NMB, hesabu zenu za mkopo sijazielewa

NMB, hesabu zenu za mkopo sijazielewa

Memtata

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
587
Reaction score
1,863
Mwezi uliopita nilipata shida ya pesa nikaona kuliko kwenda kwa kausha damu bora niende NMB nikafanye top-up sababu nilikuwa tayari namkopo, lakini baada ya kuchungulia account yangu wananiambia bado inasoma negative siwezi kupata chochote!

Tangu nichukue mkopo ni mwaka mmoja sasa, lakini nimeenda bank wananiambia kwasasa siwezi kupata chochote labda nienda January kuangalia kama itawezekena. Sasa najiuliza yale makato ya mwaka mzima hayajapunguza hata mia?! na kama umepungua kwanini nikose chocote cha kuchukua? Kuna mwenzangu alienda kabla yangu ambapo alikuwa na miezi8 tu tangu achukue mkopo ila yeye alifanikiwa.

Pia naomba kueleweshwa haya kwa mwenye kufahamu;
  1. Kama mwanzo nililipia bima kwa mkopo wa miaka minne (mf. 2022-2025) na baada ya kutumikia mwaka mmoja tu nikafanya top-up ukaongezeka mwaka mmoja mbele (badala ya mkopo kuisha 2025 itakuwa 2026) kwanini nilipie bima ya mkopo wa miaka minne tena wakati nimeongeza mwaka mmoja tu?
  2. Kama mwanzo nilichukua 20m nikalipia ada ya mkopo, kabla sijamaliza deni nikafanya top-p up ikaongezeka 5m tu kwanini tena nilipie ada ya mkopo wa 25m wakati hii 20m ya mwanzo ilikuwa imeshalipiwa?
Nimejitahidi kuelezea kwa uelewa wangu kwa aliyeelewa naomba msaada kama kuna sehemu hujaelewa niulize nifafanue zaidi.
 
Unapofanya topup maana yake ni unachukua mkopo mpya lakin hupewi pesa zote, kiasi kinatumika kulipa mkopo wa kwanza then kinachobaki ndo unapewa cash, ndo maana unalipishwa bima na fee upya maana wao kwenye system ni wana process mkopo mpya, sema kuna argument kwenye kudai refund ya premium ya mkopo wa kwanza.
 
Unapofanya topup maana yake ni unachukua mkopo mpya lakin hupewi pesa zote, kiasi kinatumika kulipa mkopo wa kwanza then kinachobaki ndo unapewa cash, ndo maana unalipishwa bima na fee upya maana wao kwenye system ni wana process mkopo mpya, sema kuna argument kwenye kudai refund ya premium ya mkopo wa kwanza.
Asante sana mkuu hapa kwenye kudai refund nimekupata zaidi. Ubarikiwe
 
Umejitetea utadhani ualimu ni jinai,halafu ukute hata mshahara nakuzudi Mimi mwalimu ila akili Yako inaamini walimu ni watu wa low profile
Nilipokuwa volunteer wa elimu ya UKIMWI kuna kitu tulikuwa tunawafundisha wenye maambukizi kuhusu 'kunyanyapaa' na 'kujinyanyapaa' hili nalo lilikuwa ni tatizo kubwa
 
Back
Top Bottom