NMB kupata faida inayovunja rekodi zote ya TZS 775 bilioni ni matokeo ya Sera chanya na rafiki za kibiashara za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

NMB kupata faida inayovunja rekodi zote ya TZS 775 bilioni ni matokeo ya Sera chanya na rafiki za kibiashara za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Bank kupata faida kubwa ni ishara ya ukuaji wa uchumi kuwa ni WA kuridhísha
Faida wanaipata kwa kufanya biashara na serikali, kukopesha serikali, na kukopesha watumishi wa umma. Hiyo haina msaada wa maana kwenye uchumi wa nchi na watu. Inatakiwa benki ikopeshe kwa wingi biashara na kilimo, ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa ajili ya soko la ndani na exports. Hizi report ni utapeli wa kudanganya watu na shareholders. Ila kwa ground hawana impact kwa wananchi. Zaidi sana kukatakata hela zao.
Screenshot_20240201-173623.png

Hiyo table ndio inaonesha. Kati ya 6T waliyokopesha 3.7T imekopeshwa watumishi. MSE, SME na Kilimo kimekopeshwa hela ndogo.
 
View attachment 2890989
Hiyo table ndio inaonesha. Kati ya 6T waliyokopesha 3.7T imekopeshwa watumishi. MSE, SME na Kilimo kimekopeshwa hela ndogo.
Mfanyabiashara yeyote anaangalia zaidi Biashara yenye risk kidogo,

Sijui kama umeshawahi kufanya biashara
 
Mkuu pongezi zimwndee mwendazake bila yeye hii benki ilikuwa inaenda ICU kwa maksudi aliamua wafanyakazi wote wa serikali mishahafra yao ipitie NMB kwa maana hiyo NMB walipata mtaji tosha kutoka serikalini, bila mnwendazake kufanya upendeleo maalumu NMB ingekuwa hoi bin taabani penye kusifiwa tuwe wakweli na tusiwe kama akina Mwijaku.
Huu ni uongo
 
Tunachoongelea ni source of profit ya bank ambayo ina dependent sana kufanya biashara na serikali na hakuna economic impact kubwa kwenye growth kama mleta mada anavyodai (kwanza mikopo inapunguza purchasing power ya wafanyakazi).

Mikopo karibu yote interest charge is based on reducing rate so hakuna kitu special hapo.. Ukipiga hesabu za reducing rate unalipa zaidi (if, i remember correctly its been a while kufanya hesabu za hire purchase na mortgages).

But that’s beside the point, 16% interest charge is unjustifiable. Unapo set interest ya mikopo cha msingi kujumlisha ‘rate ya faida + inflation risk + default risk’.

Kwa wafanyakazi wa serikali na utaratibu NMB waliojiwekea wa watu kukatwa juu kwa juu kwenye pay slip zao huo mkopo risk aversion yake is as good as a ‘secured loan’ ya mtu anaeweka asset kupata mkopo maana kuna government warranty.

Kwa hivyo 16% is ridiculous ndio maana asset turnover yao inakuwa, faida inakuwa, over half of their asset is tied to government investments (employees loan + treasury bonds) huko ni kutegemea sehemu kubwa ya faida yao kupitia serikali.

Bila ya biashara na serikali, bank aiwezi pata hizo faida wanazoringia.

Wakitoka hapo kulinda ugali wao wanamuongopea ‘bi tozo’ unakuza uchumi wakati sehemu kubwa ya faida ni interest za mikopo ya wafanyakazi wa serikali, interest ya government bonds na services charges za wizi.

Halafu wapambe wanakuja hapa ohoo sijui huyu mama mkurugenzi ana miakili mingi sana. Akili gani wakati bank ina monopoly.

Good Afternoon, muda wa kufanya kazi huku 👋
Najua wewe ni mtumishi wa CRDB,

Umeandika mambo mengi sana fine,

But, Nataka unijibu maswali haya,

1. Je, hayo mabenki mengine yanazuiwa kukopesha wafanyakazi hasa wa Serikali?

2. Kama CRDB ni 13% why do them opt kwenda kwenye 16%?

3. Je, wanalazimishwa?

Tukubali tukatae NMB inatoa "the Good service"

"The good service is to provide who or she wants",

Kumpa kile kitu mtu anapenda ndio huduma Bora sio kile wewe unataka,

Huwezi kuzungumzia mafanikio haya bila kumtaja Ruth Zaipuna na Rais Samia Suluhu Hassan
 
Kwa muda mrefu, tunasemaga hiyo nmb inabebwa na serikali na watumishi wa serikali, haipo kwa ajili ya wananchi wa kawaida na biashara za watanzania za uzalishaji wa bidhaa na huduma. Siku serikali ikiacha kufanya kazi na nmb. Ndani ya sekunde chache hiyo benki inafilisika.

