ALL IN ONE
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 262
- 176
Habari za kazi wakubwa
Biashara ya mkaa Ni biashara ambayo inawez kukutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ,hivo kwa fursa hyo napenda yeyote ambaye atakuwa vizuri tuwekeze pamoja katika mchanganuo huu lakin kwa upande wangu nitawekeza nguvu zaidi (yaani Sina mtaji).
Update:
Biashara yetu hii hatutauzia mijini wateja wetu wote wanafwata porini tunapochomea, na wateja wa huku wanakuja na mifuko ya kujazia wao wenyewe.
Kwanza tujue Nini kinahitajika ili kupata matokeo mazuri, mkaa tutakao choma hapa sio mti Poli yan ule mgumu tutachoma wa kawaida.
💢Kununua miti kwa wastan miti wanaanza kuuza tsh laki mbili eneo linakuwa kubwa la miti.
💢Gharama za ukataji miti hyo kwa ajili ya kupanga zinagharimu elfu hamsin.
💢Gharama za upangaji tanuli hlo la mkaa tutatumia watu wawili ambao nitasaidiana nao na kwa siku tutawalipa tsh elfu sita maana inaweza tumia siku mbili sawa na elfu ishirini na nne.
💢💢Kwa ujumla Gharama zitakazo maliza maandalizi Ni tsh laki mbili na elfu Sabin na nne ,hivo inabidi tufanye makadilio kwa sababu tupo Poli iwe laki tatu kamili...
Matokeo baada ya kupanga tanuli na kuchoma
💢 Kwa miti tutakayoipata hyo la laki mbili yaweza kutoa tanuli tatu za uhakika tanuli moja ambalo hupangwa na kutoa gunia hamsini hivo kwa tanuli tatu tutakuw na gunia 150. Na gunia moja huku huku polin linauzwa tsh elfu kumi hyo bei anakuja kuchukua anayejumua hvo huja pamoja na mifuko yake hapo sisi hatutahusika kwa Gharama yeyote.
💢💢 Hivo baada ya kuwekez tsh laki tatu .matokeo yake baada ya uendeshaji tunapata tsh million na laki tano
💢💢 na kazi za uchomaji hutumia siku Saba kwa tanuli la gunia hamsini
💢💢💢💢💢
Kama upo tayali ndugu karibu tuwekeze Mimi nitatoa nguvu zangu(Sina mtaji) nawe mwenzangu Kama upo vizuri kifedha wekeza
💢💢💢
Nipo mkoani Njombe hivo kazi hizo tutazifanyia Sana huko maan itakuwa rahisi kwa upatikanaji wa miti
💢💢💢 Karibu pm tuyajenge
Maoni ya Wachangiaji

Jamaa anachosema ni kweli kabisa, nilishafanya hiyo biashara kama muandaji na mnunuzi wa mkaa.
Mtaji mkubwa hapo ni nguvu ya kukata, kusomba miti na kuandaa tanuru.
Cost za kifedha ndio hizo za kununua miti, chakula camp, mafuta ya elfu 10 kwa mashine ya kukata miti kwa haraka kuliko kutumia shoka.
Huyu jamaa kusema kuchangia gharama ameamua kugawa faida kubwa, wanachofanya wakulima wengi wa mkaa, unampa advance ya kununua mzigo anaanda mkaa ila anakuuzia gunia elfu 7 badala ya elfu 10.
Ndio maana nimemshauri jamaa asiuzie mkaa shambani, atafute mtu wa kuchangia mtaji, waandae mkaa, wanunue roba, wakodishe vibali 30,000, walipe ushuru, watafute advance ya lori fuso kama laki 4 wakodi gari, wakifika mjini wakiuza mkaa wanamalizia pesa ya gari milioni 1 na laki 1. Sijajua kama nauli ya fuso ya njombe to dar ilishapanda.
Wakiuza huo mkaa dar gunia 150 hawakosi faida ya milioni 2
Hasara za biashara ya mkaa zipi?
1. Kununua mkaa ambao ni chenga, ukiuza gunia kwa kupima inakataa balaa lakini kama unachoma mwenyewe au unasimamia wakati wanajaza maroba unapata mkaa mzuri.
2. Vijana wauzaji ambao sio waaminifu
3. Kuhonga mademu/wateja wakuu.
4. Hasara za kujitakia kutokuwa na vibali
Ni miaka 3 sasa imepita tangu niache hiyo biashara.