Ngoja nikujibu upande wa trekta maana ndio napata kula na kuendesha maisha huko.
Kwanza nikutoe wasiwasi wa kusema trekta zipo nyingi sana. Trekta bado ni chache sana hapa nchini, yani hazitoshelezi mahitaji ya wakulima. Na kwakua upo Dodoma basi experience yako ya matrekta nahisi itakua ime base hapo Dodoma hasa maeneo ya Kibaigwa.
Trekta na bajaji vyote vinahitaji usimamizi wa hali ya juu. Trekta ukikuachia dereva afu wewe unasubiri hesabu jioni, nakuambia utapigwa vibaya mno(naongea kwa uzoefu hapa). Utapigwa mpaka utatamani ukatambikiwe na ukoo.
Kama huna muda wa kusimamia trekta lako achana nalo. Hela hiyo kawekeze sehemu nyingine. Ila kama una muda wa kutosha kusimamia basi trekta litakutendea maajabu mazuri mno.
Naona unataka trekta lako lifanye kazi Dodoma, kama utabase Dodoma peke yake basi ni matumaini yangu una uhakika wa kazi za kutosha hapo. Ila ni bora uwe mtu wa kuzunguka maeneo tofauti tofauti. Ujue misimu ya maeneo husika na gharama za kufanya kazi huko alafu uamue kwenda au kubaki. Mimi huwa naenda Ifakara, Kilosa, Tanga, hadi Matui. Kote huko nazunguka na matrekta. Vile vile ujitahidi uwe unalima na mashamba yako, hii itakupa faida zaidi.
Usiwe mtu wa kukubali kila kitu unachoambiwa na dereva wako au dalali. Ukipewa taarifa yoyote kuhusu kazi au matengenezo ya chombo chako, ichukue hiyo taarifa, ichakatez omba ushauri ikiwezekana then chukua maamuzi. Na uwe mtu wa kwenda kukagua wewe mwenyewe physically. Biashara ya simu pekee isiyo na wizi ni betting tu. Huku kwingine ukifanya biashara kwa simu utaibiwa ni suala la muda tu.
Yapo mengi sana ya kuelezea kuhusu biashara ya kukodisha trekta. Ila nitayaeleza kadri utakavyouliza maswali. Kutype kwenye simu kunachosha.
NB:Nauza trekta used massey ferguson, farmtrack na new holland. Kama unahitaji moja kati ya trekta tajwa hapo usisite kunitafuta pia. Makao yangu ni Morogoro mjini