Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Ilikuwa mwaka 2004 Mzee wetu alihamishiwa kikazi mkoa fulani kanda ya ziwa, ikabidi familia yote tuhamie huko..
Kutokana na uchache wa nyumba za serikali akapangisha nyumba mtaani.

Mzee akapata safari ya kikazi kwa muda, Maza nae akawa chuo mkoa mwingine.. Nikabakia mimi na brother.
Mambo yakaanza, siku ya kwanza tukasikia madirisha ya nyumba yanafunguliwa na upepo mkali unaingia ndani ilikuwa saa nne usiku, tukatoka na mapanga kutafuta mwizi hakuonekana.

Siku ya pili mlango ukafunguliwa na kiumbe kilichoingia kikawa kinafanya shughuli zote tunazofanya mchana mf. Kuwasha radio na kubadili station, kufagia, kufungua fridge nk.

Tulihangaika ikawa kila siku mziki unanza saa mbili usiku, tukawa hatulali.. Akaja mshikaji wake broo akamwambia tukae nje usiku kwenye pembe ya nyumba tutawaona wanaotusumbua.

Tukajipanga tukaenda kukaa, baada kama ya dakika arobani alipita mtu wa kwanza anakimbia kinyume nyume mwendo wake sijapata kuona, baada ya muda akarudi akiwa na mwenzake wakiwa na mwendo wa kawaida tukawatambua kumbe ni baba mwenye nyumba na jirani yetu.

Jambo la kutisha waliamua kutuadhibu baada ya kutugundua tumewaona.. Hivyo tulipigwa ganzi karibia masaa matatu hamna kusogea wala kuongea hata kujikuna. Wao wakaendelea na mambo yao.
chai ya maziwa
 
Ilikua mwaka 2004 nikiwa darasa la 5 mkoani Dodoma mitaa ya mailimbili almaarufu kwa Mwarabu.

Tulikua na nyumba kubwa tu ya vyumba kama 10 na frem tatu ambazo tulipangisha vyota tukabaki na vyumba 2 na seble tukivitumia kama familia. Kulia chumba cha wazee, katikati seble na kushoto chumba chetu ambacho kwa wakati huo tulikua tunalala watu 6, Mimi na broo kitanda cha kulia, madogo wawili kitanda cha pili na chini ya mlango wa kutokea sebleni kulikua na madada wawili wanalaza godoro chini na wanalala hapo.

Ilikua tumeshazoea shoo za ucku za kuckia watu wanatembea juu ya bati mpaka tukawa tunaona kawaida tu plus mandoto yasioeleweka pamoja na mauzauza mengi yaliyokua yakimtokea mama ndani kwake, lakini akawa hatusimulii coz alihofia kututisha na vle tulikua bado wadogo, so alimezea tu.

Kimbembe kilianza saa 8 za ucku broo aliamka akaniamsha nimsindikize chooni (choo kilikua nje) akakojoe. Nikaangalia saa yangu (nlikua nalala nayo) nikakuta ni saa nane na dkk kadhaa iv. Nikakataa kumsindikizs kwa uoga tu na vile nlikua nikiamini mida ya wachawi ni kuanzi saa 7 hadi 11. Nikamwambia mida hii siwezi kutoka akanambia poa na ww kuna cku utabanwa afu utaona.

Basi akafungua chandarua akatoka nje ya kitanda wakati huo me nmelala upande ukutani. Akawa kama anapiga push up iv baina ya vitanda viwili. Katika hali isiyo ya kawaida watu wote mle ndani tukajikuta tupo macho na stori zikaanza ucku ule huku broo bado akiwa nje ya kitanda.

Tulipiga story nyingi ucku ule mpaka mmoja wa wale wanawake akasema jamani tulaleni ucku tunapigia watu kelele. Tukakubali wazo la kulala ( broo bado yuko nje ya chandarua).

