Njooni tusemezane. Sheria gani inakataza watu kuchangishana? Waziri Mkuu yupo sahihi kumkamata Niffer?

Njooni tusemezane. Sheria gani inakataza watu kuchangishana? Waziri Mkuu yupo sahihi kumkamata Niffer?

Embu peleka upumbavu wako huko hiyo sheria haikatazi mtu mwingine kukusanya michango.
Watu wanaweza kukusanya ila wanatakiwa waiwasilishe kwenye kamati ya maafa.
Sasa huyo binti si alikuwa anawasaidia kukusanya halafu awapelekee.
Kimsingi Kasimu Majaliwa kachemsha sana kwenye hiyo ishu kwa kutoa agizo la ajabu na hovyo kabisa AMEKURUPUKA
Unless otherwise wangemsubiri akusanye na asingeziwasilisha kwenye kamati ndio wamkamate.
Wewe ndo miongoni mwa lile jeshi la Niffer (zombie wake)

Vifungu vya sheria unavyo lakini hata akili ya kuvielewa huna.

Onyesha sehemu palikoandikwa kwamba mtu binafsi anaruhusiwa kukusanya michango kwenye maafa ya kitaifa kupitia account zake binafsi kwa lengo la kwamba ataiwasilisha kwenye kamati.
 
Sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2022, kifungu cha 26(2) inasema jukumu la kuchangisha litafanywa na Kamati ya maafa iliyo chini ya ofisi ya Waziri mkuu, kupitia akaunti maalumu.

Kiufupi ni kwamba Niffer alikuwa anaingiliia majukumu ya ofisi ya waziri mkuu, mbaya zaidi akaanza kujibizana na waziri mkuu mtandaoni huku akijinasibu kwamba ana jeshi kubwa nyuma yake...... Nadhan hilo jeshi alimaanisha watu kama wewe mtoa mada
Wachukue hela wamuachie Madam..Mbona kosa Takatifu tu hilo?
 
Kabbla hajasajili mwaka 2022 tulikuwa tunatuma kwenye no zake za voda, nimeanza kuchangia 2020 kabla hajasajili, nyie UWT kwanini hamnaga akili? kwani TCRA wameshindwa nini kutrack miamala aliyochangisha kama ameiba? mara kwa mara tunachangia watu huku kitaa nani huwa anagonga mhuri? Nifer hajasema ni mchango wa lazima ni hiari yeye Majaliwa amechangia na kwanini ameumia kuliko sisi tuliochangia? Kuna alichangia amelalamika hela yake kuliwa? baada ya faza kunyimwa mzigo ameamua kumkomoa dada wa watu.
Zamu ya nani kumpelekea chakula Niffer usiku huu?

Wewe bwabwaja mwenzio akiachíwa atakapoanza kumsifu mama Samia ndio utajuwa hujui Bar vichaa.
 
Tangu huyu PM adanganye kuwa rais aliyepita yupo ofisini anachapa kazi wakati ameshakata moto sina imani nae tena
Mnakuza hili jambo, kwani nani alisema ukweli hadi mumkazanie Majaliwa tu ndio alisema uongo? Hata Samia alisema Rais anaumwa vimafua tu, ila sioni watu kumuandama nae kuwa alisema uongo.
 
Ni jambo la kusikitisha na pengine kukera..km mtu anafikia umri km wako au wa niffer lkn hajui maana ya neno ORDER au UTARATIBU kwa vitendo..shule ya kwanza kwa binadamu ni nyumbani kwa wazazi wako, na kati ya wanayokufundisha ni kufuata ORDER, unaambiwa muda wa kulala, muda wa kuamka, muda wa kula nk..na wapo/yupo anayetoa hizo ORDER, ukienda shule hali ni hiyo hiyo..km mtoto wa miaka 3 anaweza kujua na km kuna chochote kipya nje ya utaratibu lazima aulize..mtu mzima anashindwa vipi kukumbuka tunaishi kwa ORDER??? mfano watu 100 wangefanya hivyo alivyofanya kukusanya michango, unadhani nini kinaweza kutokea..unaweza kulist hasara za kufanya hivyo?? lakini moja iko wazi..haitakuwa rahisi kufahamu nani kati ya hao 100 anakusanya michango ya wahanga wa tukio na nani anakusanya kwa kutapeli..!
Tuwe na kumbukumbu, kila kitu/tukio au mambo yanayotokea kwa nadra upo utaratibu wa jinsi ya kufanya..si lazima kuwepo sheria!
Haiwezekani watu mia kukusanya michango wewe!
Akitokea mmoja kuchangisha hakuna mwingine atatokea!
 
Wewe ndo miongoni mwa lile jeshi la Niffer (zombie wake)

Vifungu vya sheria unavyo lakini hata akili ya kuvielewa huna.

Onyesha sehemu palikoandikwa kwamba mtu binafsi anaruhusiwa kukusanya michango kwenye maafa ya kitaifa kupitia account zake binafsi kwa lengo la kwamba ataiwasilisha kwenye kamati.
Soma hiko kifungu namba 36 (2) halafu nitafsirie umeelewaje hicho kifungu.
Kwa mujibu wa hicho kifungu watu wa kawaida wanaruhusiwa kukusanya michango na kuiwasilisha kwenye kamati .
Wewe utakuwa kichwa maji flani walamba viatu aka machawa wa viongozi.
Huyo majaliwa kachemsha vibaya sana
 

Attachments

  • Screenshot_2024-11-19-15-09-34-72.png
    Screenshot_2024-11-19-15-09-34-72.png
    274.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom