Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Nikiwa na umri mdogo kama miaka 15-17 hivi Niliwahi kwenda msibani na shangazi yangu. Kipindi hicho naishi kwake. Tulipofika yeye alielekea kwa wamama (wanawake wenzake) kuendelea na shughuli za jikoni na mambo mengine ya akina mama, mimi nikabaki nje ila maeneo hayo hayo ya msibani.

Nikiwa nimejitenga mbali kidogo na watu alikuja mbaba mmoja sio mkubwa sana na wala sio mzee akakaa nami, alionekana kuhuzunishwa sana na ule msiba. Nilimuamkia akaitika alafu kila mtu akawa kimya.

Baada ya dakika chache akanambia "Kijana, wewe bado mdogo sana. Ukipata nafasi ya kufurahia maisha furahia kadri uwezavyo" nikamwambia "sawa". Wala sikumuelewa ila sikusema neno lengine.

Baada ya muda mwili ukafika na watu wakaanza kuaga, nikasubiri ilivyofika zamu ya watu wengine nami nikaenda kuaga.

Yule mbaba alienambia nifurahie maisha ndo yule alikuwa amelala kwenye jeneza. Oya asikwambie mtu, jasho lilinitoka balaa. Kidogo nianguke mtu wa nyuma yangu akanishika kunisogeza pembeni.

Tulivyorudi nyumbani katika kumuuliza muuliza shangazi akanambia marehemu ana pacha wake na wanafanana balaa. Hata msibani pia alikuwepo. Lakini mbona wakati wa kuaga sikumuona? Mbona aniambie maneno yale?
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]aisee hatari sana
 
Kumbe jina la Yesu lina nguvu Hivi maana wengi wanapokutana na vitimbi vya nguvu za Giza wakilitaja wanapata ushindi.
Ukiwa na imani nalo. Ni zaidi ya balaa.

Kuna jamaa aliwahi kufanya mazingaombwe yake na kujifanya mganga uchwara hiki kibuyu huwezi kukinyanyua nkamwambia Mimi nitakinyanyua kwa jina YESU KRISTO. Sikuwa na shaka moyoni, nikakinyanyua ila wakati nakishika ni kama nilikula shoti ndogo ya umeme.
So ukiliamini unatoboa

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
KISA CHA NYUMBA YA KUPANGA ILIYOKUWA NA MAUZAUZA KIPINDI NIKO

Baada ya baba yangu kuachana na mama yangu wa kambo aliwekuwa ananisulubu huku ananifunza maisha tulihama ule mtaa na kuhamia mtaa mwningne mtaa mwa ng'ambo maana unavoka bonde kubwa sana.Kipindi hicho nlikuwa darasa la 6.

Baada ya kuhamia kwny ile nyumba mambo yalikuwa shwari kbs kipindi cha mwanzoni,huku tukikaa mimi na baba tu na wapangaji wnengine vijana wawili wakisabato.Nyumba ilikuwa ya mtindo wa self containing kwamba choo iko ndani na wote tunaitumia pamoja wale wapangaji wa kisabato.Sisi tulikuwa na sebule kubwa chumba changu,cha baba pamoja na jiko wakat wale jamaa upande wao walikuwa na chumba chao jiko na se hall ambayo walikuwa hawaitumii na hata hicho choo kilikuwa upande wa kwao.

Basi baada ya kipindi fulani kupita nadhan itakuwa nlikuwa darasa la saba tayar maana tuliahamia mwishon mwa mwaka,nlianza kuota ndoto za kutisha sana tena sana ukizingania miaka yangu ndio hyo 13 au 14 hv,nlikuwa naota ndoto niko makaburini ambayo yako jirant tu pale mtaani,yaan naota nimevaa mavazi meupe na naona kuku wekundu wanakimbizana pale makaburini mimi hapo nakuwa nasali sana hadi mwanga meupe unatokea then nashtuka nmeloa jasho na nimechoka ni ndoto NAJIAMBIA.