Yule binti alosema tulale wakati anajifunika vzur ili alale akageuka upande wa pili ndo tuamsikia akisema kumbwambia mwenzie "Fatuma muone huyu mtu kalala hapa". Kalikua na kamtu fulani kafupi kamelala pembeni yao lkn kwa nje ya chandarua. Ndipo Fatuma alipotazama akakiona na chenyew baada ya kuonekana kikainua pale kikawa kinakuja upande wetu mm na broo. Broo alipokiona alipanda kitandani katika spidi ambayo sikuielewa kwa kwel. Ndani ya sekunde chache tu alifungua chandarua akapenda kitandani akanitoa upande wa ukutani akaniweka mwanzo wa kitanda. Na hapo ndipo kelele za kumwita mama zilipoanza ( Baba alikua mpwapwa kikazi).

Tulipiga kelele za kuita mama huku mmoja katika wale mabinti akikitukana kile kimtu matuc heavy. Kikawa kinaendelea kuja upande wetu huku kimetunyooshea mikono kama style ile mazombi wanafanya. Wakati tunaendelea kupiga kelele nikackia kama mama anafungua mlango kuja ndani kwetu. Kile kimtu kilikuja mpaka pembeni yangu kabla ya kugusa kitanda kikapotea na hapo hapo mama akafika ndani kuangalia kuna nin.

Kwa kweli tulikua tunatetemeka na hakuna hata mmoja aliyeweza kumueleza mama kilichotokea. Basi mama akatubembeleza pale tulale kwa hakuna tena tatizo tukawa kama tumemwelewa iv.
Wakat anatoka kurud ndani kwake wote tukaanza kumfwata kwa nyuma hatukutaka kubaki.
Akatumia busara akatuletea redio akaweka kanda ya Quran then akatwambia hapo hakuna mchawianaweza ingia tena. Hapo kdg tukapata nguvu ya kulala.
Siwez kusahau abadan ile cku. Ilipita mwez mzima hatuwez lala bila kuweka casette za Quran

Litabaki tukio kubwa sana la kutisha nlilolishuhudia kwa macho yangu na siwez kilisahau na hasa pale broo alivokuja kujificha yeye kupitia mimi akaniweka mwanzo ili iweje? si nianze kunyongwa mimi au?
Kila nimimuuliza huwaga hanipi majibu ya kueleweka anacheka tu.
 
Nyumba ilikua na mauzauza ile kila mtu mle ndani aliwahi kukutana la lake.

Kuna csta mmoja mpangaji alikua akitoka chooni ucku. Katikati ya nyumba kulikua na mzabibu, basi alivoupita tu hatua mbili pakaripuka moto alikimbia breki ya kwanza kitandani mwake. Alivochungulia pale hakuuona tena ule moto.

Kuna dogo mmoja alitokaga kigoma kuja kusalimia ndugu zake miaka ya 2008 nikiwa form 2 kama sikosei nikaambia nilale nae wakat huo nshakua mkubwa nkapewa chumba changu kuna mpangaji aliondoka. Sasa yule dogo kumbe alikuaga na mashetani ucku akaota kama kuna wachawi wanakuja kunichezea akawatoa nduki kumbe nikweli sio ndoto. Nilikuja kumwamini baada ya kunionesha alikowafikisha ambako ni mbali na nyumbani na ukizingatia alikua mgeni kaingia jana yake jioni.
Basi siku ya pili wakatuma kibwengu cjui ndo msukule aje amtie adabu yule dogo. Ilikua kama mida ya saa nne ivi dogo akanambia naenda chooni , baada ya srkunde kadhaa ivi nackia kishindo kutoka kwenda kuangalia namkuta yule dogo anagaragara chini huku akiunguruma, nikamburuta mpaka chumbani kumuangalia vzur kwenye shavu ana alama tatu za kucha za kukwanguliwa na kiumbe kama paka iv uku anavuja damu.

Tukio jingine hili nikikumbukaga huwa nacheka mwenyew coz nlikua mdogo sasa cjui kama ilikua ni mauzauza au la.
Nilibanwa tumbo ucku ikabidi lazma nitoke nje kwenda chooni. Nlishindwa kuamsha wenzangu coz me nlikuasitakagi kusindikiza wenzangu nikahofia lazma wangekataa tu.

