Nkana wataka mil 800 kwa Bwalya , Simba wagoma

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Imeripotiwa kuwa klabu ya Simba imegoma kutoka kiasi cha fedha ambacho Nkana Red Devils wanakitaka ili kumuachia mchezaji wao Walter Bwalya.

Taarifa za ndani zinasema Nkana wanahitaji kiasi cha dola 350,000 sawa na shilingi milioni 800 za kitanzania jambo ambalo limekuwa ni gumu kuzitoa.

Uongozi wa juu wa Simba kupitia kwa Ofisa Mtendaji wake, Crescentius Magori, umesema kwa fedha hiyo hawataweza kumsajili Bwalya na badala yake watamsaka mchezaji mwingine.

Imeelezwa kuwa Magori amefunguka kwa kusema Nkana wanadai fedha kubwa tofauti na uwezo wa mchezaji mwenyewe ulivyo kitu ambacho kinaleta ugumu kumnunua.

Tetesi za Bwalya kutua Simba zimeanza muda mrefu lakini mpaka sasa pande zote mbili hazijaelewana juu ya usajili wake.
 
Simba bado hajafika level za kuwanunua hao watu.
Level za Simba ni kama Yanga tu bado, average players au la sivyo wawekeze kwa wachezaji ambao ni vijana wenye kuweza kuwa wachezaji wazuri.
Angekuwa amemaliza mkataba ingekuwa rahisi kumsajili
Timu zetu kuvunja mikataba na kununua hazijazoea
 
Na mtu kama Huyo akimaliza mkataba unakuta tayari ana timu nyingi zinamujitaji.
Watafte kwa club za kawaida ambazo zina strikers wazuri.
Simba pesa ipo labda wanaangalia mkali zaidi ya huyo
 
Kama hajaiweka bilion 20 sasa pesa gani ambayo ametoa mfukoni?

Mzee Kilomoni ashtukà ila vijana mbubumbu bado mpo kizani
Process hazijakamilika za kufanya aweke bilioni 20 kwenye account ya Simba kuwa muelewa wewe,
Pesa inayotumika Sasa Ni Kama ufadhili tu
 
Hahahaha mali kauli, ndo mnavyoambïwa hivyo kuwa process hazijakamilīka? ponjoro mjanja sana
Process za kurasimisha Mali za Simba bado ikiwemo hati alionayo mzee Kilomoni na nyaraka zingine zipo kwenye kesi inayowakabili Aveva na Kaburu so zote zitakapopatikana pesa itawekwa hiyo haina shida
Punguza wenge Simba iko makini
 
Hizo stori za vijiweni hakuna biashara ya kuuza Kagere kwa bilioni 1.2
Niligoma na nitaendelea kugoma. Hakuna mchezaji wa bn anayecheza Tanzania. Nakubaliana na mdau aliyeandika kwenye huu Uzi kwamba Mo anawaoverprice wachezaji kwa lengo maalum analolijua yeye.
 
Process za kurasimisha Mali za Simba bado ikiwemo hati alionayo mzee Kilomoni na nyaraka zingine zipo kwenye kesi inayowakabili Aveva na Kaburu so zote zitakapopatikana pesa itawekwa hiyo haina shida
Punguza wenge Simba iko makini
Wapigaji ambao wasaka opportunities ndo wapo makini kuliko nyie wafuata upepo. Hapo klabun kwenye mtu makini ni mzee kilomoni tu, wengine mbumbumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…