KISA CHA NYUMBA YA KUPANGA ILIYOKUWA NA MAUZAUZA KIPINDI NIKO
Baada ya baba yangu kuachana na mama yangu wa kambo aliwekuwa ananisulubu huku ananifunza maisha tulihama ule mtaa na kuhamia mtaa mwningne mtaa mwa ng'ambo maana unavoka bonde kubwa sana.Kipindi hicho nlikuwa darasa la 6.
Baada ya kuhamia kwny ile nyumba mambo yalikuwa shwari kbs kipindi cha mwanzoni,huku tukikaa mimi na baba tu na wapangaji wnengine vijana wawili wakisabato.Nyumba ilikuwa ya mtindo wa self containing kwamba choo iko ndani na wote tunaitumia pamoja wale wapangaji wa kisabato.Sisi tulikuwa na sebule kubwa chumba changu,cha baba pamoja na jiko wakat wale jamaa upande wao walikuwa na chumba chao jiko na se hall ambayo walikuwa hawaitumii na hata hicho choo kilikuwa upande wa kwao.
Basi baada ya kipindi fulani kupita nadhan itakuwa nlikuwa darasa la saba tayar maana tuliahamia mwishon mwa mwaka,nlianza kuota ndoto za kutisha sana tena sana ukizingania miaka yangu ndio hyo 13 au 14 hv,nlikuwa naota ndoto niko makaburini ambayo yako jirant tu pale mtaani,yaan naota nimevaa mavazi meupe na naona kuku wekundu wanakimbizana pale makaburini mimi hapo nakuwa nasali sana hadi mwanga meupe unatokea then nashtuka nmeloa jasho na nimechoka ni ndoto NAJIAMBIA.
Tuko darasa la saba mwanzoni pale darasan akafariki mwanafunzi mwenzetu tenaaa nlikuwa nakaanaye dawati moja,[emoji3064][emoji3064][emoji3064] yule bwana alikuwa na vipaji vingi sana,ijapokuwa uwezo wa darasani ulikuwa sio mzur sana,jamaa alikuwa anajua kucheza mpira vzr sana,bek mzr foward ndio kabs kipa ndio usiseme,jamaa anaogelea kinoma mchizi zile nyimbo za kongo anacheza hadi unapenda but alikuwa hajui kuchora na alikuwa anapenda kuchora,mimi ndio nlikuwa masta wa michoro.Hvyo nlikuwa namfundisha,jamaa alikuwa artist naturally,sikuwahi kumwambia ila nlikuwa najua.
Basi ikafika siku hyo nko na jmaa zangu wnegne mtaani tunacheza zetu akaja rafikiangu nyumba ya jirani akaniambia bwana kuna mwanafunzi unasoma nae kafariki,akaniambia sifa zake alivyo nikatambua kuwa ni jamaa ninae kaa nae kiti kimoja pale class,but sikuamini sana sabab huyu mtoa taarifa anakuwaga na masikhara sana na siku hyo ilikuwa siku ya pili kabla ya kuanza wiki mpya ndio jamaa kafariki ghafla.
Basi nkaenda kwa jamaa nlikuwa nasoma nae tukakutana na jamaa mwngne wa pale class tukawa watatu,wote hatukwa tunaamin lile taarifa maana mwana alikuwa afya njema kbs,maana hata jamaa mwngne akaanza kutania na kuleta mzaha juu swala lile.
Ikafka siku tunaripot shule baada wikend kuisha,ndio tukajipatia ukwel halis,Wanafunzi wa madarasa mawili ya juu tukaambiwa na mwalim mkuu tutaenda kumuaga mwenzetu lakn hatutaenda kumzika maana atasafirishwa hadi kijijini kwajili ya maziko.Tukafika msbani pale majonzi mengi na vilio tukaingia chumbani alikolazwa marehemu,Mwili umelala pale tumbo limekuwa kubwa na kavaa nguo za shule...dah kiukweli nasema wazi.Mimi uchungu siku ukaniisha nikakuta niko relaxed ni kama jamaa hajafa.Hadi nkashangaa kwann.Mwili ukaandaliwa ukawekwa kwny jeneza tukawa tunapita kuuangalia....[emoji3064][emoji3064][emoji3064] nasema wazi kbs nlipigwa tu butwaa ubongo ulifreeze sikuwa na ufahamu bali nlikuwa lite headed,sikuw na judgement nzur hata kidg sjui kwnnn lakn maan kila nichek kwny kioo cha jeneza mi naona kiza totoro na shada za maua,nkamuuliza mwanafunz wanmbele ya ngu vp umeona? akanijibu ehhh tena uso umevimba sana hadi umegusa kioo[emoji3064][emoji3064][emoji3064] nikiangalia huku najongea mandg sion kitu.Tukamaliza mjongeo tukaenda kusimama pembeni ila kichwani mawazo na fikra nying zinanijia.Kitu gan kimefanya nisimuone yule ndg pale kwny jeneza?Sikupata jibu maana tukaambiwa sasa turudi majumbani tukapumzike na tulipoti shule baada ya siku 3
Tukarudi majumbani but mimi nikiwa troubled sana huku tayar iman kuwa jamaangu kafanyiwa kitendo sicho,nlifika nyumbani na mbua ilinyesha sana siku ile.Mimi nkaamua nkalale maana nlikuwa nmechoka sana.
NDOTONI
Nikiwa nmelala nikaanza kuota lakn kuota kwnyw sio kwa kawaida ni kama niko active awake kbs,nkaona niko makaburini kule jamaa anazikwa,ilikuwa ni kwny kilima kias,watu wamezunguka kaburi huku mvua inanyesha,na kwakwel nikamuona marehemu nae ananiangalia mimi,ana huzuni mpweke.Kuna mtu nyuma yake kama kawaida nashuhudia mazishi.Sikumtambua mtu yyte pale makburini ila niliamka nimeloa jasho huku nahema ovyo...Nikanyamaza maana hata wa kumuambia sielewi.
Siku 3 baadae kama kawaida nmelala nkaomuota tena jamaa,safar hii nlikuwa nasikia akiniita jina langu maana sasa nkaona nipo maeneo ya kwao nje ya uwanja kabla hujaingia fensini
Jamaa ananipa directives nimfikie alipo,ananiambia "X njoo uwanjan kabla hujaingia getini kushoto kuna shimo"kweli sikuwa naogopa bali nlikuwa najiskia kama adventure hiv nikafika pale kweli kuna shimo toka nlipo kama mita tano.Lakn lilikushimo dogo mithili ya mdomo wa chungu cha mboga lilikuwa rough sana vipande vya vyungu vilivovunjika na majivu.Ajabu kila nikisogea panakuwa pakubwa baadae likawa pango kbs,nkaingia nkajikuta nipo kwny shimo limekaa kama chungu ndan halafu kuna uwazi kuelekea upande mwngne ambao ndio sasa nlikuwa namsikia jamaa ananiambia "x jifiche bibi anakuja asikuone".Ndg sielew ilikuwaje bali mimo nlikuwa kamtu kadg sana bibi yake sikumuona sura bali nliona miguu mikubwa imevaa ndala inashuka kutoka nje huku mimi nikiwa chini kushoto pembeni ya tuta miguu inamopita....masalaaleeee nliamka ktk njozii hii jasho kama kawaida.
Jamaa baada ya hapo alikuwa anajia ndotoni haongei tena bali ananitazama sana,hapo nlianza kujisikia vibaya sana na guilty ni kama sikumsaidia jamaangu,aliendelea kunitokea but haongei na alikuwa na huzuni sana,mara ya mwisho kumuota ilibid ndio nimwambie "J mbona ulushakufa wewe?"alicheka sana baadae alipotea.Ikawa mwisho.
ILE NYUMBA YA KUPANGA NAYO SASA
Mara zote nlipokuwa natoka shule baada ya kujipikia chakula basi nalala usngz,baadae naamka naweka mabo sawa jikoni then nafanya kazi huko nje.
Sasa ilikuwa ikifika usiku tu hali inakuwa sio nzr baba anakabwa mpk namsikia ananiita inabid niende nikamuamshe,then anasema ni wachawi,sasa kipind baba anapokuwa ananiita ndani kwake nasikia saut ya kama ukizama ndani ya maji ile saut inayosikia ndio nakuwa naisikia,bas mzee nae akakubal kuwa panashida.Uski watoto wanalia darini mara bundi kwnye kamba uwanjani na kila kitu ilimradi vitimbi.Sasa wakat wote huo wale wapangaji wenzetu hatujawah kudiscuss nao hali inayoendelea pale ndan bali kila tu anapigana vita yake,wale jamaa walikuwa wanaamka usik wanapiga maombia ya kutosha.so pale ndan hapakuwa clean
Kuna binamu yangu mmoja alikuja kututembelea,yeye ana kama mizimu huwa inamwambia vitu,wakat mwngne anakuwa kama kachanganyikiwa but ndio hali yake kwa kipindi hicho.Huyo binamu hakuwa kufika kabla pale nyumban hapo awal hyo ilikuwa ndio awam ya kwanza.Ikabid mimi nimwachie alale chumbani kwangu na mdg wake na mimi na binam yang mwngne tulale sitting room,ikawa hvyo.