Basi ile nafungua mlango tu hamadi nikaona ungo utatoka juu ya ule mzabibu unaanguka chini ktka style ambayo ilinishangaza kwa kweli. Ungo ukafika chini ukatulia. Kwa kweli nlihisi faeces zikitoka kwenye rectum zikarudi mpaka kwenye illeum kama sio doudenum asee. Nikafunga mlango taratibu nkarudi kulala mpaka asubuh ndo nkaenda chooni.
 
wakuu mie binafsi sijawahi kukutana na kisa kikubwa chakutisha kivile sema kunakimoja ambacho kilitokea ambacho kinanipa maswali mpaka iitwayo leo

ilikuwa ni kipindi flani wazee wangu wanapata huduma ya kiroho ka waumini wengine katika kanisa flani basi wakawa wanapata shuhuda mbalimbali toka kwa wenzao basi nao wakataka nao wapate baraka hizo za Mungu maana hakuna asiyezitaka ukizingatia nao walikuwa na shida zao. Basi wakaendelea kufanya taratibu zao ka kawaida ili wawezepata kibali chao cha kumshuhudia Mungu wao namie nikiwa ka mtu wa kando ka hayo mambo hayaniusu. Wakaendelea kupata maombi na kuhudhuria ibada basi siku moja kiongozi wao wa kiroho akawaahidi kufika nyumbani kwaajili ya kufanya maombi na kuombea nyumba na familia kwa ujumla

Day one alifika mida ya usiku ka mida ya saa mbili, ikiwa mama ndo alikuwepo akanialika namie kuweza kupata baraka na mengine ya kiroho, mchungaji akafanya maombo kiasi pamoja na wasaidizi wake baada ya muda akasema nitakuja sikunyingine kwaajili ya maombi tena. basi akaondoka. na mzazi akaondoka siku iliyofuatia mie ndo nikaachwa kwaajili ya kumpokea kiongozi huyo wa kiroho siku atakayokuja.

Siku iliyofuatia baada ya siku kadhaa ilikuwa ngumu kumpata kiongozi huyo wa kirohoo maana alikuwa anahudumia watu wengi na alikuwa busy na majukumu mengine ya Kanisa, nikafanya jitihada za kuwasiliana nae mara kwa mara basi akaniahidi one day atafika.

Hiyosiku aloyofika akafika salama maana alikuwa anatokea mbali kiasi na alifika mida ya usiku maana alitoka kutoa huduma sehemu nyingine basi akafanya maombi nikiwa nae na baadhi ya watu wengine baada ya hapo akaanza kumwaga maji ya baraka nyumba nzima na vyote vilivyokuwepo nyumbani hasa magari na nyumba zote na vyumba vyote, baada ya hapo akarudi tena akafanya maombi kiasi then akaniambia twende nje.

Tukazunguka kwenye eneo la nje akaanza kutafuta tafuta akaniambia ka naona kitu, nikamjibu sioni akatafuta tena na tena kwakutumia mwanga wa simu basi akaanza kusema 'lilikuwa linataka kukimbia tena na leo' basi akakiona kumbe ilikuwa kibuyu na kichupa vimefungwa pamoja na vinashanga na kitu ka irizi nyeusi na nyekundu, nilistaajabu sana. akanijuza kuwa ilikuwa inataka kukimbia na ndo maana siku ya kwanza alishindwa kuikamata. na hizo zana za kishirikina zilikuwepo sehemu nyeupe ambayo ni rahisi kuviona ila akaniambia vilikuwa ndani ya banda lililokuwepo karibu ila kwakuwa alimwaga maji yaliyobarikiwa kikashindwa kukimbia kikaishia hapo nje na akanijuza kwa macho ya kawaida huwezi ona

Mpaka leo najiuliza sana hivi ule ushirikina ulitoka wapi na uliwekwa pale nyumbani toka lini na unawezaje kukimbia pindi nguvu ya Mungu ijitokezapoooo? Mpaka leo lile tukio huwa nalikumbuka sana na vile kibuyu kilivyousisimua moyo wangu.
kama una hela nicheki PM nikuuzie kitabu kinaitwa CHURCH MAFIA...huwa wanatuma watu wao kuja kuvifukia hivyo vitu..matapeli wachungaji wa mwendokasi hao
 
Nina kawaida ya kuamka kila saa 9 au 10 alfajiri kwa ajili ya kwenda kuchuja. Visa hivi vimenitokea sana wakati huo, ila hiki cha mwisho kimenikaa sana.