Tuko darasa la saba mwanzoni pale darasan akafariki mwanafunzi mwenzetu tenaaa nlikuwa nakaanaye dawati moja,[emoji3064][emoji3064][emoji3064] yule bwana alikuwa na vipaji vingi sana,ijapokuwa uwezo wa darasani ulikuwa sio mzur sana,jamaa alikuwa anajua kucheza mpira vzr sana,bek mzr foward ndio kabs kipa ndio usiseme,jamaa anaogelea kinoma mchizi zile nyimbo za kongo anacheza hadi unapenda but alikuwa hajui kuchora na alikuwa anapenda kuchora,mimi ndio nlikuwa masta wa michoro.Hvyo nlikuwa namfundisha,jamaa alikuwa artist naturally,sikuwahi kumwambia ila nlikuwa najua.

Basi ikafika siku hyo nko na jmaa zangu wnegne mtaani tunacheza zetu akaja rafikiangu nyumba ya jirani akaniambia bwana kuna mwanafunzi unasoma nae kafariki,akaniambia sifa zake alivyo nikatambua kuwa ni jamaa ninae kaa nae kiti kimoja pale class,but sikuamini sana sabab huyu mtoa taarifa anakuwaga na masikhara sana na siku hyo ilikuwa siku ya pili kabla ya kuanza wiki mpya ndio jamaa kafariki ghafla.
Basi nkaenda kwa jamaa nlikuwa nasoma nae tukakutana na jamaa mwngne wa pale class tukawa watatu,wote hatukwa tunaamin lile taarifa maana mwana alikuwa afya njema kbs,maana hata jamaa mwngne akaanza kutania na kuleta mzaha juu swala lile.

Ikafka siku tunaripot shule baada wikend kuisha,ndio tukajipatia ukwel halis,Wanafunzi wa madarasa mawili ya juu tukaambiwa na mwalim mkuu tutaenda kumuaga mwenzetu lakn hatutaenda kumzika maana atasafirishwa hadi kijijini kwajili ya maziko.Tukafika msbani pale majonzi mengi na vilio tukaingia chumbani alikolazwa marehemu,Mwili umelala pale tumbo limekuwa kubwa na kavaa nguo za shule...dah kiukweli nasema wazi.Mimi uchungu siku ukaniisha nikakuta niko relaxed ni kama jamaa hajafa.Hadi nkashangaa kwann.Mwili ukaandaliwa ukawekwa kwny jeneza tukawa tunapita kuuangalia....[emoji3064][emoji3064][emoji3064] nasema wazi kbs nlipigwa tu butwaa ubongo ulifreeze sikuwa na ufahamu bali nlikuwa lite headed,sikuw na judgement nzur hata kidg sjui kwnnn lakn maan kila nichek kwny kioo cha jeneza mi naona kiza totoro na shada za maua,nkamuuliza mwanafunz wanmbele ya ngu vp umeona? akanijibu ehhh tena uso umevimba sana hadi umegusa kioo[emoji3064][emoji3064][emoji3064] nikiangalia huku najongea mandg sion kitu.Tukamaliza mjongeo tukaenda kusimama pembeni ila kichwani mawazo na fikra nying zinanijia.Kitu gan kimefanya nisimuone yule ndg pale kwny jeneza?Sikupata jibu maana tukaambiwa sasa turudi majumbani tukapumzike na tulipoti shule baada ya siku 3

Tukarudi majumbani but mimi nikiwa troubled sana huku tayar iman kuwa jamaangu kafanyiwa kitendo sicho,nlifika nyumbani na mbua ilinyesha sana siku ile.Mimi nkaamua nkalale maana nlikuwa nmechoka sana.

NDOTONI

Nikiwa nmelala nikaanza kuota lakn kuota kwnyw sio kwa kawaida ni kama niko active awake kbs,nkaona niko makaburini kule jamaa anazikwa,ilikuwa ni kwny kilima kias,watu wamezunguka kaburi huku mvua inanyesha,na kwakwel nikamuona marehemu nae ananiangalia mimi,ana huzuni mpweke.Kuna mtu nyuma yake kama kawaida nashuhudia mazishi.Sikumtambua mtu yyte pale makburini ila niliamka nimeloa jasho huku nahema ovyo...Nikanyamaza maana hata wa kumuambia sielewi.

