisha niliyowahi kukutana nayo hapa duniani, ambayo kiukweli mpaka leo inanipa shida sana, na ilichukua miaka kadhaa mpaka kuweza kukubali hii hali mpaka kufikia kuzoea kidogo. Ila hapa duniani kuna viumbe vya ajabu mno, na kama ukitaka kuviona unaweza.

View attachment 1430585

Sent from my iPhone using JamiiForums
Tupe uzi kiongoz mzmu wa mtu gan ilikuwaje kuwaje n uyo simba
 
Niliachana na private school, nilipata ajira ya serikali mikoa ya nyanda za juu kusini. Japo napenda sana zile moments za beach, upepo mwanana na kutizama vyombo vya wavuvi baharini na vitoweo Kama ngisi, pweza, kamba, kolekole, kibua, changu na kumbwa ndo basi tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Millenium beach hpo napajua kwa mbele kun makonde beach club skuiz police mess pia nyinyi mlimuw mnaish ple ndanda ndog hosptal n masista suvyo?
 
sitasahau Shulen Tanga kuna jamaa alikurupuka kitandan bukta iko magotin usiku akatoka mbio had nje huku anatukana.. tulijua kapandisha mashetan.. kutoka nje tunamkuta ameshika fimbo anatukana kumuuliza akasema kuwa kuna binti mwanafunzi alikuwq anambaka.. na amemfanyia hivyo mara mbili..

sasa alikuwa amemtime amdake sema binti kamchomoka.. tukajiuliza mbona hatujaona mtu aliekuwa anamkimbiza akasema alikuja kichawi.. watu wakabisha akasema kweli ninusen kuna msela akanusa akasema dah kweli unanuka ****
na jamaa dushe lilikuwa limesimama..

masela kuona hivyo eti wengine wakawa usiku wanavua bukta wamelala uchi wanamuomba mariam aje awabake.. dem alikuwa anaitwa mariam eti hawatambishia watatoa ushirikiano

kisa cha pili siku hiyo tunatoka kuangalia mpira UEFA kijijini.. tulikuwa na kaka mkuu pamoja na Patron ambaye alikuwa mshakaj tu.. sasa tunakatiza mabwen ya wavulana ambayo yako
umbali wa kiwanja cha mpira kutoka majengo mengine ya shule ikiwemo bwen la
wasichana tukaona mtu kachutama kimuibukia kumbe binti wa pale shule alikuwa anawanga ndo ameweka ungo chini anajiandaa kuanza ushirikina sijui alikuwa anaenda wapi.. basi Patron kuona hivyo akachagua masela watatu akasema mpelekea mabwen ya wasichana muwambie walinzi wamuamshe matron ili mumkabidhi matron kesho tutalizingumzia na matron

Asubuh Patron anaenda kwa matron Kumuuliza ishu ya jana usiku matron anashangaa hana taarifa.. Ikabidi Patron awaite masela aliowakabidhi binti kuwauliza kulikon wakasema wakati wanamrudisha aliwaloga wakamsamehe

kumbe masela wameona binti yuko
uchi kaumbika wakamwambia awape mzigo wamwachie dem akawapa mzigo wakapiga mtungo wakamwachia

na ikawa kila siku usiku wanavizia maeneo yale eti wakamate mabinti wachawi wawale
mtungo

maisha ya boarding school shule tosha ilitakiwa tupewe vyeti nje ya vyeti vya taaluma..
 
Back
Top Bottom