MKOA WA RUVUMA 2016
Kuna shule moja nilisoma pale, haya haya mambo ya kushtuka usiku saa tisa/kumi, Siku hiyo tukiwa tumefunga shule, nilishtuka mida kama saa 9 Usiku hivi nikiwa Bwenini, bweni lenye mfumo wa vyumba, nikiwa chumba namba 27, niliamka kwenda kuwasha taa, wakati huo ni siku nyingine baada ya siku tuliyofunga shule, nakumbuka ilikuwa jumamosi.
Kuamka muda huo ilikuwa ni sehemu ya maandalizi ya kurudi nyumbani DSM likizo, kama ujuavyo, Ruvuma kuna baridi, nilichoamua kufanya ni kuwahi moto wa jiko la shule, huwa hawazimi, wanafukia kuni, nikachemshe maji ya kuoga.
Jiko lilikuwa mbali kidogo, ni safari ya takribani mita 200 hivi, wakati huo nimebeba maji, na baadhi ya roommates wangu wakiwa wameshaamka, hiyo ikiwa ni takribani nusu saa tangu niamke na yapata saa kumi hivi, nilibeba ndoo yangu kuelekea jikoni nikajipashie maji, kwa asili mimi si muoga wa usiku, ila siku hiyo, nilianza kuwa
Wakati nipo njiani, kanjia kembamba, kwenye giza lililoangazwa na mwanga hafifu wa mbalamwezi, nikaona kwa mbali watu wawili wakija usawa wangu na masikioni nilisikia sauti zao, sikuwahofia wala kujiuliza ni akina nani, kwa sababu shule yetu haikuwa na bweni moja, bweni lingine lipo baada ya kuvuka jiko, nikajua ni ndugu zetu waislamu wanaenda kusali ALFAJIR, chumba cha ibada kilikuwa bwenini kwetu.
Kadiri navyozidi kwenda naona wanazidi kufifia, mbaya zaidi wakawa kama wamenyamaza kwa sababu ya kuiona labda, lakini nilivyowakaribia sikuweza kuona mtu yeyote, niliogopa sana, kuangalia chini nipo nje ya njia niliyokuwa napita, yaani nimesimama pembezoni kabisaaa ya njia, kwenye mijani, watch this out, nikathubutu kugeuka nyuma (yahitaji ujasili) nikaona watu wale wana endelea na safari yao, as if wanapiga stori hivi, mwangaza uliotoka kwenye taa ya ukumbi wa bweni la shule uliwaangaza, nikaona vijana wawili wakiingia bwenini, wakiwa wamevalia kanzu. Nilishikwa na butwaa, ila cha ajabu, moyo ukawa na ujasiri wa kuendelea na safari yangu, nikafika mpaka jikoni, nikatenga maji, yakapata joto, nikawa narudi, wakati narudi, nikakuta nje ya dirisha la kwanza la bweni letu, kuna bundi amesimama pale akiangalia usawa wangu. Moyoni nikajisema "siogopi" ghafla yule bundi akaruka, nami nikapita mlango ule ule waliopita wale watu niliowaona kwa kuwa ulikuwa ukielekea chumbani kwangu.
Siku nzima safarini nilikuwa nimezubaa tu, mpaka nafika UBUNGO.