NMB Kariakoo Siku ya Huduma kwa Wateja haiwahusu

NMB Kariakoo Siku ya Huduma kwa Wateja haiwahusu

katawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2010
Posts
1,103
Reaction score
2,575
Tawi lenu lililipo mtaa wa Livingstone Kariakoo ni tawi linalotoa huduma mbovu zaidi ya matawi yote niliyowahi kuhudumiwa.

Ni mara kadhaa inanichukua hadi saa tatu kuhudumiwa huku nikiwa na kadi yenu ya Loyal customers ambayo pia nailipia.

Kuna madirisha manne lkn mara nyingi kama sio zote madirisha mawili ndo yanakuwa yanatoa huduma.
Mnaofahamiana nao ambao nimewahi kuelezwa kuwa mara nyingi wanatoa takrima huhudumiwa kwa haraka na hawapangi foleni.

Vimemo vinapita, jina lake linaitwa na anapewa huduma akiwaacha wengine kwenye foleni kwa saa kadhaa.
NMB Kariakioo nadhani haina meneja mwenye uwezo wa kuwapanga wafanyakazi watoe huduma bora.

SIKU HII YA HUDUMA KWA WATEJA TAFADHALI SANA NMB KARIAKOO MSISHEREHEKEE KWAKUWA BADALA YA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA WENU, MNATENGENEZA KERO KWA WATEJA WENU.L
 
Back
Top Bottom