Acha nami nishee story yangu japo si mzuri sana katka uandishi.
Ilikua 2010 Dar es salam enzi hizo nikiwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapo. Ukweli sikukutana nakiumbe cha kutisha bali ni binaadam alienifanya nibaki na sintofaham na maono tofauti ktk maisha.
Sikubahatika kupata chumba ktk hostel za chuo ikanibidi nipange kitaa flan uswahilini karibu na mwenge hapo. Maisha yalikua fresh tu fadha house alikua na wake wawili na watoto kadhaa hapo kijana mkubwa wa mwenye nyumba alitokea kua mwanangu sana story za hapa na pale, jamaa alikua mstaalabu sana na anasura ya upole by that time alikua kama ana 30 yrs nakuendelea.
Tukio lilotokea lilinifanya nibaki mdomo wazi ni siku moja mida ya saa tisa kasoro huyo bro aliniamsha kwa kugonga mlango nlisita kuitika lkn mwisho nilifunua nakumkuta amemkamata kijana mmoja wa makamo. Jamaa akanambia kwamba huyu ni mwizi na huwa anaibia watu hapo mtaani. Nikamuuliza vp ushahidi unao akadai hana ila amemkuta na kisu mfukoni. Nilitaka kuacha kumpa ushirikiano ila nikaona nimsaidie huyo kijana asijedhurika kwani hakukua na ushahidi wowote. Nilimshauri jamaa kua tuamshe majirani au ndg zake jamaa akawa mbogo. Ilibidi nimfate kwanyuma akiwa amemkamata yule kijana shingoni tukielekea nyumba iliokua opposite na hii tunayokaa. Nilipata bahati ya kumuuliza jamaa akakubali ni kweli hapo aliwahi iba shati na sendoz. Nilijua itakua kesi ndogo lkn tulipofika kwa huyu jirani aligonga mlango mara mbili tatu huyo mzee akafungua na kuelezwa dhumuni la sie kuwepo hapo. Alimtazama yule kijana kwa macho ya dharau na kuulizia mimi kwani hakuwahi niona maeneo hayo ndo jamaa akanitambulisha kama mpangaji wao. Yule mzee haraka bila uoga alitupa jukumu tumuue huyo dogo then tukimaliza tumchome moto hapo hapo. Nilihisi kuogopa nikaona ni kama mzaha vile kwani tulikua wawili tunaopewa jukum hilo. Alipomaliza kufunga mlango wake mzee yule nilimwambia huyu mshkaj kwanini tusimteme tu dogo coz vitu alivyoiba nividogo sana. Msela alinifokea sana na kunipolomoshea matusi makali. Ilibidi niwe mtazamaji asikwambie mtu kifo ni kitu rahisi sana, dogo alishushiwa kipigo hevy ngumi na mateke mpaka akazimia ndipo jamaa alipoanza kutumia mawe yaliyokua pembeni . Ilifika muda dogo alipiga mayowe maskini it was too late, jamaa alihitaji kuua siku hiyo. Baada yakama dakika saba dogo alivuta nikimshuhudia alimsihi yule jamaa akimtaja kwa jina kua unaniua bure bro mimi ni mdogo wako, haikusaidia kitu dogo alipigwa taili mbili na kumwagiwa mafuta ya taa. Aliwaka mpaka mwisho. Niliogopa sana na usiku huo sikulala tena taswira ya kile kipigo ilikua ikinijia kichwani. Niliogopa sababu dogo alouwawa na huyu jamaa ni wa pale mtaani vp mimi mgeni. Nakwanini jamaa hakutaka watu waamshwe na dogo mbona hakua amemuibia huyu jamaa kitu.
Ilibidi iwe siri yangu mpaka nilpokuja kufahamishwa na majirani wengine juu ya kuokotwa mara kwa mara maiti zisizo julikana mtaani. Ilibidi nihame kimya kmya na kujiapiza kua sintokuja kupanga uswahilini tena na hawa binadam wenye sura nzuri za upole niishinao kwa tahadhari kubwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app