Siku 3 baadae kama kawaida nmelala nkaomuota tena jamaa,safar hii nlikuwa nasikia akiniita jina langu maana sasa nkaona nipo maeneo ya kwao nje ya uwanja kabla hujaingia fensini
Jamaa ananipa directives nimfikie alipo,ananiambia "X njoo uwanjan kabla hujaingia getini kushoto kuna shimo"kweli sikuwa naogopa bali nlikuwa najiskia kama adventure hiv nikafika pale kweli kuna shimo toka nlipo kama mita tano.Lakn lilikushimo dogo mithili ya mdomo wa chungu cha mboga lilikuwa rough sana vipande vya vyungu vilivovunjika na majivu.Ajabu kila nikisogea panakuwa pakubwa baadae likawa pango kbs,nkaingia nkajikuta nipo kwny shimo limekaa kama chungu ndan halafu kuna uwazi kuelekea upande mwngne ambao ndio sasa nlikuwa namsikia jamaa ananiambia "x jifiche bibi anakuja asikuone".Ndg sielew ilikuwaje bali mimo nlikuwa kamtu kadg sana bibi yake sikumuona sura bali nliona miguu mikubwa imevaa ndala inashuka kutoka nje huku mimi nikiwa chini kushoto pembeni ya tuta miguu inamopita....masalaaleeee nliamka ktk njozii hii jasho kama kawaida.

Jamaa baada ya hapo alikuwa anajia ndotoni haongei tena bali ananitazama sana,hapo nlianza kujisikia vibaya sana na guilty ni kama sikumsaidia jamaangu,aliendelea kunitokea but haongei na alikuwa na huzuni sana,mara ya mwisho kumuota ilibid ndio nimwambie "J mbona ulushakufa wewe?"alicheka sana baadae alipotea.Ikawa mwisho.

ILE NYUMBA YA KUPANGA NAYO SASA

Mara zote nlipokuwa natoka shule baada ya kujipikia chakula basi nalala usngz,baadae naamka naweka mabo sawa jikoni then nafanya kazi huko nje.
Sasa ilikuwa ikifika usiku tu hali inakuwa sio nzr baba anakabwa mpk namsikia ananiita inabid niende nikamuamshe,then anasema ni wachawi,sasa kipind baba anapokuwa ananiita ndani kwake nasikia saut ya kama ukizama ndani ya maji ile saut inayosikia ndio nakuwa naisikia,bas mzee nae akakubal kuwa panashida.Uski watoto wanalia darini mara bundi kwnye kamba uwanjani na kila kitu ilimradi vitimbi.Sasa wakat wote huo wale wapangaji wenzetu hatujawah kudiscuss nao hali inayoendelea pale ndan bali kila tu anapigana vita yake,wale jamaa walikuwa wanaamka usik wanapiga maombia ya kutosha.so pale ndan hapakuwa clean

Kuna binamu yangu mmoja alikuja kututembelea,yeye ana kama mizimu huwa inamwambia vitu,wakat mwngne anakuwa kama kachanganyikiwa but ndio hali yake kwa kipindi hicho.Huyo binamu hakuwa kufika kabla pale nyumban hapo awal hyo ilikuwa ndio awam ya kwanza.Ikabid mimi nimwachie alale chumbani kwangu na mdg wake na mimi na binam yang mwngne tulale sitting room,ikawa hvyo.

Sasa usiku ule kule jikoni wakawa wanasikika watu wanapiga soga huku wanasikika kbs wanapika na ugali maana sufilia lilikuwa linapiga kelele mtindo wa kutoa vishindo vidogovidogo huku banio la ugal nalo kama linafyatuaka na kupiga kelele,daaah mazee pale ndan hatunaga panya wala nyau.Yule binamu wetu mwenye watu kichwani akaniita kwa sauti kubwa hadi nikashtuka,nikaenda kule room kumsikiliza,akanuliza "Bina,hapa ndan kuna wachawi?"heheheh nkajua tu hilo sio swali bali ananiambia nikamjib ni kweli wachaw wapo na wanasumbua sana...akasema tukalale nae kule ndani basi ikawa hvyo na tayar muda ule ilikuwa mida yenyew ya 9 usik.