Kuna hizi neti zenye zipu, huwa natandika mkeka na kigodoro, nalala, wiki kama mbili zilizopita mida ya saa 9, nimeamka kwenda kukojoa, nikarudi kulala, sasa nikafungua ile neti kwa kuvuta zipu yake juu, kisha nikaifunga nikajilaza, ghafla nikajiona mchovuuuu, halafu nikasikia hatua za mtu anakuja spidii, kuelekea napolala, najaribu kugeuka kumuangalia ni nani nashindwa, kichwa kizito, kilichonishinda nguvu ni pale niliposikia zipu ya neti ikifunguliwa, najitahidi kuamka nigeuze kichwa nashindwa.

Mpaka pale nilipotaja jina YESU kwa sauti xa chini sana, nikafanikiwa kugeuza kichwa na sikuona kitu, amini usiamini, nilikuta zipu imefunguliwa, nikaifunga na kuanza kusali huku moyo ukienda mbio. [emoji2962]
 
MKOA WA RUVUMA 2016

Kuna shule moja nilisoma pale, haya haya mambo ya kushtuka usiku saa tisa/kumi, Siku hiyo tukiwa tumefunga shule, nilishtuka mida kama saa 9 Usiku hivi nikiwa Bwenini, bweni lenye mfumo wa vyumba, nikiwa chumba namba 27, niliamka kwenda kuwasha taa, wakati huo ni siku nyingine baada ya siku tuliyofunga shule, nakumbuka ilikuwa jumamosi.

Kuamka muda huo ilikuwa ni sehemu ya maandalizi ya kurudi nyumbani DSM likizo, kama ujuavyo, Ruvuma kuna baridi, nilichoamua kufanya ni kuwahi moto wa jiko la shule, huwa hawazimi, wanafukia kuni, nikachemshe maji ya kuoga.

Jiko lilikuwa mbali kidogo, ni safari ya takribani mita 200 hivi, wakati huo nimebeba maji, na baadhi ya roommates wangu wakiwa wameshaamka, hiyo ikiwa ni takribani nusu saa tangu niamke na yapata saa kumi hivi, nilibeba ndoo yangu kuelekea jikoni nikajipashie maji, kwa asili mimi si muoga wa usiku, ila siku hiyo, nilianza kuwa

Wakati nipo njiani, kanjia kembamba, kwenye giza lililoangazwa na mwanga hafifu wa mbalamwezi, nikaona kwa mbali watu wawili wakija usawa wangu na masikioni nilisikia sauti zao, sikuwahofia wala kujiuliza ni akina nani, kwa sababu shule yetu haikuwa na bweni moja, bweni lingine lipo baada ya kuvuka jiko, nikajua ni ndugu zetu waislamu wanaenda kusali ALFAJIR, chumba cha ibada kilikuwa bwenini kwetu.

Kadiri navyozidi kwenda naona wanazidi kufifia, mbaya zaidi wakawa kama wamenyamaza kwa sababu ya kuiona labda, lakini nilivyowakaribia sikuweza kuona mtu yeyote, niliogopa sana, kuangalia chini nipo nje ya njia niliyokuwa napita, yaani nimesimama pembezoni kabisaaa ya njia, kwenye mijani, watch this out, nikathubutu kugeuka nyuma (yahitaji ujasili) nikaona watu wale wana endelea na safari yao, as if wanapiga stori hivi, mwangaza uliotoka kwenye taa ya ukumbi wa bweni la shule uliwaangaza, nikaona vijana wawili wakiingia bwenini, wakiwa wamevalia kanzu. Nilishikwa na butwaa, ila cha ajabu, moyo ukawa na ujasiri wa kuendelea na safari yangu, nikafika mpaka jikoni, nikatenga maji, yakapata joto, nikawa narudi, wakati narudi, nikakuta nje ya dirisha la kwanza la bweni letu, kuna bundi amesimama pale akiangalia usawa wangu. Moyoni nikajisema "siogopi" ghafla yule bundi akaruka, nami nikapita mlango ule ule waliopita wale watu niliowaona kwa kuwa ulikuwa ukielekea chumbani kwangu.


