Benki inakushawishi ufanye saving au uweke akiba, wewe kwa kutokujua au kukosa elimu ya fedha unafanya wanavyotaka wao.
Fedha yako na wenzako kama wewe zinatumika katika uwekezaji wao na wanatengeneza faida kubwa sana.
Wakati huo fedha inapoteza thamani pia Kuna inflation n.k. mfano ukiweka milioni tatu akiba mwaka huu, pesa hiyo hiyo mwakani kama ilikuwa inaweza kununua mifuko 200 ya cement basi hatutaweza kupata tena mifuko 200 ya simenti kutokana na kushuka kwa thamani ya fedha au bidhaa kupanda bei.
Kwa hiyo benki wanapata faida kubwa kwa uwekezaji wa pesa za wanaoweka akiba.