Njooni Tusemezane sasa, Neno au jina la Walokole limetokea wapi, na linamaanisha nini kwenye imani?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Neno la Bwana katika Injili iliyoandikwa katika
Mathayo 28: 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Je neno au jina la Walokole limetokea wapi? Je kuwa Mkristo ni hatua ya awali kisha ulokole ni daraja la juu?

Je ni ubaguzi ndani ya dini au ni kujihesabia haki zaidi ya wengine?
 
Ni kujihesabia haki kulikochanganyika na ujinga,coz utamsikia muamini akikwambia “Mimi kabla sijaokoka ulikuwa hunikosi bar nilikuwa nakesha bar mpaka asubuhi” wakati huo huo skate mtaani hazimpiti.

Ameacha kukesha bar sasa anakesha guest akizini anadhani kwa sababu haonekani basi siyo dhambi,na hii tabia wanayo sana hawa wanaosali kwenye mabanda ya mabati full suit Wasabato included.
 
Naam mkuu
Tunaweza kupatq facts za hili?
Neno "Walokole" limetokea kwenye lugha ya Kiganda kutoka Uganda.

Maana yake halisi:
Walokole = "Waliokolewa" kwa Kiswahili
Inatoka kwenye kitenzi cha Kiganda "okola" = kuokoa

Historia fupi ilivyotokea:

Miaka ya 1930 huko Rwanda na Uganda kulikuwa na kundi la Wakristo waliokuwa na shauku kubwa sana na Mungu. Waliitwa "East African Revival" kwa Kiingereza.

Watu wa kawaida walianza kuwaona na kuwaambia:
"Aba lokole" kwa Kiganda = "Watu waliokolewa"
Kutokana na maisha yao ya toba, kuomba sana, na kuishi tofauti na wengine.

Neno hilo likasambaa sana East Africa yote. Hadi leo nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda wanatumia Walokole kumaanisha Wakristo waliozaliwa mara ya pili au Wakristo wa Pentekoste/Karismatiki waliokolewa na wanauishi maisha ya utakatifu.

Kwa hiyo leo:
Unaposikia "Walokole" inamaanisha:
1. Kikundi cha watu waliopata wokovu
2. Mtindo wa ibada wenye sifa za: kuimba kwa nguvu, kuomba, kuhubiri wokovu, na maisha ya kuepuka dhambi

Kitu cha kufurahisha:
Awali neno lilikuwa ni la kejeli kidogo. Watu wengine waliwatania wakisema "hawa ni Walokole". Lakini baadaye wakalibeba wenyewe kwa fahari 😊

Kwa kifupi: Walokole = Waliokolewa na Yesu
 
Je neno au jina la Walokole limetokea wapi? Je kuwa Mkristo ni hatua ya awali kisha ulokole ni daraja la juu?
Ni neno la Kitanzania tu lililotokea kule east african revival, nadhani ilikuwa miaka ya 1930 kutokana na dhana ya Kuokoka.

Maelezo mengine nasubiri kujifunza pia kwa watakao kuja kujibu hapa.
 
Ni kujihesabia haki kulikochanganyika na ujinga,coz utamsikia muamini akikwambia “Mimi kabla sijaokoka ulikuwa hunikosi bar nilikuwa nakesha bar mpaka asubuhi” wakati huo huo skate mtaani hazimpiti.

Ameacha kukesha bar sasa anakesha guest akizini anadhani kwa sababu haonekani basi siyo dhambi.
Kama haonekani wewe umejuaje kwamba analala guests?
 
Neno "Walokole" limetokea kwenye lugha ya Kiganda kutoka Uganda.

Maana yake halisi:
Walokole
= "Waliokolewa" kwa Kiswahili
Inatoka kwenye kitenzi cha Kiganda "okola" = kuokoa

Historia fupi ilivyotokea:

Miaka ya 1930 huko Rwanda na Uganda kulikuwa na kundi la Wakristo waliokuwa na shauku kubwa sana na Mungu. Waliitwa "East African Revival" kwa Kiingereza.

Watu wa kawaida walianza kuwaona na kuwaambia:
"Aba lokole" kwa Kiganda = "Watu waliokolewa"
Kutokana na maisha yao ya toba, kuomba sana, na kuishi tofauti na wengine.

Neno hilo likasambaa sana East Africa yote. Hadi leo nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda wanatumia Walokole kumaanisha Wakristo waliozaliwa mara ya pili au Wakristo wa Pentekoste/Karismatiki waliokolewa na wanauishi maisha ya utakatifu.

Kwa hiyo leo:
Unaposikia "Walokole" inamaanisha:
1. Kikundi cha watu waliopata wokovu
2. Mtindo wa ibada wenye sifa za: kuimba kwa nguvu, kuomba, kuhubiri wokovu, na maisha ya kuepuka dhambi

Kitu cha kufurahisha:
Awali neno lilikuwa ni la kejeli kidogo. Watu wengine waliwatania wakisema "hawa ni Walokole". Lakini baadaye wakalibeba wenyewe kwa fahari 😊

Kwa kifupi: Walokole = Waliokolewa na Yesu
Thread ifungwe zaidi ya hapa basi mleta mada atakua na chuki bifsi
 
kila kitu huwezi ukafanya kwa usahihi utaonekana wakati ukiingia au matokeo ya hayo unayoyafanya mafichoni yataonekana hadharani mimba maradhi etc.

Mungu tu anajua yupi msafi yupi mchafu kujifanya mwokovu ni kujilisha upepo.
Hivi wote wanajifanya au baadhi yao?
 
😊
Kwa kifupi: Walokole = Waliokolewa na Yesu
Je Bwana Yesu alitaka sisi tuliookolewa kwa kumkiri tuitwe wanafunzi wake au walokole?

Nimeelewa ulichokieleza hapo juu kuhusu WANAUAMSHO (Revivals) wa kutoka Baganda.

Twende kwenye muktadha wa aliyetukomboa alitaka tuwe au tuitweje?
 
Walokole siwakubali hata siku moja. Lazima mkubaliane na huu ukweli wangu, lakini msinitenge ndugu zangu.
Kuwakubali ama kutowakubali siyo tatizo sana.
Kwanza wanajua maana ya hilo neno mlokole au walokole linamaanisha nini?

Mantiki hujenga dhana ya kushawishi ili kukubalika ama kukataliwa.

Dini😀
 
Je Bwana Yesu alitaka sisi tuliookolewa kwa kumkiri tuitwe wanafunzi wake au walokole?
Uanafunzi ni mchakato mwingine mara baada ya kuokoka. Mlokole = Aliyeokoka. Siyo kila aliyeokoka ni mwanafunzi wa Yesu, ila wapo walokole ambao ni wanafunzi wa Yesu.
 
Kwa muktadha upi?

Utudadavulie hii hoja yako mkuu
 
Back
Top Bottom