Basi tukatandika mito ya makochi pale chumbani tukalala zetu,Mazee ule usiku ulikuwa special sana kwa wachawi sijui how ila tu timbwili lile lilikuwa sio mchezo.Tukalala mimi kama kawaida ni mzee wa njozi, kaanza kuota tena vivid kbs nko hewani juuu na kilichonipeleka sielewi ila tu nlikuwa na elea nyumba naiona toka juu vzr na ajabu naona na kitu ndan kama haina paa.mzee nkaanza kushuka kwaspidi isiyoelezeka,wakat nakaribia nkaona pale sebuleni kuna watu kama waarabu lakin wanabarakashia na kanzu wamenyanyua mikono kama wanataka wanidake huku midomoni wamejaa damu,sisemi uongo na sipata faida yyte kuusema,nlipokuwa nawakaribia tu nkaaamka tena sio kufumbua macho tu bali hadi kuinua kichwa,UCHAWI NA MAJINI VIPO nliona pale mlangoni maana tulilala miguu inaangaliana na mlango tena mlago haukuwa na lango lenyew la kufunga na komeo bali mapazia ya mtumba ndio yaliwekwa,pale mlangon nliona mtu 3seconds vivid kbs kavaa kanzu nyeupeee na barakashia na alikuwa anangozi nyeupe anapotelea kulia koridoni,pazia halikuwa lifunguliwa kama tulivozoea bali pazia lilikuwa linaslide kwny kamba yake,sasa na lile pazia ni mimi ndio nililiweka ila jins ya kulipitisha kwny ile kama ya ilikuwa kazi hvyo kulislaidhisha haikua rahis ukichangia na kuwa ile kama ilikuwa na vifundo.basi pazia lili slife na mtu alipotelea kiupandeupande koridon lakn nikama anaingia ukutani hv.kama vile mlango wa dvd deck unaingia ndani.i was shocked nlipouliza wenzangu kama wameona hakuana hata alieona chchte.
Basi tukalala kukakucha fresh.

KIBWANGA KILICHOTUHAMISHA KABISA NYUMBA.

Siku hyo kama kawa mtabe niko zang form 2nmetoka shuke nmechoka nkapika nkala then nkadose off,mida ya saa 12 hv nkaamka then nkaenda jikoni,niwakumbushen kitu ile nyumba ni ilikuwa imejitenda na ilikuwa na eneo kubwa sana hvyo majirani unawaona kwa majirani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].Basi nko zangu jikoni ambapo mlango wa jiko unatazamana na chumba cha kulala mzee wangu (R.I.P my wisdom and philosopher) hapo kati ndio korido had mlango wa room yangu pamoja na sebulen. Basi mzee nahangaika niwashe mkaa mara nkasikia saut hapo kwny hilo kolodo...nkatulia labda kuku wa mtu kaja ndan.nkasikia tena sauti safari hii nliisikia vzr maana ni kama uchukue kiatu chenye soli ngum halafu uwe unakanyaga sakafu yenye mchanga.duuh nkaona zile sauti zinazid kusonga mbele kuelekea maeneo ya room kwangu na sebule.Sauti zenyew zinapokanyaga zinaachiana sekunde mojamoja...Mzee nlijikaza hata hewa nikawa sivuti vzr nkajongea mpk pale kwny lile pazia langu ambalo yule mtu mwny kanz na baragashia alipotelea nkalishika ilinione kama kaingia room kwangu maaana hakuna mlangonwa kuufunga,Ndg jamaen ile kulishika lilepazia nilipigwa shot yaumeme ambao hata waya wake sijauona.nlitoka mbio mpk nje huko nlikaaa mpk mzee anakuja saa1 usik.Nikamueleza,wiki ile tuliihama ile nyuma.
Why? hukumsaidia mwenzako na alikuita sana.
 
