NMB acheni kutuibia wakulima wa korosho

NMB acheni kutuibia wakulima wa korosho

Malcom Sr

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2021
Posts
1,163
Reaction score
1,647
Wakuu,,
Nina Hasira kwa kiwango Cha PGO huwezi amini. NMB nyie Ni wachamungu wezi na Kama wezi wengine tu ...licha ya kuwa na wateja wengi.

Ipo hivi kwenye mabango ya malipo ya korosho huwa mnapunguza pesa kiwizi Sana huwa mnashirikiana na makatibu au mmeamua kujiongeza KUTUIBIA WAKULIMA.
Mfano mnada wa Kwanza baada ya makato nilitakiwa nipate laki 722534 inakuja 711214...mmefyeka zaidi ya elfu 10 na ushee.

Mnada wa tatu bango linasoma 779384..inakuja 771201 mmefyeka zaidi ya elfu 8 na ushee..

Mjomba bango lake linasoma 4225781 inakuja milioni 4 na chenji kiduchu.

Kwa kifupi NMB TZ mmeamua kutuchakachua mchana kweupe licha ya kuwa hamkutukopesha pembejeo!

Huu wizi wenu mmefanya kwny malipo kwa WAKULIMA karibu wote ..Tunaomba mamlaka ziimulike Nmb..

Huu wizi wenu wa kishamba halafu mna ujanjaujanja wa kizamani mara oooh akaunti imezidiwa mara imezeheka mara ipo dormant halafu mkaifyeta 20k yangu.

Juzi nimefanya malipo mara 3 mmefyaka 20k kwenye laki 5.

Hela zangu nitaenda kuchimbia Chumbani...muje kuzikata wezi nyie.
 
Hivi bei ya korosho imefika kiasi Gani?Kangamba nayo ikoje?
 
Bank si salama kwa mtu wa kipato cha chini.
Hela wanayokufyeka kimasihara ukipiga hesabu kwa kuitafuta unakuta ni siku nzima au mbili.
 
Wakuu,,
Nina Hasira kwa kiwango Cha PGO huwezi amini.NMB nyie Ni wachamungu wezi na Kama wezi wengine tu ...licha ya kuwa na wateja wengi ..

Ipo hivi kwenye mabango ya malipo ya korosho huwa mnapunguza pesa kiwizi Sana huwa mnashirikiana na makatibu au mmeamua kujiongeza KUTUIBIA WAKULIMA.
Mfano mnada wa Kwanza baada ya makato nilitakiwa nipate laki 722534 inakuja 711214...mmefyeka zaidi ya elfu 10 na ushee...

Mnada wa tatu bango linasoma 779384..inakuja 771201 mmefyeka zaidi ya elfu 8 na ushee..

Mjomba bango lake linasoma 4225781 inakuja milioni 4 na chenji kiduchu...

Kwa kifupi NMB TZ mmeamua kutuchakachua mchana kweupe licha ya kuwa hamkutukopesha pembejeo!!!

Huu wizi wenu mmefanya kwny malipo kwa WAKULIMA karibu wote ..Tunaomba mamlaka ziimulike Nmb..

Huu wizi wenu wa kishamba halafu mna ujanjaujanja wa kizamani mara oooh akaunti imezidiwa mara imezeheka mara ipo dormant halafu mkaifyeta 20k yangu..

Juzi nimefanya malipo mara 3 mmefyaka 20k kwenye laki 5...

Hela zangu nitaenda kuchimbia Chumbani...muje kuzikata wezi nyie...
NMB ni WEZI sana wala hilo halina ubishi.

Ndio maana hata Makato yao Hayako wazi kabisa.

Bank yenye wateja kibao mpaka leo ukiangalia salio la pesa zako wanakata.

Ukitoa pesa hawasemi umekatwa kiasi gani kama user fee.
 
Bank si salama kwa mtu wa kipato cha chini.
Hela wanayokufyeka kimasihara ukipiga hesabu kwa kuitafuta unakuta ni siku nzima au mbili.
Unyonyaji wao hauna maana kabisa yaan jiulize km wanatuka 2000k WAKULIMA elfu 2 kwa mnada wa kata moja tu,,zidisha kata 15 ...fanya kata 15 ×4milions =60m huo mnada mmoja tu ,,,Sasa wakikata 8k Kama walivyonifanya Mimi ....huu sio uungwana kabsa
 
Back
Top Bottom