Samahani
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 221
- 335
KAZI ni mojawapo kati ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu. Mahitaji muhimu katika maisha ya mwanadamu ni matokeo ya kazi. Unapokatiza mitaani, katika mitandao ya kijamii, majarida na wavuti mbalimbali, maombi na matangazo ya kazi vinapewa kipaumbele kikubwa. Wengi hudamka asubuhi kuziangazia kurasa za ajira, wengine wakiperuzi kujua mustakabali wa maombi yao. Eneo hili mara nyingi huwalenga zaidi wataalamu na wasomi mbalimbali wa kati na wabobevu. Hapa, wapo wanaopata na wapo ambao wanaendelea kungoja.
Kadhalika, kila siku tunasikiasikia au kuona fursa mbalimbali za ujasiriamali na wengine wakijitumbukiza huko. Huku nako, wapo wanaofanikiwa na wapo wanaoendelea kusubiri!
Nimetafakari kwa kina juu ya uhusiano baina ya hawa ambao wana kila hadhi ya kuitwa “wasomi na wataalamu” na wajasiriamali, (nikiyalenga makundi ya wajasiriamali wadogo kabisa na wale wanaoanza).
Imekuwa bayana kwangu kuwa, kuna tatizo pahala! “Wasomi” wanazunguka na bahasha kutafuta ajira! Matarajio yao ni kuwa, waajiri pekee ni serikali, kampuni, mashirika, taasisi na asasi. Ni wachache wanaoweza kuwapa kipaumbele wajasiriamali wadogo kuwa wanaweza kuwa waajiri. Kadhalika, wajasiriamali nao wanawatazama na kuwahukumu wasomi hawa kuwa ni “watu wa daraja la juu sana” kiasi cha kutoweza kufikiwa kirahisi.
Kwa kuziangalia changamoto za wajasiriamali ambazo nyingi zimeshaandikwa na kuelezwa sana, ipo kila sababu ya “wasomi wa bahasha” kujaribu kuzitumia elimu zao kubwa katika njia rahisi na inayofaa kuzitatua baadhi ya changamoto nyingi wanazokutana nazo wajasiriamali wachanga. Nitaziainisha tu baadhi ya taaluma kati ya nyingi ambazo pamoja na ukweli kuwa zimekuwa na wahitimu wengi wasio na ajira, zinahitajika sana kwa ustawi wa ujasiriamali hapa Tanzania.
i. Sheria
Wajasiriamali wengi bado ni waathirika wakubwa wa vikwazo kwenye mikataba, sera, sheria zinazosimamia biashara, sheria za kazi hasa kwa wale ambao wamefikia uwezo wa kuajiri na namna ya kuthibitisha na kutunza nyaraka na hakimiliki kisheria. Hizi zimepelekea wengi wao kufikia hatua ya kushindwa kabisa kuendelea na biashara. Lakini ni wazi kuwa, mtaani tunao wahitimu wengi mno wanaozunguka wakitafuta ajira. Kama wangejikita katika kutatua miongoni mwa changamoto hizi, ni wazi kuwa changamoto hizi tungezipunguza.
ii. Uhasibu na usimamizi wa fedha
Wasomi na wataalamu wa fedha wa kati na wabobevu tunawahitaji kutusaidia kutatua changamoto kama vile kushindwa kukokotoa faida na mtaji, hatua za kupata mikopo, uhifadhi wa fedha na mengine mengi. Mathalani, mama ntilie mbobevu, anahitaji ushauri mzuri juu ya namna ya kukuza mtaji kutoka kwenye “price discrimination theory”. Aondolewe hofu na wataalamu wetu wa benki kuwa kukopa ni kuuziwa nyumba na hofu zingine zinazofanana na hiyo.
iii. Rasilimali watu
Wajasiamali wengine wameishia kuwa watumwa wa makampuni ya kibiashara kwa mgongo wa ajira. Gazeti la Mwananchi, toleo la Jumanne 12, 2022 katika Makala yake “Mtego wa ajira unavyowanasa vijana wengi” liliangazia jinsi vijana wengi wanavyotumbukia katika mtego kwa “kuajiriwa” kinyemela na makampuni, mengi yasiyo hata na usajili. Wao wanajitambua kama wajasiriamali ambao kimsingi wanalipwa kwa kile ambacho wameuza, lakini kiuhalisia wako katika mateso na manyanyaso makubwa. Hapa, wataalamu wa fani ya sheria na rasilimali watu tuna jambo la kuweza kufanya tofauti na kuendelea kungoja ajira kubwa bila mafanikio.