Hilo tukio lako la kukuta watu saa tisa wapo darasani wanasoma liliwahi kunikuta hata mimi, ila mimi haikuwa darasani....ilikuwa mida hiyo hiyo mibovu, nikiwa kikosi fulani huko Nachingwea mwaka 2013. Siku hiyo nipo zamu, kiongozi wa eneo nililopaswa kulifanyia ungalizi siku hiyo. Na niliwajibika kwa sehemu mbili zote zikiwa karibu: sehemu A, na ambapo zamu ilinisoma sehebu B, lakini nikiangalia sehemu zote mbili.

Jioni katika kushusha bendera nikawapanga watu wa kituo A ndo washushe, halafu sisi wa kituo B tutapandisha asubuhi. Na mimi nilikuwa wa mwisho kulinda siku ile, ina maana baada ya kuzurura zurura mpaka saa 6 nkaamua nilale ili saa kumi nishike zamu yangu. Sasa ilipofika saa kumi kasoro nikaamka, pako salama nikawapumzisha waliopo nasi wa zamu ya saa kumi tukaamka... Nikamwambia mwenzangu hebu baki hapo mi nifike kituo A nikacheki nako kuko poa, sasa nikiwa naenda kituo A nkapita sehemu ambapo kuna milingoti ya bendera... wacha kabisa, nikakuta watu wawili wafupi mno kwa kipimo cha kawaida wananifika kiunoni, wapo kwenye milingoti ya bendera wanashusha bendera, wamevaa kombati, wana silaha kama kawaida, na nyuma yao kuna watu nane wapo kwenye paredi ya kushusha bendera! Nikatulia nikawacheki, baadaye wakamaliza, wakageuka nyuma, wakaungana na paredi hao wakasepa kuelekea kwenye misufi... na wakapotea.

Nilishangaa sana maana sisi bendera tukishusha huipeleka kituo A, wao wakapeleka kwenye misufi na wakapotelea huko. Siku za baadae nilipowauliza wakongwe wakasema hiyo ni kawaida, yaani sisi tunaposhusha hao hupandisha, na sisi tunapopandisha wao huwa washashushandio , ila shukuru hawajakuona... wakasema hivyo vituo unaweza ukashangaa hata usiku magari yanawashwa hafu humuoni anayeyawasha, mabovu hutengenezwa na usimuone anayeyatengeneza pia... nikastaajabu sana!!!
Si useme ulikuwa kikosi no 41

Sent from my SO-01K using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka nlikuw bado nasoma sekondari wakati huo nikiw form2.Kuna nyumba moja tulikiw tukiishi ilikuw na mauzauza sana,yaan ilikuw ikifika jion nawaza sana,maana pia wakati huo nlikuw naishi na baba yangu tu.Ilikuw ikifika usik unakuta watoto wanalia dalini,usk njozi mbaya,mauzauza ya ndotoni yanamalizikia unapofumbua macho unaamka.

Sasa kuna siku tulipata wageni ambao walikuw ni binam zangu.Hao binam walikuw wa5.Wa3 kati yao walitangulia kufika kitambo kdg hvyo hali ya pale walikuw wanaijua lkn hawa binam 2 wakike walikuw ni wagen kbs.Binam hawa waliokuja mara ya mwisho walikuw wakike mmoja alikuw tyr ninmtu mzma kbs na alikuwa na yale wanaita maluhan kama sikosei na mwngne alikuwa bado mdg nadhan alikuw 10yrs

