NMB kupata faida inayovunja rekodi zote ya TZS 775 bilioni ni matokeo ya Sera chanya na rafiki za kibiashara za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Bank kupata faida kubwa ni ishara ya ukuaji wa uchumi kuwa ni WA kuridhísha
Faida wanaipata kwa kufanya biashara na serikali, kukopesha serikali, na kukopesha watumishi wa umma. Hiyo haina msaada wa maana kwenye uchumi wa nchi na watu. Inatakiwa benki ikopeshe kwa wingi biashara na kilimo, ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa ajili ya soko la ndani na exports. Hizi report ni utapeli wa kudanganya watu na shareholders. Ila kwa ground hawana impact kwa wananchi. Zaidi sana kukatakata hela zao.

Hiyo table ndio inaonesha. Kati ya 6T waliyokopesha 3.7T imekopeshwa watumishi. MSE, SME na Kilimo kimekopeshwa hela ndogo.
 
Mfanyabiashara yeyote anaangalia zaidi Biashara yenye risk kidogo,

Sijui kama umeshawahi kufanya biashara
 
Huu ni uongo
 
Najua wewe ni mtumishi wa CRDB,

Umeandika mambo mengi sana fine,

But, Nataka unijibu maswali haya,

1. Je, hayo mabenki mengine yanazuiwa kukopesha wafanyakazi hasa wa Serikali?


2. Kama CRDB ni 13% why do them opt kwenda kwenye 16%?

3. Je, wanalazimishwa?

Tukubali tukatae NMB inatoa "the Good service"

"The good service is to provide who or she wants",

Kumpa kile kitu mtu anapenda ndio huduma Bora sio kile wewe unataka,

Huwezi kuzungumzia mafanikio haya bila kumtaja Ruth Zaipuna na Rais Samia Suluhu Hassan
 
Hapo unapoiona NMB ndio tayari Serikali imeshaondoa deposit zake zote toka enzi za Magufuli,

Ndio maana unaona interms of Liquidity CRDB iko juu but before NMB ilikuwa juu.

NMB kinachowabeba ni Uongozi thabiti tu wa Ms Ruth Zaipuna otherwise yangekuwa majanga kama CRDB
 
Mwendazake ndio alitoa pesa yote ya Serikali kule kwa lugha laini alitaka kuiua kifo Cha polepole


Naipenda sana NMB mpaka naumwa ndio maana familia yangu yote hadi watoto wanaakaunti NMB
 
Huko sasa ni kuleta mambo ambayo hayana uhusiano na kichwa cha habari.

Huu aukuwa mjadala wa CRDB v MNB, hoja ilikuwa kuongezeka kwa faida MNB ni ishara ya kukuwa kwa uchumi. Implying MNB inafaidika na economic activities.

Source ya mapato ya MNB ni; ‘interest income’ ndio sehemu kubwa ya mapato yao na ina uhusiano na biashara yao ya kukopesha (hapo unaweza kuona mchango wao kwenye uchumi).

Source ya pili kwenye kuingiza mapato yao ‘fees and commissions interests’ hii si mikopo ya uzalishaji bali ni mitozo ya wizi. Na source ya tatu foreign exchange aina impact kwenye uchumi if anything ni withdraw.

Sasa basi kwenye hiyo source yao kuu (interest income), ukipekuwa unakuta faida yenyewe sehemu kubwa inatokana na mikopo kwa wafanyakazi, business overdraft na treasury interest; kwa pamoja ni kama 80% ya assets zao zinazozalisha hiyo faida ya interest income.

Wakati sehemu ndogo iliyobakia kama 20% ndio inaenda kwenye mikopo ya uzalishaji kwenye kilimo, SME, Corporates and other consumptions (assuming hizi ni fixed and movable assets).

Based on that info si kweli faida ya MNB inatokana na ukuaji wa uchumi hakuna ushahidi huo, isipokuwa faida yao inategemea kufanya biashara na serikali. Sasa tena CRDB sijui NBC na mambo mengine hayakuwa sehemu ya habari ya upotoshaji inayopingwa kama ilivyowasilishwa na mleta mada.
 
NMB inabebwa na mbeleko ya serikali.
 
Kwani Serikali sindio watu?
Serikali ni viongozi tu, kama NMB wanataka kuendeleza watu ilitakiwa fedha zipelekwe kwenye uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa ajili ya soko la ndani na la nje (exports). Ilipaswa fedha zipelekwe kwenye MSE, SME na Agribusiness.
 
NMB baba lao TZ,
 
Naunga mkono hoja. Kwenye masuala ya uchumi na biashara Rais Samia anafanya vizuri
Hata sasa wazee wa baishara ya Ganda amabyo serikali haioati Kodi imetulipa sana kipindinhiki, hivyo hata benki zinapata faida kwani fedha inaigua kwenye mzyngukonwa benki nakutengeza faida
 
Hata sasa wazee wa baishara ya Ganda amabyo serikali haioati Kodi imetulipa sana kipindinhiki, hivyo hata benki zinapata faida kwani fedha inaigua kwenye mzyngukonwa benki nakutengeza faida
Hizo ngada mnauzia wapi?
 
Benki ya NMB lazma wapate faida kubwa kwa sababu kaongeza unyonyaji mkubwa sana kwa wateja

1. Benki ina Makato makubwa sana kuliko Benki zote hasa ukitoa kwa Wakala mfano ukitoa 100,000 kwa wakala wa NMB unakatwa 4500 plus Tozo ya 500 jumla unakatwa 5000 ila CRDB unakatwa 3950 plus Tozo ya 500

2. Uwepo wa makato ya kila mwezi ya shilingi 1800

3. Makato ya kila mwaka ya Shilingi 13900 kwa ajili ya Kadi

Hayo ni baadhi ya makato wanaokata kwenye akaunti milioni 7 ambao ni wateja Hai

So Bank ni wanyonyaji sana mimi ni wakala wateja hulalamika sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…