iv. Teknolojia ya Habari
Mojawapo kati ya msingi muhimu sana wa ukuaji wa ujasiriamani ni upatikanaji wa taarifa sahihi, kwa wakati sahihi na mbinu ya kuzichanganua taarifa hizi ziweze kuwa na tija katika biashara. Ndio maana katika siku za hivi karibuni, jumbe kama vile “na mikoani tunatuma” zimekuwa maarufu. Wapo ambao hawahitaji ofisi kuuza bidhaa zao, bali huhitaji simu zao tu na mitandao ya kijamii kuwafikia wateja wao. Hii pia ni fursa kubwa kwa wataalamu wetu wa fani ya teknolojia ya habari kufikia lengo. Kumbuka, wao wana mbinu. Wanapokutana na wenye mawazo, mbinu zao zinahuishwa kuliko kuendelea kuzurura na bahasha za kaki.
v. Lishe, Kilimo na ufugaji
Umekuwa ni wimbo wa kudumu kuwa, “kilimo ni uti wa mgongo wa taifa”. Sijakataa. Lakini wajasiramali waliojiingiza kwenye kilimo na ufugaji, bado wanakabiliwa na changamoto kama vile namna ya uhifadhi wa vile wanavyozalisha, ufungashaji na namna ya kuongeza thamani ya kile wanachozalisha. Katika wavuti rasmi ya Wizara ya Kilimo, Wakala wa taifa na hifadhi ya chakula wanakiri kuwa mojawapo kati ya changamoto zinazowakabili wawekezaji katika kilimo ni kushuka kwa bei za nafaka pamoja na uwepo wa mawakala wasio rasmi wa ununuzi. Hapa nauona waziwazi mchango mkubwa wa wataalamu wetu wa Lishe, Kilimo na ufugaji katika kutuelekeza njia sahihi kabisa za kufuata.
vi. Saikolojia
Leo hii asilimia kubwa ya wanasaikolojia wazuri utawapata katika idara nyeti kabisa. Wajasiriamali wengi tunaishia kwenye sonona na baadae kuachana kabisa na biashara kwa msongo mkubwa wa mawazo. Wachache tunaosalia, tunateseka tukiwaza namna ya kurejesha mikopo au wapi tukakope tena. Wapo walioishia kujiua kutokana na kuyumba kwa biashara zao ndogo walizozihangaikia kwa muda mrefu. Njooni wataalamu wetu wa afya ya akili, ili mtusaidie katika udogo wa biashara zetu, tena kwa ada ndogo kabisa, ili tusonge mbele, tufanikiwe tuwape ujira mkubwa zaidi.
Njia ya kufikia lengo
Ni wakati muafaka sasa wa kuangalia namna bora ya kuimarisha mitaala yetu kwa kuwaandaa pia wasomi hawa kuwa washauri na waelekezaji kwa taaluma zao (consultants). Ni wakati wa kuwa na ofisi nyingi zaidi za watendaji wanaokutana na jamii moja kwa moja, tena kwa bei rafiki kabisa, lengo likiwa, mosi, kukuza zaidi vipaji na taalima zao katika yale waliyoyasoma kwa nadharia darasani. Pili, kuwawezesha kukuza zaidi sekta walizozisomea. Ni jambo linalotia faraja sana kwa taaluma pale tunapokuta kuwa, jamii ya wafanyabiashara wadogo wana uwezo wa kujieleza vema juu ya maswala yanayoihusu taaluma hiyo. Tatu na muhimu zaidi, ni kukuza ujasiriamali na kuongeza kipato!
Ni vema katika hili tukakumbuka kuwa, wapo ambao wamejaliwa maarifa katika kuibua mawazo lakini wanakosa rasilimali na utaalamu wa kutosha wa kuendeleza mawazo yao. Hapa sasa ndipo umuhimu wa ushauri wa kitaalamu (consultancy) unapotusaidia kuwaunganisha watu hawa.
Huenda wengi kati ya “wasomi” hawaliwazi hili kutokana na aina ya kipato ambacho wanakitarajia. Ninaamini kuwa, bado ujasiriamali una nafasi kubwa zaidi ya kukua, na fursa nyingi bado hatujazifikia kutokana na aina ya muingiliano tulionao sasa baina ya “wenye elimu” na “wenye jicho la fursa”. Tukiboresha na kuimarisha mahusiano kwa namna nilivyonyumbulisha hapo juu, ni wazi kabisa tunaweza kukuza kipato zaidi na kila mmoja akafaidika kutokana na kile anachokifanya kwa ajili ya mwenzake.

Upvote
6