Sasa usiku wa siku ile waliyofika ikabid sisi wakiume tuwapishe room yetu na tukajilaze huko sebuleni kwny makochi.Basi tukalala fresh.Sasa mimi kwakwel ikiw kama kuna mchaw au shughul ya kichaw usk huwa nakosa usngnz kbs.Basi ndivyo ilivyokuw siku ile,yaan kila nikilala ni mauzauza naamka kila nikilala amuzauza naamka,wenzangu wanakoroma tu hapo,bas bwana mida ileile ya hatar(saa9)yule binam wa kike akaniita kwa kwa saut kama yenye kutaajab sana,nikaenda kule kumsikiliza akaniuliza je pale nyumban kuna wachaw?wachaw huwa wanakuja na kusumbua?[emoji38][emoji38][emoji38] aisee nikamshangaa nikamuiliza kwani vp bina.Akasema anawasikia wachawi wanapika ugali jiko(jiko ilikuwa ukitoka tu pale chumbani unatokea koridoni mlanho wa kwanza sebuleni wa pili jikonupande wa kulia)nikamjib nikwel bina pale ndani ni tatzo sana.Basi akasema anaomba tuende mimi na wale binam zangu wengne tukalale mle chumbani,ikawa hvyo.

Tukatandika godoro na mito ya makochi tukalala[emoji38][emoji38][emoji38](mito ya makochi kulalia shughul sana tuliiweka upande wa ukutan tukasapot na godoro)
Mungu mwaminifu na mimi ndio nikapata usingiz!!!!!!!!!!!!!!!

Aisee kuna zile ndoto mtu unaota lkn kila kitu katika ulimwengu halisi unakiona ndotoni yaan nikama huoti bali unashuhudia kwa macho,maana upepo unafeel kabs,mazingira ni very vividy yaan kila kitu ni kama vile vile,basi mimi ndio nikaota niko juu sana kama nimening'inizwa halafu chini ndio nyumban penyewe ndan ndio nmelala,nikiaangalia toka kule juu naona hadi ndani,upepo unanipuliza na barid lile la kule nyanda za juu kusini nalisikia,ukungu nauona.Kutoka kule juu nliweza kukna hadi ndani ni kama paa na dali vilikuw vimeondolewa,pale ndani kulikuwa na watu wamevaa nguo nyeupe sana lakn walikuwa na damu mdomoni ni kama walikuwa wametoka kula lkn ni walikuwa wamekula ovyo ovyo kama mtoto mdogo alavyo yaan walichafuka mdomoni hadi mashavuni kwa damu.Aisee ghafla nikakuta naanza kuanguka kuelekea mle ndani.Ile nawakaribia tu nikashtuka usingizini hadi nakuamka hapohapo(yaan ile kufumbua macho na kuinuka hapohapo)

Pale ndio niliona kitu sjui kama ntaona tena maishani mwangu.Vile nmeinuka na nlikuwa nmelala miguu imegeukia mlangoni nliona mtu mweupe naweza kusema alikuwa mwarabu au mzungu sjui mhindi kwa jins ya nywele zake.Mtu yule alikuw amevaa kanzu nyeupe sana na baragashia vile alikuw anaenda sikuiona sura yake,lakn alipofika karibu na mlango atoke kbs haikuwa hvyo(chumba changu hakikuwa na mlango wa kufunga jamani ila pazia tu ambalo nalo kuliingiza kwenye ile kamba yake ilikuw ni taab maana kamba ilikuwa na vifundofundo halafu njia ya pazia ilikuw nyembamba pia hvyo hata ufanyaje lile pazia haliwezi kuteleza kwenye ile kamba)Yule mtu badala yake lile pazia lilislide[emoji38][emoji38][emoji38] nayy hakupitiliza kutoka bali alisimama na akaanza kuslide kwenda kulia kuingia ukutani huku pazia likirudi polepole kufunika eneo la mlango ambapo tu yule anaiacha.Aisee niliganda tu nilikuwa kama kopo hiv.kuongea siwez kuita siwezi.mpk yule mtu kapotea kbs

Sikumsimlia mtu nlibaki nalo mwnyw.

2.PALEPALE MLANGONI YULE MTU ALISLIDE KUINGIA UKUTANI SASA SIKU YA MWISHO NA BAADA SIKU KADHAA TUKAHAMA.

Siku hyo nmetoka skuli fresh jion kama kawaida yangu nikajipikia mlo nikala nikapata usingiz kdg.Kwny saa12 na nusu jion nikaamka nikasogea pale jikon niweke mambo sawa.Mlango wa kutokea nje nmeurudishia kizushi.