Sasa usiku ule kule jikoni wakawa wanasikika watu wanapiga soga huku wanasikika kbs wanapika na ugali maana sufilia lilikuwa linapiga kelele mtindo wa kutoa vishindo vidogovidogo huku banio la ugal nalo kama linafyatuaka na kupiga kelele,daaah mazee pale ndan hatunaga panya wala nyau.Yule binamu wetu mwenye watu kichwani akaniita kwa sauti kubwa hadi nikashtuka,nikaenda kule room kumsikiliza,akanuliza "Bina,hapa ndan kuna wachawi?"heheheh nkajua tu hilo sio swali bali ananiambia nikamjib ni kweli wachaw wapo na wanasumbua sana...akasema tukalale nae kule ndani basi ikawa hvyo na tayar muda ule ilikuwa mida yenyew ya 9 usik.
Basi tukatandika mito ya makochi pale chumbani tukalala zetu,Mazee ule usiku ulikuwa special sana kwa wachawi sijui how ila tu timbwili lile lilikuwa sio mchezo.Tukalala mimi kama kawaida ni mzee wa njozi, kaanza kuota tena vivid kbs nko hewani juuu na kilichonipeleka sielewi ila tu nlikuwa na elea nyumba naiona toka juu vzr na ajabu naona na kitu ndan kama haina paa.mzee nkaanza kushuka kwaspidi isiyoelezeka,wakat nakaribia nkaona pale sebuleni kuna watu kama waarabu lakin wanabarakashia na kanzu wamenyanyua mikono kama wanataka wanidake huku midomoni wamejaa damu,sisemi uongo na sipata faida yyte kuusema,nlipokuwa nawakaribia tu nkaaamka tena sio kufumbua macho tu bali hadi kuinua kichwa,UCHAWI NA MAJINI VIPO nliona pale mlangoni maana tulilala miguu inaangaliana na mlango tena mlago haukuwa na lango lenyew la kufunga na komeo bali mapazia ya mtumba ndio yaliwekwa,pale mlangon nliona mtu 3seconds vivid kbs kavaa kanzu nyeupeee na barakashia na alikuwa anangozi nyeupe anapotelea kulia koridoni,pazia halikuwa lifunguliwa kama tulivozoea bali pazia lilikuwa linaslide kwny kamba yake,sasa na lile pazia ni mimi ndio nililiweka ila jins ya kulipitisha kwny ile kama ya ilikuwa kazi hvyo kulislaidhisha haikua rahis ukichangia na kuwa ile kama ilikuwa na vifundo.basi pazia lili slife na mtu alipotelea kiupandeupande koridon lakn nikama anaingia ukutani hv.kama vile mlango wa dvd deck unaingia ndani.i was shocked nlipouliza wenzangu kama wameona hakuana hata alieona chchte.
Basi tukalala kukakucha fresh.
KIBWANGA KILICHOTUHAMISHA KABISA NYUMBA.
Siku hyo kama kawa mtabe niko zang form 2nmetoka shuke nmechoka nkapika nkala then nkadose off,mida ya saa 12 hv nkaamka then nkaenda jikoni,niwakumbushen kitu ile nyumba ni ilikuwa imejitenda na ilikuwa na eneo kubwa sana hvyo majirani unawaona kwa majirani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].Basi nko zangu jikoni ambapo mlango wa jiko unatazamana na chumba cha kulala mzee wangu (R.I.P my wisdom and philosopher) hapo kati ndio korido had mlango wa room yangu pamoja na sebulen. Basi mzee nahangaika niwashe mkaa mara nkasikia saut hapo kwny hilo kolodo...nkatulia labda kuku wa mtu kaja ndan.nkasikia tena sauti safari hii nliisikia vzr maana ni kama uchukue kiatu chenye soli ngum halafu uwe unakanyaga sakafu yenye mchanga.duuh nkaona zile sauti zinazid kusonga mbele kuelekea maeneo ya room kwangu na sebule.Sauti zenyew zinapokanyaga zinaachiana sekunde mojamoja...Mzee nlijikaza hata hewa nikawa sivuti vzr nkajongea mpk pale kwny lile pazia langu ambalo yule mtu mwny kanz na baragashia alipotelea nkalishika ilinione kama kaingia room kwangu maaana hakuna mlangonwa kuufunga,Ndg jamaen ile kulishika lilepazia nilipigwa shot yaumeme ambao hata waya wake sijauona.nlitoka mbio mpk nje huko nlikaaa mpk mzee anakuja saa1 usik.Nikamueleza,wiki ile tuliihama ile nyuma.