Njoo uwekeze kwenye biashara ya mafuta (Fuel) kwa laki 1 tu kama kima cha chini

Nikiwa kama mfanyabiashara Uliposema tu muwekezaji hatahusishwa na hasara ndo uliponipeperusha........hio deal wazungu wanasema ni "too good to be true"
kumbe umemwelewa huu ni high level utapeli
 
Dah..bosi kampuni yenu ni DINI gani? Nimevutika mno..[emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Dah...Bosi huwezi jua lengo la kampuni....labda ni kusaidia watu..au kufua pesa....
Wanachukua mkopo kwa watu na kuulipa riba ya 120% kwa mwaka...wakati benki Sasa hivi Hadi 16% kwa mwaka unapata .....
Kama si wapigaji nitajiunga nao...ila siyo kwenye biashara yao..bali kwenye dini yao......[emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Hatari hii. Kuna sheria inavunjwa hapa. Kampuni private (LTD), hairuhusiwi kukusanya mtaji kutoka kwa public (uma) namna hii. Public company (PLC) mahali pake ni DSE.

Else aseme yeye ni benki anakusanya deposits....but ikiwa hivyo biashara ya mafuta haipo.

Lakini pia return (ROI) ya 10% kwa mwezi haipo mahali popote duniani....I can bet hata wanachimba mafuta hawapati hiyo ROI.

Nipo tayari kufundishwa/kuelimishwa hapa kuhusu hili....nimesoma zamani, huenda mambo yamebadilika sasa.

Mwanzo nilidhani ni issue ya April Fools, but naona ni thread ya 31/03/2019.
 
Mkuu nimetoa ufafanuzi wa kutosha tu hapo juu namna ya ufanyaji wetu kazi na kila kitu kinafanyika kisheria hakuna longo longo. Kwa maelezo zaidi karibu ofisini kwetu Chanika Dar Es Salaam ujionee mkuu na upate ufafanuzi zaidi. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbe umemwelewa huu ni high level utapeli

Mfanyabiashara yeyote/tafsiri sahihi ya mjasiriamali ni lazima uingie risk ya pata potea ndo njia pekee ya kuongeza thamani ya pesa yako.

Hiki anachokielezea ni kama njozi. Yani wao wabebe gharama za uendeshaji na wabebe hasara halafu wewe wakupe tu faida? Charity work??? Maybe

Basi kila mtu angekua tajiri kama kuna mfumo huo wa biashara
 

Mfumo wa benki una taratibu zake. Hizo fixed deposit accounts hazijakuwepo tu. Kuna biashara ambako hio hela inapelekwa "low risks" kama government bonds au treasury bonds na vitu km hivyo. Na bado kuna usimamizi mkubwa wa BOT ili kumantain liquidity ya taasis husika

Pia biashara nyingine ambayo unawekeza na hela yako inaongezeka tu(haiwezi kula kwako) na haina gharama za uendesheji ni mifuko ya pensheni. Ina taratibu mahususi zake

Ila hii yalwako nashangaa. Hakuna gharama za uendeshaji na hakuna hasara ni faida tu. Nyie mnachapisha noti au?

Halafu kusema sehemu nyingi duniani wanafanya hivo hata telegram/deci kila aina ya ponzi schemes ziko dunia nzima hio sio sababu.

Kinachoniogopesha ni kuwa mfumo wenu wa biashara unavunja miiko yote ya biashara toka dunia iumbwe.

Unaposema ukiweka hio hela unakua sio shareholder sasa shareholder ni nani kama anayewekeza sio shareholder. Kitendo cha kuongeza mtaji kwa nia ya kupata faida automatically unakua shareholder.

Labda unipe maelezo zaidi. Unaweza kunishawishi mimi nifunge biashara zangu zoote niwaletee hata milion 200 halaf nikae likizo nasubiria miez mi3 nipate gawio la 10% bila kufanya kazi yoyote bila risk yoyote
 
Chanika mkuu, Karibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina Uzoefu mkubwa na mambo ya mafuta,
Ukisema Chanika napata wasiwasi pengine ni kituo kidogo tu cha mafuta unazungumzia. Labda unataka mjichangishe mnunue Kurasini au Kigamboni na kuuza rejareja au kwenye Petrol Station yenu kisha mgawane faida. Ukitumia bei za "Platt" basi faida ya mafuta haizidi hata 100/=. Watu wako tayari kwa uwekezaji, lakini unahitajika kua muwazi zaidi. Unless kama unaogopa kuibiwa idea yako.
 

Huwa kuna wakati nawashangaa watu kama nyie. 80% ya wana JF wamevurugwa kiamaisha (kwa mujibu wa tathmini yangu isiyo rasmi) halafu wewe unakuja na uzi usio na kichwa wala miguu.. Let me warn you si kila siku ni ijumaa acheni hizo mwisho wenu si mzuri sana.

Wana JF hii ni kama zileeeee...
 
Huo ndo ukweli, ukiona unaitwa kwenye fursa jua ww ndo fursa

Sent using My phone
 
Ndugu naomba nikujulishe tuu hiki unachokifanya ni kinyume na sheria za nchi kwahiyo hakuna mkataba ambao utasimama kwa sababu mkataba ni batili toka mwanzo ( void ab initio). Kama ungekuwa unauza share za kampuni tungekubaliana ni sawa ila hii kitu unafanya hakuna huwezi kuchukua hela kutoka kwenye public halafu ukaahidi kutoa riba wakati ujasajiliwa kama taasisi ya fedha Soma Kifungu cha sita 6(1mpaka 4 cha Bank and finance act see a link https://www.bot.go.tz/BankingSupervision/BAFIA2006.pdf ) Ukipata muda wa ziada unaweza kusoma kesi namba 66/2007 kati ya ULF NILSON dhidi ya Dr Tito M Andrew imeambtanishwa hapo chini.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…