NB: Kwa heshima na taadhima, nakuomba. Uandae thread maalum yenye uchambuzi wa kina juu ya jinsi nmb wanavyoipata faida ya mchongo.
Hapo unapoiona NMB ndio tayari Serikali imeshaondoa deposit zake zote toka enzi za Magufuli,

Ndio maana unaona interms of Liquidity CRDB iko juu but before NMB ilikuwa juu.

NMB kinachowabeba ni Uongozi thabiti tu wa Ms Ruth Zaipuna otherwise yangekuwa majanga kama CRDB
 
Mkuu pongezi zimwndee mwendazake bila yeye hii benki ilikuwa inaenda ICU kwa maksudi aliamua wafanyakazi wote wa serikali mishahafra yao ipitie NMB kwa maana hiyo NMB walipata mtaji tosha kutoka serikalini, bila mnwendazake kufanya upendeleo maalumu NMB ingekuwa hoi bin taabani penye kusifiwa tuwe wakweli na tusiwe kama akina Mwijaku.
Mwendazake ndio alitoa pesa yote ya Serikali kule kwa lugha laini alitaka kuiua kifo Cha polepole

Naipenda sana NMB mpaka naumwa ndio maana familia yangu yote hadi watoto wanaakaunti NMB
 
Najua wewe ni mtumishi wa CRDB,

Umeandika mambo mengi sana fine,

But, Nataka unijibu maswali haya,

1. Je, hayo mabenki mengine yanazuiwa kukopesha wafanyakazi hasa wa Serikali?

2. Kama CRDB ni 13% why do them opt kwenda kwenye 16%?

3. Je, wanalazimishwa?

Tukubali tukatae NMB inatoa "the Good service"

"The good service is to provide who or she wants",

Kumpa kile kitu mtu anapenda ndio huduma Bora sio kile wewe unataka,

Huwezi kuzungumzia mafanikio haya bila kumtaja Ruth Zaipuna na Rais Samia Suluhu Hassan
Huko sasa ni kuleta mambo ambayo hayana uhusiano na kichwa cha habari.

Huu aukuwa mjadala wa CRDB v MNB, hoja ilikuwa kuongezeka kwa faida MNB ni ishara ya kukuwa kwa uchumi. Implying MNB inafaidika na economic activities.

Source ya mapato ya MNB ni; ‘interest income’ ndio sehemu kubwa ya mapato yao na ina uhusiano na biashara yao ya kukopesha (hapo unaweza kuona mchango wao kwenye uchumi).

Source ya pili kwenye kuingiza mapato yao ‘fees and commissions interests’ hii si mikopo ya uzalishaji bali ni mitozo ya wizi. Na source ya tatu foreign exchange aina impact kwenye uchumi if anything ni withdraw.

Sasa basi kwenye hiyo source yao kuu (interest income), ukipekuwa unakuta faida yenyewe sehemu kubwa inatokana na mikopo kwa wafanyakazi, business overdraft na treasury interest; kwa pamoja ni kama 80% ya assets zao zinazozalisha hiyo faida ya interest income.

Wakati sehemu ndogo iliyobakia kama 20% ndio inaenda kwenye mikopo ya uzalishaji kwenye kilimo, SME, Corporates and other consumptions (assuming hizi ni fixed and movable assets).

Based on that info si kweli faida ya MNB inatokana na ukuaji wa uchumi hakuna ushahidi huo, isipokuwa faida yao inategemea kufanya biashara na serikali. Sasa tena CRDB sijui NBC na mambo mengine hayakuwa sehemu ya habari ya upotoshaji inayopingwa kama ilivyowasilishwa na mleta mada.
 
Hapo unapoiona NMB ndio tayari Serikali imeshaondoa deposit zake zote toka enzi za Magufuli,

Ndio maana unaona interms of Liquidity CRDB iko juu but before NMB ilikuwa juu.

NMB kinachowabeba ni Uongozi thabiti tu wa Ms Ruth Zaipuna otherwise yangekuwa majanga kama CRDB
NMB inabebwa na mbeleko ya serikali.
 