Aisee ile nmekaa sjui nawaza nn mawazo yako mbali pale jikon nikasikia hatua za miguu,zile hatua nikama skuna za kina dada(skonkinko[emoji38])koh koh koh yaan zinakanyaga kwa kuachiana kaumbali fulani hv very fair.Ule mwendo ni dhahil ni wa kimiss miss au kama mdada anatembea kimaringo(ila zile saut zilikuwa zinaambata na kama mchanga unasagika unapokuta na vile viatu(sjui)na sakafu)bwana bwana nikawaza nani kaingia bila kupiga hodi?form yangu hii warembo nawaogopa kweli nan huy sasa?nikatoka nachek koridon holaaa nikawaza (au kazama chumban kwangu na vile hakuna mlango wa kufunga ni oazia tu?)nikajongea hadi pale mlangoni.Ile niguse lile pazia(upande uleule wa pazia yule mwamba mzungu sjui mwarabu alipotelea)nilipigwa shoti ya umeme kwny lile pazia nikashangaa sana...nilikimbia sikufunga mlango nikaenda njian nimsubir baba (MUNGU AKUPUMZISHE MSHESHIMIWA)aje tuingie wote na nimueleze lile tukio.Kwel baba alikuja ndio tukaingia nikamueleza akaniambia usjal mwanagu keshokutwa tunahama.

MAWAZO YANGU:Nadhani kuna watu wanajenga nyumba kwajili ya kutunzia mambo ya nguvu za giza,kuzugia ndio wanapangisha watu.Tuwe makini na watoto wetu,kuna vitu wanaona sana tuwasikilize na tusipuuzie.
Jina La Yesu Ni Dawa.
 
Kanole alikuwa hasemi kitu aiseee... Kuna yule mweusi mrefu hiviii alikuwa anapenda kusema Ngurutuu mnaharisha sababu mnakulaaa maviiiii....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😅😅 hii mgambo moja
 
Pole mwagito[emoji28]
 
Hii siyo Chai kweli
Alikuja asubuhi akatutania nyie vijana ni (wajeshi sana) akimaanisha wakakamavu, baada ya wiki Tulipewa notice akidai anataka afanye ukarabati wa nyumba yake[emoji23]
Hii siyo Chai kweli😂😂😂😂
 
Hahahaaa Mimi ilikuwa siyo kukimbia,
nilikuwa nakatiza uwanjani mida ya saa sits hivi,
Ila nikitembea nasikia kabisa maisha yanaendelea kama mchana,napishana na watu na wanaongea,
nilikuja kushtuka alfajiri natembea palepale uwanjan
Ulidandia mtumbwi wa vibwengo hukua uwanjani
 
huyu mganga nilenda kwake kwa maelekezo ya ndugu yangu
niliyakuta na kufanyiwa sitasahau. mwisho nikagoma kuendelea na akaniambia hapo tulipofikia na kuyafanya tuyatunze mioyoni mwetu, yaani iwe siri. naogopaga hata kusimulia
Mimi naijua dini ila sometimes najitoaga ufahamu na kufanya ya duniani, hivyo nina ka hirizi kangu natembea nako
juzi kati nikawa safarini kwenda dasalam, nikasema ujinga huu kutembea na hirizi kwenda jijini, nikaiweka kwenye kimfuko cha pembeni ya begi
kufika sehemu ya kuchimba dawa ,ile nanyayuka, maumivi makali kwenye nyonga, nikasema labda sababu ya kukaa sana, nilikuwa seat ya mwisho .Nimekaa dar siku nne zote nameza dawa za maumivu ya nyonga,lakini wapi, yapo tu
Jioni ambayo kesho yake narudi bara, nikasema ngoja nichukue kahirizi kangu nikakaweka mfukoni. Maumivu yakapotea ghafla.
Mpaka leo silewi kilikuwa ni nini
Mshana Jr
 
Umeshaingia kwny mfumo
 
Mkuu jibu ni YESU KRISTO pekee huna haja ya kutembea na hirizi ni mizigo hiyo.......

Pole sana bwana mtukutu wa nyaigela
 
Back
Top Bottom