NMB acheni kuwahadaa watumishi wa umma kwa meseji za mikopo hadi milioni 200!!!

NMB acheni kuwahadaa watumishi wa umma kwa meseji za mikopo hadi milioni 200!!!

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Hivi karibuni watumishi katika idara mbalimbali wamekuwa wakipokea meseji kutoka NMB Benki zikiwataka kukopa hadi milioni 200 huku Benki ikijua kuwa watumishi hao hawakopesheki kutokana na mikopo walaiyo nayo.
NMB acheni kuwahadaa watumishi.
 
Tena zinakuwaga nyingi zile tarehe wanazojua hapa watumishi wamechacha na hapo ndo wanafululiza hizo msg zao ili kuwapata wale wasiojiongeza waingie kwenye mtego wao.
 
Nawashauri mhamie CRDB Benki yenye kuwajali wananchi wote.
Utapata mkopo wa ada papo hapo.
CRDB benki inayotoa huduma.
 
Nawashauri mhamie CRDB Benki yenye kuwajali wananchi wote.
Utapata mkopo wa ada papo hapo.
CRDB benki inayotoa huduma.
Hebu nitafutie mwenye control no chap nipige hela! 10 per cent ipo
 
75% ya mikopo inayotolewa na na mabenki ya kitanzania yanaenda kukopesha watumishi wa umma. Asilimia ndogo mno inayobakia wanakopeshwa wafanyabiashara wakubwa wenye assets kubwa sana kama maghorofa, majumba, magodown, hotels, gesti, vyumba, appartments, na mali nyingine mbalimbali ila wateja wakuu wa mikopo ya mabenki waajiriwa.
 
Kinachonizuia kuwablock nmb ni kwamba nitashindwa kupata sms kuhusu miamala basi! Bila hivyo siku nyingi sana ningewablock maana siku hizi hawa jamaa meseji zao imekuwa kero. Mara mshikofasta wa milioni mara mkopo wa mia mbili milioni mara... Mshahara wenyewe laki na nusu hayo yote ya nini?
 
Mil 200 kwa watumishi wa Gavoo huo ni mtego,km kuku kutegwa na mchele
 
Back
Top Bottom