Kwani Serikali sindio watu?
Serikali ni viongozi tu, kama NMB wanataka kuendeleza watu ilitakiwa fedha zipelekwe kwenye uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa ajili ya soko la ndani na la nje (exports). Ilipaswa fedha zipelekwe kwenye MSE, SME na Agribusiness.
 
View attachment 2891369
Hii ndio taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya NMB PLC,

Binafsi imenivutia na haya moja kwa Moja ni matokeo ya Sera Bora na rafiki za Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan, tunakwenda nae Mpaka 2030.

Hiki ni kiashiria muhimu kinachoonesha kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi sana.
===

Soma taarifa yao hapo chini,

Matokeo ya Kihistoria yenye kugusa maisha ya watu, jamii na uchumi,

Leo, Benki ya NMB tumetangaza matokeo ya kiutendaji ya mwaka 2023, yakionesha kuvunja rekodi kwa mwaka mwingine tena baada ya kupata mafanikio ya kihistoria.

Kati ya mengi, tumeweza:

➡️ Kuongeza Jumla ya mapato ya Benki na kufikia Shilingi Trilioni 1.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 mwaka hadi mwaka.

➡️ Uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato uliboreshwa zaidi hadi kufikia asilimia 39, wakati uwiano wa mikopo chechefu umeshuka hadi kufikia asilimia 3.2. Takwimu hizi zote ni chini ya ukomo wa kikanuni wa Benki Kuu wa asilimia 55 na asilimia 5 mtawalia.

➡️ Kutokana na ufanisi huu, Faida kabla ya Kodi imeongezeka kwa asilimia 26 hadi Shilingi Bilioni 775 huku Faida baada ya Kodi ikifika Shilingi Bilioni 542 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 kwa mwaka. Hiki ni kiwango kikubwa cha faida na cha kihistoria kwa Benki ya NMB na sekta nzima ya fedha nchini.

➡️ Mizania ya Benki imeendelea kukua na kufikia jumla ya mali ya Shilingi Trilioni 12.2 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 19 kwa mwaka.

➡️ Tuliendeleza ajenda ya ujumuishaji wa kifedha kwa kufungua akaunti mpya za wateja zaidi ya milioni 1.2, na kufanya jumla ya akaunti za wateja wetu kufikia zaidi ya akaunti milioni 7.1. Hii ni idadi kubwa zaidi ya wateja kwa taasisi moja ya fedha nchini.

➡️ Tuliwekeza zaidi ya Tsh Bilioni 6 kwenye elimu, afya na mazingira, ikiwa sehemu ya dhamira yetu ya kujitolea kusaidia jamii inayotuzunguka.

Akiwasilisha Taarifa ya Fedha ya Mwaka 2023, Afisa Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna amewashukuru wateja wetu, wanahisa, wafanyakazi, washirika wote wa Benki, Serikali kupitia Benki Kuu na Watanzania wote kwa mchango wenu thabiti na imani mliyonayo kwa Benki ya NMB.

Ahsante kwa kuendelea kutuamini.

#NMBKaribuYako
NMB baba lao TZ,
 
Naunga mkono hoja. Kwenye masuala ya uchumi na biashara Rais Samia anafanya vizuri
Hata sasa wazee wa baishara ya Ganda amabyo serikali haioati Kodi imetulipa sana kipindinhiki, hivyo hata benki zinapata faida kwani fedha inaigua kwenye mzyngukonwa benki nakutengeza faida
 
Hata sasa wazee wa baishara ya Ganda amabyo serikali haioati Kodi imetulipa sana kipindinhiki, hivyo hata benki zinapata faida kwani fedha inaigua kwenye mzyngukonwa benki nakutengeza faida
Hizo ngada mnauzia wapi?
 
Benki ya NMB lazma wapate faida kubwa kwa sababu kaongeza unyonyaji mkubwa sana kwa wateja

1. Benki ina Makato makubwa sana kuliko Benki zote hasa ukitoa kwa Wakala mfano ukitoa 100,000 kwa wakala wa NMB unakatwa 4500 plus Tozo ya 500 jumla unakatwa 5000 ila CRDB unakatwa 3950 plus Tozo ya 500

2. Uwepo wa makato ya kila mwezi ya shilingi 1800

3. Makato ya kila mwaka ya Shilingi 13900 kwa ajili ya Kadi

Hayo ni baadhi ya makato wanaokata kwenye akaunti milioni 7 ambao ni wateja Hai

So Bank ni wanyonyaji sana mimi ni wakala wateja hulalamika sana
 
Back
Top Bottom