Tetesi: Nkasi: Mkuu wa wilaya aamuru wananchi kupewa adhabu na wanajeshi

Tetesi: Nkasi: Mkuu wa wilaya aamuru wananchi kupewa adhabu na wanajeshi

Status
Not open for further replies.
Huyu tumuite dicteta ...., madaraka yenyewe hayadumu hajui kama kunamaisha baada ya kesho.
Yaan cjui viongozi wengine wakoje hapo wanawaonea wananchi jamanii
Utafkiri ana guarantee ya kuongoza muhula ujao
 
Katika kile kinachoonekana mwendelezo wa wiki ya vituko, kiki na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa sheria, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi bw. Said Mtanda jana 12.08.2017 aliamuru wanajeshi wa JKT kikosi cha Milundikwa kuwapa adhabu za kijeshi wananchi wa kijiji cha Ntuchi wilayani humo.

Habari zilizopatikana toka chanzo cha habari kilichokuwa eneo la tukio kwenye mnada uliopo kijijini hapo kinasema Chanzo cha tukio hilo ni kwamba, kulikuwa na Kazi ya ujenzi Wa darasa kwa njia ya kujitolea katika shule ya kijiji hicho lakini pia siku hiyo ni siku ambayo kijijini hapo kunakuwa na mnada (gulio) kila mwezi hivyo wananchi hupata fursa ya kufanya manunuzi ya mahtaji mbalimbali kwa ukaribu Mara moja kila mwezi maana vinginevyo wanalazimika kwenda mjini Namanyere umbali wa kilomita zaidi ya 20 toka kijijini hapo.

Hivyo baadhi ya wananchi walikwenda mnadani kujipatia mahtaji hasa baada ya pendekezo lao kwa uongozi wa kijiji kupanga siku nyingine nyuma au mbele ya siku hiyo kukataliwa kwa madai kuwa siku hiyo ndo Mkuu wa wilaya ana nafasi ya kuja kushiriki nao.

Mkuu wa wilaya alipowasili na kukuta watu wachache aliamuru Gari la Jeshi la wananchi kuwaleta askari Wa JKT ambao walitinga mnadani na kusimamisha shughuli za biashara na kuanza kutenga wananchi kutokana na vijiji wanavyotokea na aliyeonekana anatokea kijiji cha Ntuchi aliamuriwa kuruka kichura au kujiviringisha toka hapo mnadani hadi eneo la ujenzi umbali Wa zaidi ya mita 200. Walioonekana kushindwa adhabu hizo au kudanganya makazi walipigwa na kuburutwa.

Mtoa taarifa mwingine niliyeongea naye anasema wakazi wa kijiji hicho hasa wazee ambao wengine wameshapita umri Wa kushiriki shughuli za maendeleo wamepanga kulifikisha suala hili kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bw. Zelothe Stevine.

Kama mwandishi wa habari niko safarini Mbeya, nikifika Rukwa kesho kutwa nitakuwa na mwendelezo wa sakata hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wakuu wa wilaya awamu hii sijui wameokotwa wapi maana akili zao hazina tofauti na vichaa.
 
Hapana aiseeee
Oyeeee yangu uenda kwa RC na unajua yeye hana roho mbaya kabisaaa. Huyo DC bomu bomu anatia aibu uongozi wa awamu hii.
Usimsahau na yule wa juzi aliye mcharaza viboko mzazi wa mtoto aliye vunja kioo cha gari yake kwa jiwe eti kisa mzazi huyo kashindwa kumpa malezi bora mtoto huyo aiseee!
 
OMG

Na huyu tena... hawa viongozi wengine duuuuuuu wamezidi... huyu hapana sio binadamu. Yaani kazi ya kujitolea ndio analazimisha.. hapana aiseeee hao lazima wameugua.. kisa kutafuta kiki lazima pesa anaweka mfukoni huyo. Ni mnyama
Kuna MTU amehack hii account!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilikuwa wilaya ya Nkasi, huyu DC akishirikiana na kikosi cha wanajeshi walishusha wasafiri kwenye mabasi na kuwaamuru kufagia eneo linalozunguka stendi. Eti ni jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kidamva, hili uliloongelea ni tukio la kweli na kuna mtu aliliweka Mods wakaliondoa kwa kukosa uthibitisho. Alivyoona hilo limepita amezua jipya sasa na anaotumia ni wanajeshi hao hao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kujitolea maana yake si kufanya kitu kwa mapenzi yako, sasa Tanzania kujitolea imekuwa lazima basi waache kutumia neno kujitolea watumie lazima.
Mfano walimu wanakatwa makato mara ya mwenge mara ya nini na bado serikali inadai wanajitolea
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom