NMB kupata faida inayovunja rekodi zote ya TZS 775 bilioni ni matokeo ya Sera chanya na rafiki za kibiashara za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

NMB kupata faida inayovunja rekodi zote ya TZS 775 bilioni ni matokeo ya Sera chanya na rafiki za kibiashara za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Stanbic na Standard ndo benki bora maana wao hawafanyi kazi na serikali ila faida yao inaeleweka
 
Benki ya NMB lazma wapate faida kubwa kwa sababu kaongeza unyonyaji mkubwa sana kwa wateja

1. Benki ina Makato makubwa sana kuliko Benki zote hasa ukitoa kwa Wakala mfano ukitoa 100,000 kwa wakala wa NMB unakatwa 4500 plus Tozo ya 500 jumla unakatwa 5000 ila CRDB unakatwa 3950 plus Tozo ya 500

2. Uwepo wa makato ya kila mwezi ya shilingi 1800

3. Makato ya kila mwaka ya Shilingi 13900 kwa ajili ya Kadi

Hayo ni baadhi ya makato wanaokata kwenye akaunti milioni 7 ambao ni wateja Hai

So Bank ni wanyonyaji sana mimi ni wakala wateja hulalamika sana
Wako huu ni uongo kutoa pesa NMB is the cheapest
 
Wako huu ni uongo kutoa pesa NMB is the cheapest
Boss nakuomba ukienda kwa wakala angalia Tarrifs za makato kisha linganisha angalia katika zile Board zao wamebandika ukutani angalia CRDB na NMB kisha utaleta mrrjesho
ukitaka Benk Cheap tumia azania, Equity, Exim na DTB hizo ndio Bank Cheap upande wa makato mimi ni WAKALA nina huduma zote ninaongea ninachokiona binafsi natumia Azania Bank na EQUITY ndio ni rafiki
 
View attachment 2891369
Hii ndio taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya NMB PLC,

Binafsi imenivutia na haya moja kwa Moja ni matokeo ya Sera Bora na rafiki za Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan, tunakwenda nae Mpaka 2030.

Hiki ni kiashiria muhimu kinachoonesha kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi sana.
===

Soma taarifa yao hapo chini,

Matokeo ya Kihistoria yenye kugusa maisha ya watu, jamii na uchumi,

Leo, Benki ya NMB tumetangaza matokeo ya kiutendaji ya mwaka 2023, yakionesha kuvunja rekodi kwa mwaka mwingine tena baada ya kupata mafanikio ya kihistoria.

Kati ya mengi, tumeweza:

➡️ Kuongeza Jumla ya mapato ya Benki na kufikia Shilingi Trilioni 1.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 mwaka hadi mwaka.

➡️ Uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato uliboreshwa zaidi hadi kufikia asilimia 39, wakati uwiano wa mikopo chechefu umeshuka hadi kufikia asilimia 3.2. Takwimu hizi zote ni chini ya ukomo wa kikanuni wa Benki Kuu wa asilimia 55 na asilimia 5 mtawalia.

➡️ Kutokana na ufanisi huu, Faida kabla ya Kodi imeongezeka kwa asilimia 26 hadi Shilingi Bilioni 775 huku Faida baada ya Kodi ikifika Shilingi Bilioni 542 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 kwa mwaka. Hiki ni kiwango kikubwa cha faida na cha kihistoria kwa Benki ya NMB na sekta nzima ya fedha nchini.

➡️ Mizania ya Benki imeendelea kukua na kufikia jumla ya mali ya Shilingi Trilioni 12.2 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 19 kwa mwaka.

➡️ Tuliendeleza ajenda ya ujumuishaji wa kifedha kwa kufungua akaunti mpya za wateja zaidi ya milioni 1.2, na kufanya jumla ya akaunti za wateja wetu kufikia zaidi ya akaunti milioni 7.1. Hii ni idadi kubwa zaidi ya wateja kwa taasisi moja ya fedha nchini.

➡️ Tuliwekeza zaidi ya Tsh Bilioni 6 kwenye elimu, afya na mazingira, ikiwa sehemu ya dhamira yetu ya kujitolea kusaidia jamii inayotuzunguka.

