Njoo tuwekeze kwenye biashara ya mkaa kijana mwenzenu sina mtaji

ALL IN ONE

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
262
Reaction score
176
Habari za kazi wakubwa

Biashara ya mkaa Ni biashara ambayo inawez kukutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ,hivo kwa fursa hyo napenda yeyote ambaye atakuwa vizuri tuwekeze pamoja katika mchanganuo huu lakin kwa upande wangu nitawekeza nguvu zaidi (yaani Sina mtaji).

Update:

Biashara yetu hii hatutauzia mijini wateja wetu wote wanafwata porini tunapochomea, na wateja wa huku wanakuja na mifuko ya kujazia wao wenyewe.

Kwanza tujue Nini kinahitajika ili kupata matokeo mazuri, mkaa tutakao choma hapa sio mti Poli yan ule mgumu tutachoma wa kawaida.

💢Kununua miti kwa wastan miti wanaanza kuuza tsh laki mbili eneo linakuwa kubwa la miti.

💢Gharama za ukataji miti hyo kwa ajili ya kupanga zinagharimu elfu hamsin.

💢Gharama za upangaji tanuli hlo la mkaa tutatumia watu wawili ambao nitasaidiana nao na kwa siku tutawalipa tsh elfu sita maana inaweza tumia siku mbili sawa na elfu ishirini na nne.

💢💢Kwa ujumla Gharama zitakazo maliza maandalizi Ni tsh laki mbili na elfu Sabin na nne ,hivo inabidi tufanye makadilio kwa sababu tupo Poli iwe laki tatu kamili...

Matokeo baada ya kupanga tanuli na kuchoma
💢 Kwa miti tutakayoipata hyo la laki mbili yaweza kutoa tanuli tatu za uhakika tanuli moja ambalo hupangwa na kutoa gunia hamsini hivo kwa tanuli tatu tutakuw na gunia 150. Na gunia moja huku huku polin linauzwa tsh elfu kumi hyo bei anakuja kuchukua anayejumua hvo huja pamoja na mifuko yake hapo sisi hatutahusika kwa Gharama yeyote.

💢💢 Hivo baada ya kuwekez tsh laki tatu .matokeo yake baada ya uendeshaji tunapata tsh million na laki tano

💢💢 na kazi za uchomaji hutumia siku Saba kwa tanuli la gunia hamsini
💢💢💢💢💢

Kama upo tayali ndugu karibu tuwekeze Mimi nitatoa nguvu zangu(Sina mtaji) nawe mwenzangu Kama upo vizuri kifedha wekeza

💢💢💢
Nipo mkoani Njombe hivo kazi hizo tutazifanyia Sana huko maan itakuwa rahisi kwa upatikanaji wa miti
💢💢💢 Karibu pm tuyajenge


Maoni ya Wachangiaji
 
Daah! Njombe napaogopa sana, niliwahi kuingizwa mjini kwenye kilimo cha viazi yaani mtu akiniambia anatokea Njombe namuangalia sana màana nakumbuka hela yangu na utapeli uliotokea kwangu.
 
Kuna mtu anauza mkaa

Anafata mkoani huko Kwa malori

Gunia 700 au kwake kitu kidogo sana

Cha kushangaza kila siku ana shida

Kila siku anauza nyumba anayoishi

Anaenda Jenga ingine kabla haijaisha kapata tena shida anauza

Niliwahi sikia biashara ya mkaa kuna aina ya miti kama inaku laani hivi...unapata shida zisizo isha..unaposhiriki kukata na kuchoma hiyo miti

Siamini but then again
 
Mkuu nayo ni businesses kama zingine zina risk pia tena kubwa tu,kuna mdada moja namfahamu tena Msukuma ila makazi yake alihamishia Njombe kufanya biashara hiyo Mara ya kwanza nilikutana naye akiwa ana kodi semi trailer anajza mkaa na kupeleka DSM-kwa kuona vile nilijua life lako lingekuwa super sana.

Siku moja nilimtembelea kwa lengo LA kujifunza,akanieleza kuwa aliacha hiyo biashara na haitaki tena amehamia kwenye mazao sababu ilimpelekea hasara sana.alinitaji sababu nyingi sana
 
Daah..! Njombe napaogopa sana, niliwahi kuingizwa mjini kwenye kilimo cha viazi yaani mtu akiniambia anatokea Njombe namuangalia sana màana nakumbuka hela yangu na utapeli uliotokea kwangu.
Viazi havina tofauti na madini ni kilimo cha risk vibaya sana kuliko hata nyanya.na risk ni kwa wote Mkulima na mfanyabiashara.
 
Shida kubwa wengi huipenda biashara ya mkaa lakini huingia kujumua hapo ndo inawagharimu lakini ukinunua miti ukasimamia mwenyew kuchoma hutojutia.

💢 Ila changamoto zipo pia ndugu
 
💢💢 Changamoto ipo pale utakapo wekwa mtu Kati yaan huo mkaa ukajumue au uchukue kwa madalali huwezi kufaidik hata uwe na gunia Mia ..lkn kma unasimamia mwenyw naiman utapat kitu afu Jambo zuri kuuzia polin huko ndo utaion faida
 
Biashara zenye mavibali vibali mengi na milolongo hasara zake huwa zipo hatua moja mbele
Vibali vinahitajika pale unaposafilisha mkaa lakin hii biashara yetu haihitaji vibali vyovyote hivyo risk sio kubwa
 
Laki na na nusu unaweza kupata milioni na laki tano, alafu umeshindwa kukuza mtaji unatafuta mtu wa kuwekeza, kuza mtaji wako songa mbele.
 
Mchanganuo mzuri sana
 
Dah, ni biashara nzuri tatizo niko mbali yanj Zenji..mpaka nivuke maji...sasa hata nikiingia ubia na wewe mara moja kunitia changa la macho😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…