Njooni tumuombe msamaha Mo kwa yote yaliyotokea

Njooni tumuombe msamaha Mo kwa yote yaliyotokea

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Ule msemo wa kuwa Siasa haina rafiki au adui wa kudumu naomba leo uhamie kwenye soka!

Mimi binafsi naomba Mo unisamehe, niliaminishwa maneno kuwa wewe ni mbaya na jamaa fulani ila leo nimeamini tulidanganywa!

Kweli muda ni mwalimu mzuri sana!
 
IMG-20210824-WA0022.jpg
 
Dunia ina mambo. Yaani Manara huyu huyu aliyekuwa analia Simba ikifungwa eti leo kaenda Yanga na kuvaa jezi ya kijani? Poleni bodi ya Simba wachezaji, wanachama na mashabiki wote kwani mlikuwa mnauzwa bila kujua kwa muda mrefu. Na iwapo huyu jamaa angekuwa Simba kwenye mechi ya Kigoma basi hata lile kombe mngekosa.

Aisee Simba mnapaswa mumushukuru sana na kumpa zawadi aliyewapa siri ya kuwa Manara ni Yanga lia lia na anawahujumu kwani leo kadhihirika wazi kabisa. Maisha yangu yote sijawahi kuona shabiki damu wa Simba kwenda Yanga au wa Yanga kwenda Simba halafu akapewa nafasi ya uongozi. Kwa wachezaji kidogo linaeleweka lakini si kwa uongozi.
 
Siku zote nilikuwa najiuliza kwa miaka hii mitatu/minne iliyopita inakuwaje Simba ipo "on fire" kweli kweli lakini ikikutana na Yanga wanakaa kimajabu ajabu wakijipapatua sana ushindi wao ni droo. Leo ndio nimejua sababu mubashara kumbe walikuwa wanahujumiwa bila kujua.
 
Back
Top Bottom