Akiwasilisha Taarifa ya Fedha ya Mwaka 2023, Afisa Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna amewashukuru wateja wetu, wanahisa, wafanyakazi, washirika wote wa Benki, Serikali kupitia Benki Kuu na Watanzania wote kwa mchango wenu thabiti na imani mliyonayo kwa Benki ya NMB.

Ahsante kwa kuendelea kutuamini.

#NMBKaribuYako
hivi kuna updates zozote kuhusu nmb scholarship foundation
 
Najua wewe ni mtumishi wa CRDB,

Umeandika mambo mengi sana fine,

But, Nataka unijibu maswali haya,

1. Je, hayo mabenki mengine yanazuiwa kukopesha wafanyakazi hasa wa Serikali?


2. Kama CRDB ni 13% why do them opt kwenda kwenye 16%?

3. Je, wanalazimishwa?

Tukubali tukatae NMB inatoa "the Good service"

"The good service is to provide who or she wants",

Kumpa kile kitu mtu anapenda ndio huduma Bora sio kile wewe unataka,

Huwezi kuzungumzia mafanikio haya bila kumtaja Ruth Zaipuna na Rais Samia Suluhu Hassan
NMB Sasa akaunti ni buku tu
 
View attachment 2891369
Hii ndio taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya NMB PLC,

Binafsi imenivutia na haya moja kwa Moja ni matokeo ya Sera Bora na rafiki za Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan, tunakwenda nae Mpaka 2030.

Hiki ni kiashiria muhimu kinachoonesha kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi sana.
===

Soma taarifa yao hapo chini,

Matokeo ya Kihistoria yenye kugusa maisha ya watu, jamii na uchumi,

Leo, Benki ya NMB tumetangaza matokeo ya kiutendaji ya mwaka 2023, yakionesha kuvunja rekodi kwa mwaka mwingine tena baada ya kupata mafanikio ya kihistoria.

Kati ya mengi, tumeweza:

[emoji3591] Kuongeza Jumla ya mapato ya Benki na kufikia Shilingi Trilioni 1.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 mwaka hadi mwaka.

[emoji3591] Uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato uliboreshwa zaidi hadi kufikia asilimia 39, wakati uwiano wa mikopo chechefu umeshuka hadi kufikia asilimia 3.2. Takwimu hizi zote ni chini ya ukomo wa kikanuni wa Benki Kuu wa asilimia 55 na asilimia 5 mtawalia.

[emoji3591] Kutokana na ufanisi huu, Faida kabla ya Kodi imeongezeka kwa asilimia 26 hadi Shilingi Bilioni 775 huku Faida baada ya Kodi ikifika Shilingi Bilioni 542 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 kwa mwaka. Hiki ni kiwango kikubwa cha faida na cha kihistoria kwa Benki ya NMB na sekta nzima ya fedha nchini.

[emoji3591] Mizania ya Benki imeendelea kukua na kufikia jumla ya mali ya Shilingi Trilioni 12.2 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 19 kwa mwaka.

[emoji3591] Tuliendeleza ajenda ya ujumuishaji wa kifedha kwa kufungua akaunti mpya za wateja zaidi ya milioni 1.2, na kufanya jumla ya akaunti za wateja wetu kufikia zaidi ya akaunti milioni 7.1. Hii ni idadi kubwa zaidi ya wateja kwa taasisi moja ya fedha nchini.

[emoji3591] Tuliwekeza zaidi ya Tsh Bilioni 6 kwenye elimu, afya na mazingira, ikiwa sehemu ya dhamira yetu ya kujitolea kusaidia jamii inayotuzunguka.

Akiwasilisha Taarifa ya Fedha ya Mwaka 2023, Afisa Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna amewashukuru wateja wetu, wanahisa, wafanyakazi, washirika wote wa Benki, Serikali kupitia Benki Kuu na Watanzania wote kwa mchango wenu thabiti na imani mliyonayo kwa Benki ya NMB.

Ahsante kwa kuendelea kutuamini.

#NMBKaribuYako
Akili kisoda wewe. Kama hujui pato la NMB linapandaje nyamaza. Huyo mamako ana nini zaidi ya kutunyonya Watanzania?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom