Tetesi: Nkasi: Mkuu wa wilaya aamuru wananchi kupewa adhabu na wanajeshi

Tetesi: Nkasi: Mkuu wa wilaya aamuru wananchi kupewa adhabu na wanajeshi

Status
Not open for further replies.

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Katika kile kinachoonekana mwendelezo wa wiki ya vituko, kiki na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa sheria, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi bw. Said Mtanda jana 12.08.2017 aliamuru wanajeshi wa JKT kikosi cha Milundikwa kuwapa adhabu za kijeshi wananchi wa kijiji cha Ntuchi wilayani humo.

Habari zilizopatikana toka chanzo cha habari kilichokuwa eneo la tukio kwenye mnada uliopo kijijini hapo kinasema Chanzo cha tukio hilo ni kwamba, kulikuwa na Kazi ya ujenzi Wa darasa kwa njia ya kujitolea katika shule ya kijiji hicho lakini pia siku hiyo ni siku ambayo kijijini hapo kunakuwa na mnada (gulio) kila mwezi hivyo wananchi hupata fursa ya kufanya manunuzi ya mahtaji mbalimbali kwa ukaribu Mara moja kila mwezi maana vinginevyo wanalazimika kwenda mjini Namanyere umbali wa kilomita zaidi ya 20 toka kijijini hapo.

Hivyo baadhi ya wananchi walikwenda mnadani kujipatia mahtaji hasa baada ya pendekezo lao kwa uongozi wa kijiji kupanga siku nyingine nyuma au mbele ya siku hiyo kukataliwa kwa madai kuwa siku hiyo ndo Mkuu wa wilaya ana nafasi ya kuja kushiriki nao.

Mkuu wa wilaya alipowasili na kukuta watu wachache aliamuru Gari la Jeshi la wananchi kuwaleta askari Wa JKT ambao walitinga mnadani na kusimamisha shughuli za biashara na kuanza kutenga wananchi kutokana na vijiji wanavyotokea na aliyeonekana anatokea kijiji cha Ntuchi aliamuriwa kuruka kichura au kujiviringisha toka hapo mnadani hadi eneo la ujenzi umbali Wa zaidi ya mita 200. Walioonekana kushindwa adhabu hizo au kudanganya makazi walipigwa na kuburutwa.

Mtoa taarifa mwingine niliyeongea naye anasema wakazi wa kijiji hicho hasa wazee ambao wengine wameshapita umri Wa kushiriki shughuli za maendeleo wamepanga kulifikisha suala hili kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bw. Zelothe Stevine.

Kama mwandishi wa habari niko safarini Mbeya, nikifika Rukwa kesho kutwa nitakuwa na mwendelezo wa sakata hili.

-----------
Taarifa hii imekanushwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Zaidi soma => News Alert: - Usahihi wa taarifa toka Nkasi
 
~~~>>>>Hawa wakuu wa Wilaya wakapimwe "mkojo".... Inawezekana kuna kitu cha ziada wanatumia.
 
Habari hii inanikumbusha ile habari ya Mh. fulani kumtandika viboko mzazi kwa kosa alilofanya mtoto,, Kama matukio haya hayatadhibitiwa basi ushirikiano baina ya w/nchi na viongozi wao hautakuwepo na maendeleo vilevile.

*Haki itendeke*
 
Huwezi kuwa na kiongozi mkuu mwenye roho mbaya nchi ikabaki salama, taifa linaangamia kwa ujinga wa mtu mmoja tu
 
Huo mkoa wazee wake walikuwa wanaogopeka na kuheshimiwa sana kumbe siku hizi umekuwa wa mchezo mchezo? kuna haja gani ya kumshtaki kwa mkuu wa mkoa wakati "Sumbawanga" iko huko huko?
 
Tusiwalaumu hawa ma DC nakumbuka siku ya kuapishwa kwao waliambiwa wana sheria ya kuwaweka raia ndani waitendee haki. Sasa kinachoendelea kina mibaraka toka juu [emoji107]

Cairo's
 
Na cha kusikitisha hii michezo inatokea ktk majimbo yanayoongozwa na ccm
Jana baba kachezea bakora dodoma huko
Leo wanakijiji wanapiga mbizi ktk mchanga rukwa huko

Sent from my Phillips Savy
 
Nchi ina vituko hii, mtu kapata ukuu wa wilaya, tayari anajiona ni untouchable. Ipo siku na wao vitu wanavyofanya vitakuja kuwageukia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom