Kuna changamoto upande wa NMB Bank, nimekumbana na changamoto ambayo hadi sasa haijapatiwa suluhisho. Juzikati nilituma fedha kwenda kwenye akaunti nyingine, zikaonekana zimekatwa kwenye akaunti yangu, lakini hadi siku ya tatu, mlengwa hajazipokea.
Nilipojaribu kuwasiliana na NMB kupitia DM, nilipewa Namba ya WhatsApp ambayo inaendeshwa na mfumo wa roboti. Nimekuwa nikifuatilia lakini muda unaenda bila tatizo langu kutatuliwa. Nikawapigia simu, nikaelezwa kuwa fedha hizo “zipo hewani” na hatimaye zitamfikia mlengwa, lakini hadi sasa bado hazijafika.
Hii si mara yangu ya kwanza kukutana na changamoto kama hii. NMB iliwahi kutangaza maboresho ya mfumo wao na baadaye ikaeleza kuwa huduma zimerejea kikamilifu, lakini kwa uzoefu wangu NMB Mkononi bado haifanyi kazi kwa ufanisi unaotarajiwa. Nimeona pia malalamiko ya wateja wengine kwenye ukurasa wa NMB Instagram kuhusu changamoto zinazofanana.
Naomba sauti yetu isikike na NMB pamoja na mamlaka husika iliangalia tatizo hili na kuhakikisha fedha za wateja zinafika kwa walengwa kwa wakati, na pale kunapotokea hitilafu, mteja apewe majibu na suluhisho la haraka badala ya kuzungushwa na mfumo wa roboti.