Bhizabhityo BB
Member
- Aug 18, 2022
- 7
- 16
Hii ni bondi (hati fungani) ya kwanza kabisa ya Shilingi ya Tanzania kutolewa kwenye soko la hisa la kimataifa. Lakini hii si bondi ya kwanza ya IFC (IFC ni miongoni mwa taasisi za kifedha zilizo chini ya benki ya dunia (World Bank) ya sarafu ya ndani.
Haya ndiyo unayopaswa kujua kuhusu hili;
1. Utaratibu: fedha za bondi → makundi lengwa
Utaratibu upo hivi, ni: Taasisi za uwekezaji huko london zinanunua hizi bond → IFC (mtoaji mwenye AAA, aliyeorodheshwa London, anayelipwa kwa USD) → NMB (mkopaji wa TZS) → Wafanyabiashara Wadogo, wa Kati (MSMEs). Masharti yaliyothibitishwa ya IFC: bondi ya TZS bilioni 262.5 (sawa na Dola za Kimarekani milioni 100) yenye muda wa miaka 5 ina riba ya 7.60% na iliuzwa kwa wawekezaji wa taasisi za Ulaya.
Goldman Sachs International ndiye aliyekuwa "dalali" wa mpango huu.
Malipo yanafanyika kwa Dola za Kimarekani (USD) licha ya hatari (risk) ya thamani ya TZS kwenye riba, maana yake wawekezaji ndio wanaobeba hatari ya kushuka kwa thamani ya TZS kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia riba na urejeshaji wa mtaji, si NMB.
Utoaji huu unasaidia mkopo wa TZS wenye thamani ya Dola milioni 100 kwa NMB Bank Plc kupanua ufadhili kwa Wafanyabiashara Wadogo, wa Kati (MSMEs) kote Tanzania, huku asilimia 20 ikitengwa mahususi kwa MSMEs zinazomilikiwa na wanawake.
2. Historia ya IFC na wanunuzi wake
Katika miaka mitano iliyopita, IFC imetoa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 50 za ufadhili wa sarafu za ndani katika zaidi ya sarafu 60 za masoko yanayoibukia, kupitia utoaji wa umma, mauzo binafsi, bondi za kimaudhui, na bondi za sarafu za ndani (kwa mfano, bondi za Masala za India na Komodo za Indonesia).
Huu pia si mwanzo wa uhusiano kati ya NMB na IFC, IFC ina ushirikiano wa muda mrefu na NMB ikiwemo uwekezaji katika mipango ya bondi za kijinsia na uendelevu za benki hiyo. Kwa hiyo, mpango huu unaongeza uhusiano uliopo badala ya kuanzisha mpya.
Wanunuzi wengi ni taasisi za Ulaya: Taasisi za Fedha za Maendeleo (DFIs) kama FMO, BII, wawekezaji wa ESG na taasisi za pensheni/bima zinazotafuta faida kwenye bondi za AAA kwenye sarafu za masoko yanayoibukia.
3. Makadirio ya riba
Wastani wa riba za mikopo ya benki Tanzania ni karibu 15-16%, na mipango ya NMB yenye riba nafuu iliyowekwa wazi iko chini zaidi ya wastani huo, mikopo ya sekta ya kilimo ina riba isiyozidi 10% kwa mwaka, na mpango wa wafanyabiashara wadogo unaofanywa na serikali una riba nafuu ya 7%.
Ikiwa NMB itafuata mtindo wake wa kawaida, riba inayotarajiwa kwa MSMEs inaweza kuwa kati ya 9-13% (tusubiri taarifa rasmi kutoka NMB).
4. Impact kwa NMB na Tanzania
Kwa NMB: deni la TZS lenye gharama fasta kwa miaka mitano kwa riba ya 7.60% jumla linapunguza kwa kiasi kikubwa gharama ambazo NMB ingelazimika kubeba kama ingekopa kupitia amana/deposits za wateja (muda mfupi, hatari ya kutolingana kwa mali na madeni) au kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) (lenye ukwasi hafifu kubeba kiasi kikubwa cha TZS bilioni 262.5 kwa wakati mmoja). Pia inaimarisha uhusiano uliopo wa bondi za kijinsia na uendelevu na IFC — njia ya ufadhili inayoweza kurudiwa.
Kwa Tanzania: hii ni ushahidi wa malengo ya Dira ya 2050 ya ukuaji unaoongozwa na sekta binafsi — mpango huu pia unaunga mkono juhudi pana za IFC za kuimarisha masoko ya mitaji na kupanua upatikanaji wa ufadhili wa sarafu za ndani. Kwa mtazamo mpana zaidi, huu ni mfano unaothibitisha kuwa bondi za sarafu za ndani zinazotolewa nje ya nchi zinaweza kuvutia mtaji wa kimataifa na kupanua ufadhili wa sarafu za ndani katika masoko yanayoibukia zaidi ya uwezo wa masoko ya ndani.