Siku nzima safarini nilikuwa nimezubaa tu, mpaka nafika UBUNGO.
 
Kuna siku nikiwa nipo home nje ya mji huko bunju. Nimejiegesha zangu majira ya saa sita za usiku. Umeme ulikatika eneo letu lote la mtaa lilikuwa kiza kinene.

Mapazia ya chumbani yalikuwa wazi basi ile nafunhua jicho nitazame kwa nje kuona kama umeme umekatika kote ama ni kwangu tuu naona mtu amesimama dirishani anatazama ndani haonekani vizuri sababu ya kiza ila unaona mtu kabisa yule pale.

Dah, nyumba nzima nipo pekee yangu ndani ya fensi. Nitafanyaje sasa nikajifunika shuka taratibu kwa minyato nikafumba macho. Baadae nikatazama nikaona hayupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nikiwa nipo home nje ya mji huko bunju. Nimejiegesha zangu majira ya saa sita za usiku. Umeme ulikatika eneo letu lote la mtaa lilikuwa kiza kinene.

Mapazia ya chumbani yalikuwa wazi basi ile nafunhua jicho nitazame kwa nje kuona kama umeme umekatika kote ama ni kwangu tuu naona mtu amesimama dirishani anatazama ndani haonekani vizuri sababu ya kiza ila unaona mtu kabisa yule pale.

Dah, nyumba nzima nipo pekee yangu ndani ya fensi. Nitafanyaje sasa nikajifunika shuka taratibu kwa minyato nikafumba macho. Baadae nikatazama nikaona hayupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watoto wa dar kwenye ubora wenu
 
Mi sijielewagi kabisa
Sijui huwa sioti ndoto isipokua ndoto mbaya za KUTISHA?

Sikumbuki kiwahi kuamka na kukumbuka ndoto nzuri nilio iota
Siku ikitoka nimeota basi itakua nakabiliwa na hatari kubwa na ninakua kama ninusu nimelala na nusu nipo macho

Imefikia hatua sasa ndoto hizo zikinijia najiambiza binafsini nikiwa ndotoni kwamba hii ni ndoto tu na najua nifanueje kuimaliza fasta niamke
 
Mi sijielewagi kabisa
Sijui huwa sioti ndoto isipokua ndoto mbaya za KUTISHA?

Sikumbuki kiwahi kuamka na kukumbuka ndoto nzuri nilio iota
Siku ikitoka nimeota basi itakua nakabiliwa na hatari kubwa na ninakua kama ninusu nimelala na nusu nipo macho

Imefikia hatua sasa ndoto hizo zikinijia najiambiza binafsini nikiwa ndotoni kwamba hii ni ndoto tu na najua nifanueje kuimaliza fasta niamke

Umebarikiwa
 
Katika harakati zangu. Za kutibu "Nafsi" zilzojeruhiwa. Nimeshakutana na viumbe kadha kutoka ulimwengu wa majini. Ni viumbe vya kutisha mno. Na usiombe ukutane no kama ujajipanga kiroho na kimwili utadhurika daima. Kama wengi waliojaribu na wamepotea. Ulimwengu wa majini upo kama ilivyothibitishwa ktk vitabu takatifu. Quraan na Biblia.

Kwa hiyo ikikutokea kwa bahati umekutana uso kwa uso na hawa viumbe. Usikimbie wala usiitetemeke zingatia mafundisho ya imani yako. Na mtaje jina la mwenyezimgu. Jinsi imani yako iliokufunza. Kwa hakika viumbe hao watakuheshimu na wanaweza kupoteza vishawishi vya nguvu ya "Moto" waliokufikia. Kisha mnapiga story utakavyo.

Zingatia kua baadhi ya sifa mbaya ya Viumbe yawa ni kukudanganya na kukupoteza kwa uongo. Kwahiyo elewa kua sio kila jambo unapewa na majini ni sahihi. Mengine tumia ufahamu wa ubinadamu wako....
 
Back
Top Bottom