Dunia ina mambo. Yaani Manara huyu huyu aliyekuwa analia Simba ikifungwa eti leo kaenda Yanga na kuvaa jezi ya kijani? Poleni bodi ya Simba wachezaji, wanachama na mashabiki wote kwani mlikuwa mnauzwa bila kujua kwa muda mrefu. Na iwapo huyu jamaa angekuwa Simba kwenye mechi ya Kigoma basi hata lile kombe mngekosa.
Aisee Simba mnapaswa mumushukuru sana na kumpa zawadi aliyewapa siri ya kuwa Manara ni Yanga lia lia na anawahujumu kwani leo kadhihirika wazi kabisa. Maisha yangu yote sijawahi kuona shabiki damu wa Simba kwenda Yanga au wa Yanga kwenda Simba halafu akapewa nafasi ya uongozi. Kwa wachezaji kidogo linaeleweka lakini si kwa uongozi.